muuza ubuyu
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 3,539
- 3,551
Habari wakuu, mimi naishi mkoani (kanda ya ziwa). Wiki ijayo ninakwenda Dar kwa ajili ya shughuli zangu binafsi. Katika huo muda nitakaokuwepo, nitakuwa na muda wa free hivyo natamani kupata namna ya kuutumia. Mimi ni mtu ambaye nataka kuwekeza katika mradi wa kuku wa mayai/nyama, ningeomba yeyote anayefanya biashara hii (hasa wa mayai) kuanzia elfu moja kwenda juu na kwa njia ya kisasa (cages) anikaribishe ili ikiwezekana nije kupata mawili matatu.
Lakini pia hata yule anayefanya biashara ya kusaga unga wa mahindi na ku package (asiwe wale wenye viwanda vikubwa, hapana, nahitaji mjasiliamali wa kati tu) nitashukuru sana. Hizi projects ni projects za ndoto yangu na ninaona muda wa kuanza kuzifanya ni huu na hivyo kuanza kwa kuona na kuuliza maswali mawili matatu basi nitafurahi sana.
Asanteni sana, na karibuni.