Kuteua watu kabla ya kuwajulisha: Wapi kwingine duniani wanafanya hivyo?

Kuteua watu kabla ya kuwajulisha: Wapi kwingine duniani wanafanya hivyo?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Leo/ jana Rais Samia kafanya tena ile kazi aiwezayo vizuri: kateua na kutengua baadhi ya watumishi wa serikali.

Ila safari hii yawezekana kaandika rekodi ambayo haijawahi kuandikwa duniani [nasimama kusahihishwa endapo nitakuwa nimekosea].

Kateua mtu ambaye keshakufa!

Hii ni aibu sana. Ni ishara inayoonyesha tunaongozwa na watu wasio makini kabisa.

Baadhi yetu tumeshaizungumzia hiyo tabia ya kuteua watu bila hata ya kuwajulisha na watu hao wanakuja kujua juu ya hizo teuzi zao kupitia mitandao ya kijamii au vyombo vya habari.

Binafsi nilianza kuiona hiyo tabia kipindi cha Rais Magufuli. Rais Samia naye naona anaiendeleza hiyo tabia kwa ari maradufu na kilele chake ndo hizi teuzi mpya!

Miaka 4 iliyopita tulijadili hiyo tabia.

Modus operandi ya Rais Magufuli ni ya ajabu!

Baada ya Rais Samia kuingia madarakani, tukalijadili tena hilo suala.

Mtu Pekee aliyekataa teuzi wakati wa Magufuli ni ndugu Maswanya

Mwaka jana napo tukaendelea kulijadili suala hilo hilo!

Kuteuliwa na mamlaka za nchi ni heshima kubwa, anayekataa basi kuna maovu anataka kuficha kwenye nafasi aliyo nayo

Leo tena/ jana suala hilo hilo limejirudia!

Wanateuliwa mpaka waliokufa.

Mbona ni jambo rahisi sana….ingalikuwa wateuliwa wanajulishwa kabla ya kuteuliwa kwao, aibu kama hizo za kuteua watu waliokwishakufa zisingekuwa zinatokea.

Just a simple phone call to the person letting them know ‘hey, I’m thinking of appointing you to this or that position, what do you think’?, would prevent all this embarrassment.

Bumboclats….

Pia soma:
 
halafu tunaambiwa urais ni taasisi mbona tunatukanwa hivi... naandika nafuta naandika tena nafuta ngoja niache tu nisijejikuta mikononi mwa nunda!
Ni kama vile hiyo taasisi haina hata mtu mmoja mwenye common sense!

Sijawahi kabisa kuielewa hii dhana ya kuteua watu bila hata ya kuwajulisha!
 
Kuna mtu mmoja alikua kana ya ziwa huko anaitwa nyani ngabu na mwingine kanda ya kasikazini

Uyu wa kanda ya ziwa alikwenda wazir mkuu ziarani uko jamaa alivofanya maandaliz na ukalimu pm akamkubali sana na kumwambia anafaa kusaidia kazi nyingine akachukua jina lake akasepa.....

Within days si mkeka ukatoka nyaningabu ndan si yule wa kasikazin akawahi kwenda kula kiapo mzee lkn mlengwa Ali kua uyu wa kwetu 😅😅

Mpaka hapo nikajua protocol ya ikulu Hamna kitu aisee
 
Nimepata shida kuelewa ulichokiandika.
 
Mtu alishasema ndoto yake ilikuwa awe muhudumu wa kwenye ndege .

Shule ikamshinda kidato cha nne akapiga Bashite akaamua aolewe mke wa 4 akiwa na miaka 18

Do you expect anything tangible from her?
 
Hapa shida sio Samia. Shida ni timu yake hasa aliyesaini huo mkeka yaani Katibu Mkuu Kiongozi
Huwezi kusuka timu yako vizuri kama wewe pia haupo vizuri.

It a simple Maths hayo majina alipoletewa angeweza kujiridhisha lwa kuwatafuta mmoja mmoja na hapo ndio angejua ukweli.

Hii ni sign tosha wengi sana wanapachikwa uongozini kwa "vimemo" so yanatokea sio bahati mbaya ndio uhalisia.
 
