Pre GE2025 Kutegemea huruma ya Wananchi na kiki kupata umaarufu, kumeanza kuwaumbua Wanasiasa nchini

Pre GE2025 Kutegemea huruma ya Wananchi na kiki kupata umaarufu, kumeanza kuwaumbua Wanasiasa nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Fikra na hali ya Wanasiasa kutegemea madhaifu yao ya kimwili au kiafya kuvutia au kupata huruma ya wananchi, imeanza kuadimika, kutoweka na kupotea kwa kasi sana nchini, huku ikiwaacha wanasiasa husika katika hali ya mshangao, majonzi na simanzi kubwa mno, kwamba hakuna tena hamasa kwa wanachama wao kuwapambania viongozi wao na kusikitika nao pamoja.

Hii inamaanisha kuna mabadiliko makubwa sana katika uelewa na ufahamu wa wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya siasa, uongozi, utawala na maendeleo yao. Wananchi wanahisi kucheleweshwa sana na siasa za aina hiyo.

Taratibu wameanza kujitenga na siasa za umaarufu, kiburi, majivuno, ubishi au uhodari wa mwanasiasa kukejeli au kudharau viongozi wa umma, ama kupambana na Serikali kazini.

Badala yake wametambua kwamba wanahitaji sasa, upinzani wenye siasa za kistaarabu, zenye sera, uelekeo, mipango mikakati mbadala ya maendeleo inayotekelezeka dhidi ya ile inayotekelezwa na Serikali iliyopo madarakani.

Wananchi wanahitaji ukosowaji wa kistaarabu, ukosoaji wenye tija, ukosoaji utakao chochea Serikali iliyopo madarakani kuchangamka katika kutekeleza mipango au ilani yake ya maendeleo kwa Wananchi, ukosoaji wenye kuitia hofu Serikali iliyopo madarakani kwamba ikizembea kutekeleza ahadi zake kwa wananchi, ni dhahiri kuna kitisho cha mipango bora zaidi ya upinzani, huenda wanainchi wakaikataa kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi.

Lakini kwa upinzani uliopo, serikali inafanya kazi zake kwa kurilax, huku kukiwa hakuna kabisa kitisho eti upinzani kuna siku utaaminiwa na kuchaguliwa kuongoza nchi. hakuna.

Wananchi kwa sasa, wanahitaji vibrant opposition itakayochochea uwajibikaji, uwazi, haki, na itakayozingatia usawa katika mgawanyo wa rasilimali na maendeleo, uhuru na amani kwa kila mTanzania, kushiriki kikamilifu katika kazi za kijamii, kiuchumi na kisiasi bila bugdha wala kudeka...

Wananchi hivi sasa wanaelewa kwamba, siasa za Tanzania ni sharti zifanyike kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi, na sio kwa mujibu wa ujuaji na uerevu mwingi wa mtu fulani, anaetafuta kiki, umaarufu binafsi na kuhurumiwa na wananchi ili kusudi eti apate uongozi.

Hata hivyo, siasa zenye viashiria au mipango ya kuhatarisha umoja, amani na utulivu wa wananchi nchini, hazikubaliki, zimepitwa na wakati kufanyika Tanzania. ni vizuri kama Taifa tukazipiga vita kwa pamoja.

Kiki na umaarufu wa udhaifu wa kimwili na kiafya, sio tena kivutio na wala si hoja tena, na kabisaa havitamsaidia yeyote kwa namna yeyote kupata uongozi nchini.

Ni muhimu sana kutumia, sera, mipango mikakati mbadala, kuzingati sheria na katiba ya nchi kutafuta uongozi wa kisiasa 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Watakuja kukuuliza,huu uzi ni blah blah au ni Tlaatlaah Tlaatlaah
ni uhuru na haki ya kila mtanzania kua na maoni na mtazamo huru dhidi ya wengineo,

so,
its completely very fair wakiuliza, wasipo uliza, wakiunga mkono, wasipounga mkono au wakipuuza 🐒

lakini Ukweli si nimeweka wazi bila mbambamba yoyote gentleman 🐒
 
Fikra na hali ya Wanasiasa kutegemea madhaifu yao ya kimwili au kiafya kuvutia au kupata huruma ya wananchi, imeanza kuadimika, kutoweka na kupotea kwa kasi sana nchini, huku ikiwaacha wanasiasa husika katika hali ya mshangao, majonzi na simanzi kubwa mno, kwamba hakuna tena hamasa kwa wanachama wao kuwapambania viongozi wao na kusikitika nao pamoja...

Hii inamaanisha kuna mabadiliko makubwa sana katika uelewa na ufahamu wa wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya siasa, uongozi, utawala na maendeleo yao. Wananchi wanahisi kucheleweshwa sana na siasa za aina hiyo..

Taratibu wameanza kujitenga na siasa za umaarufu, kiburi, majivuno, ubishi au uhodari wa mwanasiasa kukejeli au kudharau viongozi wa umma, ama kupambana na Serikali kazini,

Badala yake wametambua kwamba wanahitaji sasa, upinzani wenye siasa za kistaarabu, zenye sera, uelekeo, mipango mikakati mbadala ya maendeleo inayotekelezeka dhidi ya ile inayotekelezwa na Serikali iliyopo madarakani...

Wananchi wanahitaji ukosowaji wa kistaarabu, ukosoaji wenye tija, ukosoaji utakao chochea Serikali iliyopo madarakani kuchangamka katika kutekeleza mipango au ilani yake ya maendeleo kwa Wananchi, ukosoaji wenye kuitia hofu Serikali iliyopo madarakani kwamba ikizembea kutekeleza ahadi zake kwa wananchi, ni dhahiri kuna kitisho cha mipango bora zaidi ya upinzani, huenda wanainchi wakaikataa kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi..

Lakini kwa upinzani uliopo, serikali inafanya kazi zake kwa kurilax, huku kukiwa hakuna kabisa kitisho eti upinzani kuna siku utaaminiwa na kuchaguliwa kuongoza nchi. hakuna.

Wananchi kwa sasa, wanahitaji vibrant opposition itakayochochea uwajibikaji, uwazi, haki, na itakayozingatia usawa katika mgawanyo wa rasilimali na maendeleo, uhuru na amani kwa kila mTanzania, kushiriki kikamilifu katika kazi za kijamii, kiuchumi na kisiasi bila bugdha wala kudeka...

Wananchi hivi sasa wanaelewa kwamba, siasa za Tanzania ni sharti zifanyike kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi, na sio kwa mujibu wa ujuaji na uerevu mwingi wa mtu fulani, anaetafuta kiki, umaarufu binafsi na kuhurumiwa na wananchi ili kusudi eti apate uongozi...

Hata hivyo, siasa zenye viashiria au mipango ya kuhatarisha umoja, amani na utulivu wa wananchi nchini, hazikubaliki, zimepitwa na wakati kufanyika Tanzania. ni vizuri kama Taifa tukazipiga vita kwa pamoja...

Kiki na umaarufu wa udhaifu wa kimwili na kiafya, sio tena kivutio na wala si hoja tena, na kabisaa havitamsaidia yeyote kwa namna yeyote kupata uongozi nchini ..

Ni muhimu sana kutumia, sera, mipango mikakati mbadala, kuzingati sheria na katiba ya nchi kutafuta uongozi wa kisiasa 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Unazungumzia wananchi kama wananchi au polisi-ccm?
 
Back
Top Bottom