Kutengeneza raw mango pickle nyumbani

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Mahitaji

1)Embe bichi kubwa 1 au ndogo ndogo 4

2)Chumvi 2 tablespoon

3)Pilipili ya unga 1 tablespoon

4)Mdalasini wa kijit- 1 kijiti

5)Karafuu 1 (sio lazma)

6)1/2 Kijiko cha chai cha uwatu usiosagwa (uwatu-fenugreek)

7)Paprika 1/2 teaspoon au tandoor masala

8)Chupa ya kuhifadhia mango pickle yako

9)Mafuta ya kupukia 5 tablespoon

Namna ya kutaarisha

1)Osha embe na katakata vipande vidogo vidogo viwe square

2) Weka chumvi katika sufuria kaanga hadi iwe golden brown (usiweke maji)....wacha ipoe

3)Pasha mafuta moto then wacha yapoe kidogo...then add paprika,pilipili,bizari na viungo vyote.....changanya vizuri.....

4)Weka chumvi, na maembe changanya vizuriii

5)Wrap mchanganyiko wako then funika acha ikae overnight ili embe ilainike....

6)Siku ya pili tayari kwa kutumia....plz pendelea kuiweka juani ili embe ilainike vizuri zaid (sio lazima)....


 
Lengo la kuikaanga chumvi ni ili mango pickle yetu ikae mda mrefu bila ya kuharibika

Aksante mpenzi maana mie napenda mapishi si unajua tena na mwezi huo wa Ramadhani lazima tubuni ftari mpya nitakuwa nakuchek sana mpenzi
 
Hizo pics hazipo clear #amu ila hiyo ya juu ni kama mixer ya keki
 
Reactions: BAK
Yaani we somo kiboko, jana tu nlikuwa nawaza mango pickle hadi mate yalikuwa yanantoka...

Halafu hivyo viungo maembe unachanganya wakati mafuta yapo jikoni au wakati ushayaepua.
 
Hizo pics hazipo clear #amu ila hiyo ya juu ni kama mixer ya keki

Achana ya mixer ya cake naongelea hiyo inayopika mikate ya ufuta juu na chini.
Machine hiyo ya kuchoma mikate ya ufuta
 
Yaani we somo kiboko, jana tu nlikuwa nawaza mango pickle hadi mate yalikuwa yanantoka...

Halafu hivyo viungo maembe unachanganya wakati mafuta yapo jikoni au wakati ushayaepua.


Nooo mafuta ukishaepua unaacha yapoe kidogo ndio unachanganya
 
Reactions: BAK
Achana ya mixer ya cake naongelea hiyo inayopika mikate ya ufuta juu na chini.
Machine hiyo ya kuchoma mikate ya ufuta


Siijui hiyo shoga.......
 
Reactions: BAK
Thanks kwa kutupatia ujuzi da Faa.

Ila mimi sipendi mafuta mengi jee itawezeka nipunguze au ntaharibu mapishi?
Mana hata Ile ya kununua nliacha kutumia coz of mafuta mengi.
 
Ndizi mbichi na nyama au utumbo wee!!!

Mmmh jamani utumbo mtamu ila una harufu acha tu nlinunua tena ule ulokua bleached na hauna harufu kali kama ule wa kawaida loh nyumba zenyewe hizi kila kona mkanuka utumbo nimefanya mdalasini ku elimate odors wapiiii nkaweka udi na ubani kidogo afadhali nautamani ila harufu yake yanichosha
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…