Kuteswa kwa Kibanda: Ridhiwani na Nape matatani!

Kuteswa kwa Kibanda: Ridhiwani na Nape matatani!

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,423
Reaction score
3,297
TUKIO la kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa vibaya kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Absalom Kibanda usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii, limechukua sura mpya baada ya mtu aliyejitambulisha kama Ridhiwani Kikwete akitumia ukurasa wake wa mtandao wa facebook kutoa maneno ya kejeli, akihoji kama nae ametekwa na Ikulu.

Mbali na Ridhiwani, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye,naye alitumia mateso ya Kibanda kufanya propaganda chafu, akitoa kauli inayoonesha "anawajua" waliomtesa.

Ridhiwani aliandika: "Je, hii nayo ni kazi ya Rama (Afisa Usalama wa Taifa) wa Ikulu?"

Rama Ighondu ndiye alitajwa na MwanaHALISI kuhusika na mateso ya Dk. Steven Ulimboka mwaka jana.Kauli hii ilichefua kwa kiwango kikubwa viongozi wa juu wa New Habari, kampuni anayofanyia kazi Kibanda, kiasi cha kumfanya Afisa Mtendaji Mkuu, Hussein Bashe,kuhoji chanzo chake.

Bashe ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM, alikwenda mbali zaidi na kuandika maneno makali dhidi ya Ridhiwani:"Huwezi kuleta kebehi ya namna hii. Inaonyesha namna gani hufahamu nafasi yako katika jamii.

Funga mdomo kabisa kwa sababu unajaribu kutukana hisia za watu."Futa kauli yako ya kijinga ya namna hii, hatuwezi kuvumilia kebehi ya kiwango kikubwa namna hii; umelewa madaraka ya kuwa mtoto wa rais, na kudanganywa na hayo mageti ya ikulu, na kudhani unaweza kuleta kebehi na dharau zako katika kila jambo…

"Nakuonya iwe mwanzo na mwisho;usilete kebehi katika jambo hili.Nakuonya, nakuonya, nakuonya usijaribu! Tumekaa kimya…"

Tangu Ighondu alipotajwa na MwanaHALISI kuhusika na utekaji wa Dk. Ulimboka, serikali haijamkamata wala kumhoji. Kauli ya jana ya Ridhiwani kuuliza kwa kejeli kama Kibanda naye aliteswa na watu wa Ikulu, imeibua upya hisia mchanganyiko kuhusu sakata hilo, huku watu wengine wakisema mtoto huyo wa rais anamponza baba yake kwa kutokujua wapi atoe kauli gani.

Baadhi ya waliozungumza na gazeti hili wakionesha kukerwa na kauli ya Ridhiwani, walisema mtoto huyo wa rais anafurahia mateso ya wananchi kwa sababu hajui shida zao, na amelewa madaraka yasiyo yake.Wengine wanaojua kuwa Kibanda alimfundisha Ridhiwani alipokuwa anasoma Shule ya Sekondari Shaaban Robert, Dar es Salaam,walisema hii ni dharau na kejeli iliyopitiliza, inayofanana na ukatili.

Mmoja wao alisema kauli ya Ridhiwani inatokana na kujua udhaifu au upendeleo wa serikali,na kwamba baba yake (rais) hawezi kumchukulia hatua. Wapo pia waliofikia mahali wakasema: "Mtoto huyu kuna kitu anakijua…au kuna kitu anajaribu kuficha." Katika hali isiyokuwa ya kawaida.

Nape naye alitumia ukurasa wa facebook kulijadili suala hili katika muktadha wa kipropaganda, akitaka kuwahusisha watu kadhaa bila kuwataja majina.

Aliandika hivi: "Hili la kutekwa na kupigwa na kuumizwa kiasi hichi (hiki) kaka yangu Kibanda, kila nikilitafakari maneno ya waliosema hakutatawalika na makala za Kibanda mbili au tatu za mwisho kabla ya kuhama chombo cha habari kabla ya anachofanyia kazi sasa vinajirudia kichwani mwangu sana!"

Kauli hii inaakisi maoni kadhaa yanayosambazwa tangu juzi katika maeneo na mitandao kadhaa,yakiwanukuu baadhi ya makada na mashabiki wa CCM ambao wanasema wanalenga kuinusuru serikali isihusishwe na tukio la kutekwa kwa Kibanda.

Huku wakijua kuwa Kibanda aliacha kazi Free Media na kuhamia New Habari kwa hiari yake, kama mwajiriwa yeyote, kama alivyowahi kuacha kazi New Habari, na Mwananchi kabla hajajiunga na gazeti hili, Nape na wenzake wamediriki kupandikiza propaganda kwamba kuteswa kwake kuna mkono wa mwajiri wake wa zamani.

Gazeti linajua, na Kibanda anajua,kwamba hana uhusiano mbaya na mwajiri wake wa zamani, bali amekuwa akiwindwa na kuandamwa na watu wenye mamlaka makubwa sana katika nchi hii kwa muda mrefu kwa sababu za msimamo wake wa kisiasa katika masuala
kadhaa.

Amepata kuitwa na kuonywa mara nyingi dhidi ya msimamo wake katika masuala ya kitaifa, na hasa kwa msimamo wake na makala zinazoonekana wazi kumuunga mkono kigogo mmoja anayechuana na wenzie ndani ya CCM katika kinyang'anyiro cha urais 2015.

