Kutembeza bidhaa kwa gari

Kutembeza bidhaa kwa gari

Ziltan

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2011
Posts
2,672
Reaction score
6,880
Habari wadau

Nafikiria kufanya biashara ya namna hii. Yaani nachukua bidhaa kama nguo za watoto. Simu ndogo hizi na accessories zake. Nazunguka kwenye masoko na vijiwe kuvinadi kwa kutumia mziki mkubwa. Naombeni mawazo yenu kwa ujumla, changamoto, maboresho nk.

Karibuni
 
  • Thanks
Reactions: amu
Inalipa iyo biashara lakini hujasema unataka uifanyie kazi wapi? Mjini au vijijini?

Vijijini inalipa 80%nina uhakika nisemalo.

Alafu unavyoanza biashara jitahidi kupunguza gharama za huendeshaji ili uweze kujua faida na hasara kutumia gari kuzungusha sijui labda ni mtaji kiasi gani lakini naziona izo gharama za gari zitakusumbua kwa kuanzia.

Tafuta njia isiyo na gharama na nafuu kuwafikia wateja wateja mpaka baada ya mwezi 1 na zaidi ili ujue unafanya mauzo kiasi gani hapo utachanganua vizuri mapato na matumizi.
 
  • Thanks
Reactions: amu
zaid nalenga maeneo ya vijijn/pembezon mwa mji peny uhaba wa hudum'
gari nimefanikiw kumilik succeed/ probox
kanabana mafuta kias'
hivyo tu mkuu.
npo geita
okay,ni sawa hongera kama kama umelenga vijijini,changamoto yake kubwa ni mzunguko mdogo kwa baadhi ya maeneo,kivipi?

Ni kwa sababu wengi ni wakulima kuna kipindi cha kilimo kikifika kila kitu kinasimama hata biashara haziendi vizuri watu wanalima kwanza biashara itafufuka baada ya mavuno kwaiyo itakuwa ni biadhara ya msimu hadi msimu,tafuta vijiji wanaolima mazao ya biashara mf. Mpunga, pamba, ufuta, mahindi,alizeti,korosho n.k huwa wanakuwa pesa chakufanyia hawajui utapiga pesa mpaka utashangaa.

Kipindi ambacho unasubiri msimu kijijini uchangamke ukawachukulie pesa za kununua gari lingine basi zungusha mjini angalau utaokoa kitu nako wa hali ya chini na washamba washamba watakuwepo tu.

Punguzo ya bei kwenye bidhaa zako iyakufanya ufanye mauzo makubwa kwa mda mfupi.
 
sawa Mkuu.
ila mbal na bidhaa nilizotaja'
bidhaa gan unahic zinaweza kufaa zaid'
Mkuu,
kwa kuanzia ni bora hizo hizo,simu batani kama smart basi ni zile zisizidi laki 2 si unawalenga wanakijiji.
Na nguo za aina zote sio za watoto tu adi akinamama mfano kanga vitenge na viatu rahisi ambazo mtu wa kujijini ataweza kununua,
Utaongeza bidhaa ingine kutokana na uhitaji wa wateja wako kuna vitu watakuuliza unaweka kumbukumbu safari ijayo unawaletelea hivyo tu.
 
Hii ni nzuri kwa Bidhaa hasa za vyakula mkuy, vitu vya kula, kitu kama simu ni vitu ambavyo mtu ili anunue lazima ajipange sana tofauti na vyakula.

Weka vyakula na hasa ambavyo huwa ni scarcity eneo fulani,
 
Back
Top Bottom