Kuandamana ni mbinu ya kipuuzi sana kutumika hapa kwetu.
Kwanza hakuna mtu anayeona aibu kuona anapingwa kwa njia ya maandamano.Pili kuna watu watauwawa,wataumizwa na kuwa vilema wa maisha,na wengine kufungwa na bado hakuna hata mtu mmoja mwenye uwezo atakayechukua hatua za kutetea watu hao.
Mambo haya ndiyo yanasababisha hawa waoinzani waonekane hawana maana.Maana njia hii ni kama kuwapa nafasi ccm ya kufurahia walichokifanya.Mnataka tu muwape maneno ya kuongea huko bungeni huku mkizodolewa.
Hivi ninyi wapinzani akili huwa mnaweka wapi?Maana tayari kitendo cha ccm kujikuta wako wao peke yao,kimewafanya waanze kufedheheka.Hawana furaha kamwe.Tunaishi nao na tunawasikia.
Maana ushindi wao sio dhidi ya wapinzani,ila ni dhidi ya Tanzania.
Kwa nini msikae kimya kwanza kuliko kuanzisha mapambano sasa?