Kuteuliwa na mamlaka za nchi ni heshima kubwa, anayekataa basi kuna maovu anataka kuficha kwenye nafasi aliyo nayo

Mkuu,

1. Speaking of Malecela, Nyerere alitaka kumteua Malecela kuwa PM, Malecela akaambiwa na watu wa system, akafanya bonge la party, kabla hajatangazwa, Nyerere akaona huyu sijamtangaza kafanya party, nikimtangaza si ndo itakuwa balaa? Akaghairi.

Serikali ya Nyerere ilikuwa si tu unapewa taarifa kabla ya uteuzi, bali hata unapopewa taarifa unakuwa bado unaangaliwa.

2. Mimi naona kama vyeo wanataka kuviongezea thamani, basi wateule wangepata hata ka simu tu ka kutoka Ikulu, si lazima itoke kwa rais, mfanyakazi tu wa kawaida wa Ikulu anaweza kupiga simu ku verify kwamba mteule mzima, na rais angependa kujua mtu huyo akipewa heshima ya kulitumikia taifa katika nafasi ya ukuu wa wilaya atakubali?
Majority ya watu wangefurahi sana kupata simu hiyo na inge wa motivate sana kwenye kazi. Ikulu ime miss opportunity kuwa motivate watu hapo.

3. CWT teuzi zimetumika kumaliza migogoro, nimelitaja hapo juu (post #57 na #60). Hili jambo baya kwa sababu kama nafasi ya ukuu wa wilaya ina umuhimu, tunaifanya kama chaka la kumalizia migogoro tu. Kama haina umuhimu isiwepo kabisa.
 
Hiyo ya Malecela ninayoongelea ni tofauti kidogo ingawa nimeisahau kidogo. Nadhani alipata taarifa kupitia kwenye Radio, labda cheo kilikuwa ni kingine.

Nadhani unaposema watu wataarifiwe kabla, hii inaweza kuwa applicable pale mtu anapotokea nje ya mfumo wa Serikali. Ukisema iwe ndiyo general procedure ya serikali, inaweza kuleta ukiritimba katika uteuzi, tetesi zitakuwa zinazidi maana hakutakuwa na jinsi ya kudhibiti taarifa za teuzi kutoka kabla ya wakati, nk. Pia imagine kila mawaziri wakiwa wanahamishwa kutoka Wizara moja hadi nyingine wawe wanaulizwa kwanza, hiyo backlog ya kusubiri watu itakuwa kubwa. Wazo lako ni zuri kakini sidhani kama liko practical sana hasa kwa nchi yetu ambapo si wengi wenye options nzuri kuliko teuzi hizi wanazopewa.

Kimsingi nadhani tupunguze vyeo vya kuteuliwa na tutafute tararibu zingine za kupata watendaji na tuwe na verification system mfano kupitia Bunge kabla ya kuwaidhinisha.
 
Unaweza kuweka mfumo watu wanataarifiwa, hata kama ni muda mfupi tu kabla ya kutangazwa, wakajua kwamba mpaka unataarifiwa bado upo kwenye vetting, na mteuzi akisikia umevujisha habari, anakuona huna kifua anaghairi, kama alivyofanya Nyerere kwa Malecela.

Ukisoma kitabu cha Mkapa "My Life, My Purpose", ameeleza kabisa jinsi Nyerere alivyokuwa anamuita, anaongea naye, anamwambia anataka kumpa kazi fulani, tena kazi za kimataifa balozini. Nyerere alijua umuhimu wa kuwasiliana na watu kabla ya teuzi, hususan mawaziri nyeti. Hizi cabinet reshuffle unaweza kumbadili mtu tu kwa sababu ile si appointment mpya ni reshuffle tu. Hata kwa wakuu wa wilaya ingewezekana kufanyika hivyo, not necessarily from the president, but from te Ikulu bureaucracy.

Kuhusu point yako ya mwisho, hivi vyeo vya ukuu w awilaya mimi hata sielewi umuhimu wake. Ni kama vimekaa kuongeza posts tu za rais kuchomeka watu wake anaowataka kwa siasa zake.
 
Au hukubaliani na sera za aliyekuteua na hutaki kuwa sehemu ya yale anayofanya.
 
Utajuaje amevujisha yeye? Mpaka umeanza kuchunguza, utawachunguza wangapi? Point yangu inaweza kuwa inaleta mkanganyiko ambao kwa utaratibu wa sasa haupo. Mwingine wabaya wake wanaweza kuvujisha kwa makusudi ili kumharibia, nk.