Hapa shida sio Samia. Shida ni timu yake hasa aliyesaini huo mkeka yaani Katibu Mkuu Kiongozi
Yeye ndo anachagua watu wa kuwepo kwenye hiyo timu yake.

Kwa mtaji huo, shida ni yeye. Hawezi kukwepa lawama.

Mtu makini huchagua wasaidizi walio makini.

Lakini pia, mtu makini hawezi kukubali jina lake liwe linatumika kiholela holela tu bila ya yeye kuhusika na kuhakiki linatumika kwa heshima.
 
Huwezi kusuka timu yako vizuri kama wewe pia haupo vizuri.

It a simple Maths hayo majina alipoletewa angeweza kujiridhisha lwa kuwatafuta mmoja mmoja na hapo ndio angejua ukweli.

Hii ni sign tosha wengi sana wanapachikwa uongozini kwa "vimemo" so yanatokea sio bahati mbaya ndio uhalisia.
Kusema ukweli kuna shida kubwa sana kwenye Ofisi kubwa (Ikulu)

Kuna mambo yanatokea yanakufanya uwaze na kufikiria mengi sana

Vyovyote vile! Turudi kwenye meritocracy! Watu wapate nafasi kwa uwezo wao na uzoefu mkubwa kwenye eneo husika na sio vinginevyo.

Vinginevyo yajayo yatatisha sana!

Ndo mana kwa wenzetu ulaya huyo ukikuta CS ni 55+ au 60+, Same to Majenerali, Majaji na Makatibu Wakuu!

Uzoefu wa muda mrefu na uwezo mkubwa wa kiutendaji kila siku ndo vinatakiwa kuwa vigezo vya mtu kushika nafasi fulani.
 
Yeye ndo anachagua watu wa kuwepo kwenye hiyo timu yake.

Kwa mtaji huo, shida ni yeye. Hawezi kukwepa lawama.

Mtu makini huchagua wasaidizi walio makini.

Lakini pia, mtu makini hawezi kukubali jina lake liwe linatumika kiholela holela tu bila ya yeye kuhusika na kuhakiki linatumika kwa heshima.
Yeye anachagua ila wasaidizi wana jukumu la kuhakiki na kujiridhisha ili kuepuka fedheha kwa Kiongozi wao.

Moja ya njia za kuhakiki ni hiyo japo kuwapigia simu at least saa moja kabla wahusika wote ili wa confirm kabla ya Tangazo halijarushwa rasmi hewani.

Kuna shida ya umakini kwenye Ofisi Kuu. Kuna watu wengi sana wasio na exposure, experience ya kutosha na competency.

Ndo mana kiongozi mkuu wa nchi anadhalilika hivi
 
Yeye anachagua ila wasaidizi wana jukumu la kuhakiki na kujiridhisha ili kuepuka fedheha kwa Kiongozi wao.

Moja ya njia za kuhakiki ni hiyo japo kuwapigia simu at least saa moja wahusika wote ili wa confirm kabla ya Tangazo halijarushwa hewani.

Kuna shida ya umakini kwenye Ofisi Kuu. Kuna watu wengi sana wasio na exposure na competency.

Ndo mana kiongozi mkuu wa nchi anadhalilika hivi
Hao wasaidizi wake yeye ndiye kawaweka,hoja ya msingi inaanzia hapo. Hivyo hawezi kukwepa hii fedheha.
Pia kwa mtindo huo inaonekana wasaidizi wake amewaacha huru sana hawamuogopi wala kumheshimu boss wao.
 
Kuna teuzi hadi unashangaa. Hadi huyu

Mfano nafasi za DED. Angalau saivi wameanza kujifunza wanateua Senior Public Servants kwenda kuwa ma DED.

Kuna kipindi walikuwa wanateuliwa watoto wadogo sijui only kwa kuwa yupo UVCCM au anajuana na mkubwa fulani. Ndo mana kulikuwa na very poor performance kwenye halmashauri kwa sababu cheo cha DED ni cha Utendaji na lazima awe na uzoefu wa kutosha Serikalini hasa kujua taratibu za kazi na mambo mengineyo mengi sana.

Kuna muda wapinzani wakisema kuhusu Katiba lazima uwaelewe kwa mambo yanavyofanyika
 
Back
Top Bottom