Gazeti hili linajua pia kwamba hata mawasiliano ya simu ya Kibanda na baadhi ya wahariri wenzake (na wa gazeti hili wamo) yanafuatiliwa kinyume na sheria.

Kauli yake mwenyewe juzi akisimulia mkasa huo kwa waandishi wa habari kabla hajapelekwa Afrika Kusini kwa matibabu, inadokeza aina ya watuwaliomtesa.

Kibanda alisema kuwa alimsikia mmoja wa watesi wake aliyekuwa na silaha ya moto akikoki risasi na kisha kumuuliza mwenzake, "afande, tummalize?"

Wananchi waliopiga simu chumba cha habari jana baada ya kusoma kauli za Nape na Ridhiwani walisema nukuu hii ya Kibanda ndiyo inawapa kiwewe watu wanaodhani serikali inaweza kuhusishwa na tukio hili dhalimu.

Mmoja wa waliojibu kauli za Nape na Ridhiwani pale pale mtandaoni,aliandika kwa hasira: "Mna dola na all machineries (taasisi zote)mnashindwa nini kuwakamata na kuwachukulia hatua? Lini mtaacha propaganda za kimisukule? "Mwigulu (anadai) anao mkanda,wewe pia unataka kutuaminisha kuwajua wahaini wa Kibanda. Kama kweli acha upuuzi, peleka maelezopolisi.

Mmeanzisha propaganda za udini, na bado tu hamtuonei huruma tusio na pa kukimbilia?"

Source. Tanzania daima.
 
Nape na riz one wote walipata dv 4 unategemea wataandika nini cha maana. ila ninawasifu waliocomment wamewapa ukweli wao hapohapo!
 
Hii ni kweli haka katoto kana dharau sana,ila kwa jinsi walivomshambulia huko facebook nna imani atajirekebisha
 
Kama hawamo kwenye hii movie kwa nini wabwabwaje? psychologically hawa magamba wanajua kila kitu na bila shaka wanahusika. Iko siku watalia wasisikike.
 
Kibanda kapigwa na wafanyakazi wa IKULU kwa ajili ya misimamo yake dhidi ya UFISADI. Nape na Riz1 hana la kujidanganya hapa!! Dalili zote za watesaji wa ULIMBOKA zipo wazi. NItamuandama Rama IGHONDU hadi atakapohojiwa!! usalama wa taifa uliogeuka UHASAMA wa RAIA TZ. Wananchi sasa tujitambue tuko peke yetu! walinzi wetu ndio maadui zetu. Ukihoji dola unatumbuliwa kucha na kuvunjwa meno!! We are alone!! hatuna walinzi!! Tutafakari-----
 
Na hii pia lazima ile kwao baada ya hapo baba anafungia gazeti, akienda safari ethiopia anasema wamechochea serikali,
 
Dear Leisure Class: When the revolution comes you will no longer be able to live off the interest from daddy's money!
 
Tumeamua wenyewe kwa hiari yetu kuchezewa uhai wetu na taifa letu kama mtu anavyocheza na shilingi kwenye tundu la chooni!

Hivi tumeamua kuwaacha wafanye wafanyalo?

Yaani wapuuzi wachache wanatugeuza wajinga namna hii! yaani mtu ana uhakika hatuna la kumfanya! tunaitwa kelele za mlango!!!

ipo siku mawe yatatusaidia kupiga kelele!!
 
Rais wetu ndio anayetakiwa kuwa mkali kwa familia yake na kuwaeleza wanamweka mahali pabaya kama kiongozi wa nchi.Labda kama hili hawalielewi.Unless kama Urais wake ni wa Familia yake.
 
kama hawamo kwenye hii movie kwa nini wabwabwaje? Psychologically hawa magamba wanajua kila kitu na bila shaka wanahusika. Iko siku watalia wasisikike.
the one who hires the investigatives should be included in the list of suspects,
 
Kibanda kapigwa na wafanyakazi wa IKULU kwa ajili ya misimamo yake dhidi ya UFISADI. Nape na Riz1 hana la kujidanganya hapa!! Dalili zote za watesaji wa ULIMBOKA zipo wazi. NItamuandama Rama IGHONDU hadi atakapohojiwa!! usalama wa taifa uliogeuka UHASAMA wa RAIA TZ. Wananchi sasa tujitambue tuko peke yetu! walinzi wetu ndio maadui zetu. Ukihoji dola unatumbuliwa kucha na kuvunjwa meno!! We are alone!! hatuna walinzi!! Tutafakari-----

Ukiwa na imani ya kuwa mungu yupo basi kuwa na imani pia mtetezi wetu yupo,anahesabu siku tofauti na binadamu.Zikifika za arobaini basi atafanya atakachoona inafaa.Kwenye vitabu vyote vya dini kuna mistari inayoonya viongozi wa dunia hii.Usiwe na wasiwasi mtetezi wetu yupo tumuombe tu.
 
Kama kweli kauli iliyoandikwa kwenye habari hii imetolewa na Rizone basi ni dhahiri kuwa awamu hii tuna rais aliyebinafsisha ikulu kwa famila yake, kama ilivyokuwa kwa Saddam Hussein na kina Yundai na Udai. Na ikiwa sii hivyo basi toto la mheshimiwa litakuwa linabwiya unga.
.
 
Back
Top Bottom