Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,914
- 168,320
Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, amemwaga povu zito akilaani vikali utekaji, utesaji na ukatili aliofanyiwa kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kazungu Bakari, huku akitahadharisha kuwa wimbi hilo la kihalifu linaiweka nchi kwenye taswira mbaya mno kisheria na kimataifa.
Kupitia taarifa yake iliyotoka leo, Agosti 9, 2026, katika mitandao ya kijamii, Ado Shaibu amefunguka kusikitishwa kwake na kitendo hicho cha kinyama dhidi ya Kazungu kada anayetambulika kwa msimamo wake thabiti wa kuikosoa Serikali na CCM mtandaoni na kulitaka Jeshi la Polisi kuwasaka na kuwachukulia hatua watesaji hao.
"Habari ya kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa Kada wa CCM Kazungu Bakari anayefahamika mitandaoni kwa kauli zake za ukosoaji kwa Serikali na CCM inahuzunisha. Ninakemea kitendo hiki kwa nguvu zote na kutoa rai kwa Jeshi la Polisi kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya waliohusika. Kwa hakika, vitendo hivi vinaharibu taswira ya nchi yetu," amesema Ado Shaibu.
Kauli hii nzito kutoka kwa Mbunge Shaibu inadhihirisha kuwa ukatili wa utekaji na kuteswa kwa wakosoaji sasa umevuka mipaka ya vyama vya upinzani na kugonga hodi hadi ndani ya chama tawala, jambo linalotishia msingi wa amani na utawala wa sheria nchini.
Ado Shaibu amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi lina wajibu wa kisheria na kimaadili kuendesha uchunguzi wa haraka na wa wazi ili kuwatia nguvuni wote waliohusika na unyama huo, akionya kuwa kuendelea kufumbiwa macho kwa matukio ya aina hiyo kunazidi kuipaka matope taswira ya nchi kote duniani.