Vyeo vya wakuu wa wilaya na mkoa zina umuhimu mkubwa kwa CCM. Ni layer nyingine ya kimamlaka inayotumika kuhakikisha maslahi ya chama yanalindwa. Pia wanatumika kuwatambua mapema watu wanaoweza kukisaidia chama au kukiletea chama shida mbele ya safari. Kwa maslahi ya taifa ni vyeo visivyo na maana ila kichama vina maana kubwa sana. Kimsingi Serikali inatumia rasilimani zake kuwalipa watendaji ambao kazi yao ya msingi ni ya chama.
 
Mheshimiwa rais anajua mapato Yao hata kabla hajawateua Ila aliwateua kwa manufaa mapana ya taifa.
Ngoja tuwafanyie audit kidogo tu tuone Nani mjanja.
Kwani lazima kufanya kazi na WAHUNI? Suluhisho ni katiba mpya sasa
 
Ficha ujinga wako
 
“Nitampa ofa asiyoweza kuikataa”.

Lakini wao wameikataa!

Labda wameona hatima ya Godmother iko mashakani.
 
mkuu inasikitisha ila unaonekana umeweka imani yako na future yako kwa Gov sana...but maisha ni zaidi ya kufanya kazi Gov..siku ukitoka kwenye hilo gereza utaona life is full of enjoyable things kuliko kuwaza ajira na teuzi za Gov.
Mie siko huko Gov
Ila nawazungumzia wahusika wa hii mada walioko Gov

Nafikiri kwa ajira zao zilivyo hawapaswo kumkatalia mwajiri wao labda wajifute utumishi

Wa private huku no rahisi tunaendelea na maisha yetu

Si kama sijui life is good
Life is gooood anywhere
Ni wewe tu kujiset
Ukae unawaza uteuzi wanakujua??
 
Kwani lazima?

Kutangaza uteuzi kabla ya kupata ridhaa ya mteule ni dharau na ujinga.
Labda kama umejiajiri
Kwenye ajira huko ni mwendo wa kupangiwa vituo hadi akili ziwakae watu sawa
Hutaki jiajiri ujipangie
 
Vyeo vifutwe na hilo litampunguzia rais kazi za uteuzi.

Mlipa kodi naye atapunguziw amzigo wa viongozi wasio na maana.
 
Nashangaa watu wanavyopuyanga kwenye hii ishu
 
Labda kama umejiajiri
Kwenye ajira huko ni mwendo wa kupangiwa vituo hadi akili ziwakae watu sawa
Hutaki jiajiri ujipangie
Mimi nilishasema sitafanya kazi za serikali ya Tanzania maisha yangu yote.

Sitaki ujinga wa kupewa kazi bila makubaliano kama manamba.
 
Mimi nilishasema sitafanya kazi za serikali ya Tanzania maisha yangu yote.

Sitaki ujinga wa kupewa kazi bila makubaliano kama manamba.
Waliokubali kuwa watumishi wanakinywea kikombe and they know it
Sana sana wanakushangaa wewe
 
Waliokubali kuwa watumishi wanakinywea kikombe and they know it
Sana sana wanakushangaa wewe
Wao wanafurahia kula kwa urefu wa kamba zao.

Mimi nawashangaa wameridhika kufungwa kamba, tena fupi!

Siwalaumu, ila ni maisha ambayo nimeyakwepa tu siyataki.

Mama yangu alifanya kazi Ikulu ya Nyerere na Ofisi ya PM, najua ukiritimba wa serikalini.
 

Kuteuliwa na viongozi wa kisiasa walioko madarakani kwa wizi wa kura kuna heshima gani?
 
Wao wanafurahia kula kwa urefu wa kamba zao.

Mimi nawashangaa wameridhika kufungwa kamba, tena fupi!

Siwalaumu, ila ni maisha ambayo nimeyakwepa tu siyataki.

Mama yangu alifanya kazi Ikulu ya Nyerere na Ofisi ya PM, najua ukiritimba wa serikalini.
Kupanga ni kuchagua
Kila mtu na lwake
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] aise una hoja nzito halafu zinafikirisha na kuchekesha at the same time [emoji936]
 
Sana jamaa kiranga ana hoja nzito na ambazo kama serikali imejisahau basi wajirekebishe kuanzia hapa siyo dhambi kujisahihisha huwezi kumteua mtu bila kumwambia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…