Habari mkuu,
Kwa nini tunacheka tukitekenywa?
Kwa kawaida kuna aina mbili za kucheka, mosi ni kile kicheko cha kawaida ambacho hutokana na mabadiliko ya empotions na pili kuna kicheko kisababishwacho na kutekenywa.
Utofauti wa vicheko hivi unaonekana zaidi katika activities za ubongo wa mwanadamu pale vinavyokuwa vimetukia.
Vicheko vyote viwili vinasababisha sehemu ya ubongo iitwayo 'Rolandic Operculum' kuwa activated, hata hivyo kichekesho kisababishwacho na kutekenywa huenda mbali na kuactivate 'hypothalmus', ogani hii husababisha either 'fight' au 'flight'..
Watafiti wa tabia za binadamu wanaamini kuwa, kitendo cha kutekenya huamsha sehemu ya ubongo ambayo kazi yake ni kutafsiri maumivu au kujihami na maumivu. Ndio maana unapojaribu kuelekeza mkono wako ili umtekenye mtu iwe kwa makusudi au bahati mbaya, basi mtu yule hujikwepesha au wakati mwingine hukimbia.
NB:
Maelezo mengine yote ni nyama, kwa ufupi jibu la swali lako lipo katika maandishi mekundu.