Kutetemeka kwa usukani Gari ikifika 75 -85km/h Noah

Kutetemeka kwa usukani Gari ikifika 75 -85km/h Noah

Toa Auto pilot.. Weka Nose Down. Ikitulia rudi kwenye Cruising attitude yako... Ila usiweke tena Auto pilot. Inaonekana speedmeter ina tatizo.
Outo Pilot? For Noah!? This is crazy!
Ukishindwa vyote badilisha rims... Za mbele weka nyuma za nyuma weka mbele.. Niliwahi kuhangaika sana na Tatizo kama hilo ila ufumbuzi wake ukawa ndio huo baada ya kwenda kwenye garage moja ya mturuki pale Tankbovu! Na ni kweli maana siku chache zilizopita nilichomekewa na 124 nikajikuta napiga bega la barabara na kupasua tairi pale pale, nilipotoka pale nikafunga tairi nyingine kimbembe cha kushake kikaanzaaa... Doooooh... Nilipata shida mno mpaka kuja kupata ufumbuzi na ndo hapo nikakumbuka kua niligonga!!!
 
Plugs
Coil
Exhause imetoboka
Pump ya mafuta
tank lina uchafu

hivyo vyote vinapelekea gari kutumia nguvu nyingi kuchoma mafuta
Siyo lazima na wewe uchangie, kwani ukinyamaza ukawaachie wajuvi wa mambo hayo utapungukiwa na nini?
 
mnamchanganya yaani kila mtu anasema lake sasa mnataka gari zima libadilishwe vifaa[emoji39][emoji23]
 
Hapa gereji,au ukijua ufanye nini,tatizo la watanzia kila mtu kutaka kujua kazi ya mwengine kisha mna lalamika biashara ngumu
 
Siyo lazima na wewe uchangie, kwani ukinyamaza ukawaachie wajuvi wa mambo hayo utapungukiwa na nini?
We DAB kweli mnakariri sana ndo tatizo la watanzania ukishapata kipaso chako unajiona expeeeeert mjaribu na kugoogle basi

unadhan naongea kitu kwa kufikiria masharubu? ni sababu nishakutana na tatizo kama hilo nancauses zilikua hizo
 
Ila muhimu nenda service. Sio kubadilidha tu oil!! Check na ball joints zote . tyre rod end
 
Sasa mkuu kama ukiiwasha tu gari inatetemeka hapo tatizo sio wheel balance au stealing!
Tatizo hapo Ni AMA silencer iko juu sana AMA engine mounting!! Engine kama haikukaa Vizuri kwenye mounting itasababisha gari itetemeke kwasababu engine haijatulia
Check Pump au engine mounting...
 
Ya kwangu inatia sauti ya iiiiiiii
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] .... nimecheka kwa sauti, hiyo ni gearbox mkuu, inarudi kwao , wazungu wanaondoka taratibu..... mara nyingi utasikia kwa gari za fito (manual transmission ●)
 
Kaifanyie wheel balance & wheel alignment, Hilo tatizo litaisha
Vile vile angalia pressure ya upepo kwenye matairi yako. Iwapo tairi moja halina pressure ya kutosha hata kama kila kitu kingine kiko sawa bado utapata usumbufu huo.
 
Khaaa.....kweli kazi imemkuta fundi.

Umenikumbusha dada mmoja yeye alisikia propeller ni kifaa cha gari. Basi tatizo kidogo likitokea lazima aulize sio propeller kweli?? hata kama gari limegoma kuwaka yeye ni propeller tu.

Nimecheka 😀😀😀 sana aisee....
 
Back
Top Bottom