Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Habari za Sikukuu ya Pasaka!
Moja ya dalili kubwa kuwa taifa fulani halina rasilimali Watu ni kwa kuangalia safu ya viongozi na watawala.
Ukiona Watu wanaoteuliwa ni walewale yanaitwa miaka nenda rudi Watu ni walewale basi sababu kubwa ya jambo hilo ni kuwa nchi Hiyo haina Rasilimali Watu. Tunaposema Rasilimali Watu tunazungumzia watu wenye Tija, ili mtu awe Rasilimali inampasa awe na Tija.
Ndio maana kuna Miti na mitishamba. Miti yenye tija na matumizi ndio huitwa mitishamba.
Sababu ya pili, ni Ufisadi. Hapa nazungumzia kulindana. Únamteua huyu kisha unamuweka pembeni, kisha baadaye únamteua tena. Alafu naye atakuteua akiwa juu yako. Kisaikolojia na kisosholojia, Watu wanaolindana hu-share pia uhalifu.
Wenye Haki hawalindani. Kwa sababu Haki ndio ulinzi wenyewe.
Nchi au taifa linaloteua Watu walewale au kuongozwa na Watu walewale haliwezi kukwepa Ufisadi.
Huwezi kuwa Fisadi sehemu ambayo viongozi au watawala hawajirudii mara kwa mara au wanabadilika badilika.
Kuteuana teuana huunda undugu katika uhalifu.
vyombo vya Dola haviwezi kuwa na nguvu Katiak nchi au taifa linalochagua Watu walewale. Nguvu ya chombo cha Dola itakuwa juu ya Raia wanyonge na watawaliwa.
Kuteuana kwa Watu walewale ni kula Yamini. Kiapo cha damu cha kulindana.
Raia wa kawaida huna uwezo wa kumshitaki kiongozi katika taifa linaloteua Watu walewale. Utaishia kupoteza muda wako na gharama ngumu unaweza kuzipata.
Taifa la viongozi wanaoteuana kila mara yaani wao ni kila siku huwezi kumkuta Kiongozi amefungwa Jela.
Atafungwa na nani? Ni kweli kabisa amefanya kosa na anaweza kukiri hadharani kabisa kuwa kafanya kosa. Lakini nani wa kumfunga?
Hakimu au Jaji? Thubutu!
Vyombo vya Dola? Haupo serious!
Ushaambiwa chombo cha Dola sio chombo cha wananchi. Kipo kwajili ya serikali na sio wewe mwananchi. Hapa nazungumzia kwenye taifa au nchi ambayo viongozi miaka nenda rudi ni walewale.
Taifa la kuteuana walewale huzalisha watumwa, Machawa na waabudu viongozi ili nao waonekane. Ni jamii ya hovyo ndio maana nikasema haina rasilimali Watu.
Haiwezikaniki wala haiingii Akilini taifa la Mamilioni ya Watu ati Watu wawe walewale. Hiyo haiwezekaniki bila sababu hizo hapo juu.
Acha Nipumzike sasa. Nipo Maeneo ya Mlimani City. Karibuni Sikukuu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam