Samahani
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 221
- 335
Wakuu,
Pamoja na ukweli kuwa kipato katika jamii kinatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, lipo jambo la kushangaa kila ninapowaona wakulima!! Haiingii akilini kuona kwamba, kuna waajiriwa ambao pia ni wajasiriamali wanaoishi hasa mijini, ambao mapato yao katika mwezi kwa wastani ni kati ya MILIONI MOJA mpaka MBILI. Hawa, katika Mwaka, wana uhakika wa kutengeneza kipato mpaka kufikia Milioni 12 au zaidi.
Lakini wengi kati ya hawa, wanalalamika kuwa MAISHA NI MAGUMU, MAISHA YAMEPANDA!!
Wala sipingani nao, hata mimi ni mmoja kati ya ambao kila kukicha nakiri, HERI YA JANA KULIKO LEO!!
Lakini ajabu ni kuwa, ninao NDUGU, JAMAA na MARAFIKI, ambao wanaishi Vijijini. Hawa, Shughuli pekee wanayoitegemea katika mwaka mzima ni KILIMO, tena CHA JEMBE LA MKONO..
Napata sana shida kujua, ni kwa namna gani watu hawa wanaweza kuuona tena kila MWAKA MPYA, au kuusubiri tena kila msimu wa kilimo huku WAKITEGEMEA KILIMO CHA JEMBE LA MKONO PEKE YAKE!!!
Tena basi misimu inatofautiana. Kuna misimu wanavuna sana, lakini kuna misimu inakuwa migumu kwao. Sasa fikiri mtu ambaye msimu umemwendea mrama, akauza vyote alivyopata, akapata MILIONI MBILI au wakati fulani pungufu ya hapo, tena kwa mbinde sana.. Mtu huyu anafikia vipi msimu unaofuata???
Lakini wakati mimi nawaza haya, Kuna mkulima wala halalamikii ugumu wa maisha pamoja na ukweli kuwa, kwa mtazamo wangu, namwona akiwa anakabiliwa na hali tete ya kiuchumi!!
Hii inanilazimu tu kukiri kuwa, KUTEGEMEA KILIMO PEKE YAKE KUNASHANGAZA MNO!!