Kutelekezewa mimba VS kubambikiwa mtoto

Kutelekezewa mimba VS kubambikiwa mtoto

Mi naona hii ni mbwaimbwai....mwaga mboga nimwage ugali....anaumizwa mwanamke anaumizwa mwanaume....Yaan hapo kati Yao Kuna Kuna kakarma kametulia.Huna hatia unatelekezewa mimba ....huna hatia unabambikiwa mimba.
Aisee,Kaz iendelee
Kamwe ushindani wa maovu ni ujinga usio na maana, hasa kwanchi ya ulimwengu wa tatu. Hasa kwahaya uliyoyataja, unajua kwanini nakwambia hayo, yote hayo humuumiza mtoto vibaya sana kwakuwa nchi za ulimwengu huu haina uwezo wa kulea watoto wa mitaani au kuwasaidia familia zenye mlezi mmoja mmoja hasa kwaupande wa mama. Ushindani huu utapelekea anguko la jamii vibaya sana kwasababu kwa wenzetu jamii maadili yamekufa kabisa ila kwao wanasystem zakusaidia kulea watoto waliotelekezwa au mzazi mmojammoja. Vyote hivi unashindania kumuona nani ni bora kwenye uzinzi nanani anaweza kumkomoa mwenzake kati ya Me na Ke. Tutaanguka vibaya sana Kwakuwa asilimia ya watanzania wanaojiweza haifiki hata asilimia 40 ya total population. Hii imekuwa reflected na kushindwa kupatikana kwa bima ya afya kwawote kwakuwa watanzania walishindwa kabisa kufikia bei iliyopangwa kulipwa kwaajili ya kulipa kila mwaka. Mwisho wa yote kila mtu ataubeba msalaba wake ila nchi itaanguka kiuchumi vibaya sana ikianza kuhudumia hilo kundi. Ishini kwa akili.
 
Back
Top Bottom