KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
Mfanyabishara wa mbao anayefahamika kwa jina la Peter Stephano mkazi wa Maji ya chai wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, ameanzisha kiwanda kidogo cha kutengeneza nyumba za kisasa zinazoweza kuhamishwa kwa madai ya kutaka kuendana na maendeleo dunia ya sasa.
Peter akizungumza na GADI TV wilayani humo, amesema wazo hilo amelipata kwa mwanae wa kike baada ya kupita zaidi miaka 20 akiwa anafanya biashara ya kuuza mbao pamoja fanicha mbalimbali.
Aidha, Laura Peter ambaye ni mtoto wa mfanyabishara huyo, amesema wazo hilo aliwasilisha kwa baba yake kwa lengo la kuweka kumbukumbu lakini kwasasa wazo hilo limepanuka na kuwa wazo la kibishara kutokana na watu mbalimbali kuvutiwa zaidi na kuonyesha nia kuhitaji kutengenezewa nyumba za mfumo huo.
Hata hivyo, Laura amesema kwakuzingatia ubora wa nyumba hizo wanatumia mbao zenye ubora wa hali ya juu, na miongoni mwa nyumba hizo zitafungwa tairi ili kurahisisha uhamaji wake.
View: https://www.facebook.com/share/v/19mZ8rks12/