Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Mkuu,Una hoja muhimu na kimsingi nakubaliana na wewe ila tukumbuke mambo kadhaa wakati tunalitafakai hili:
1. Mambo ya watu kuteuliwa na kutangazwa kabla hawajaambiwa hayajaanza leo. Nakumbuka kwa mbali story ya John Malecela kupewa taarifa ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu. Serikali za Tanzania kubadilisha tararibu zake za kufanya kazi huwa ni ngumu sana ndiyo maana mpaka leo tunakalishana barabarani masaa kusubiri viongozi wapite bila kujua dunia imebadilika, idadi ya raia pia imeongeeka mno kwa hiyo utaratibu huo unaleta karaa kuzidi zamani.
2. Vyeo vya Mkuu wa Wilaya na Mkoa ni purely vya kisiasa, wanateuliwa kisiasa na wanakwenda kufanya kazi za kisiasa. Kwa muktadha huo kuna watakaokwambia Rais hawezi kujishusha na "kujikomba" kwa mtu ambaye kimsingi anakwenda kuwa mwakilishi wake katika wilaya au mkoa. Kuna suala hapa la nani amsujudie mwenzie. Hilo unalosema nadhani linafanyika pale mteuliwa anapotolewa kwenye sekta binafsi au ni jobless ila kama tayari uko ndani ya mfumo wa ajira serikalini sioni mfumo wetu ukiadapt hilo unalopendekeza (ingawa kiungwana linatakiwa kufanyika kama unavyosema). Kuna hali ya Serikali kujaribu kuviongezea thamani hivi vyeo vilivyopitwa na wakati mfano kwa kuwa na hizi "elements of surprises" wakati wanavyoteuliwa. Wewe hauoni jinsi Nyuzi za Teuzi zinavyokuwaga maarufu humu? Watanzania kwa ujumla wetu tunathamini sana vyeo.
3. Wengi tunajua CWT imekuwa compromised muda mrefu sana na ni kama wamekuwa wanatimiza matakwa ya Serikali badala ya kusimamia maslahi ya waalimu. Kuwatoa viongozi wao kwa mkupuo ni ama serikali ilianza kupoteza ushawishi ndani ya CWT wakataka kufanya mabadiliko ya haraka (labda hawa hawakuwa watu wao) au Serikali ilishawachukulia poa CWT wakajisahau tu wakijua "hawa ni wanetu".
Nadhani issue kubwa hapa ni kwa nini Serikali haikuzingatia nyazfa za hawa wateule ndani ya CWT na kwamba wana majukumu makubwa ambayo kimsingi ni kuisimamia serikali kuhusiana na masuala ya waalimu. Kuwatoa pale tena kwa mkupuo kunaweza kutafsiriwa kama njia ya kuidhoofisha CWT. Wangekuwa waalimu tu wa kawaida ingekuwa story nyingine.
1. Speaking of Malecela, Nyerere alitaka kumteua Malecela kuwa PM, Malecela akaambiwa na watu wa system, akafanya bonge la party, kabla hajatangazwa, Nyerere akaona huyu sijamtangaza kafanya party, nikimtangaza si ndo itakuwa balaa? Akaghairi.
Serikali ya Nyerere ilikuwa si tu unapewa taarifa kabla ya uteuzi, bali hata unapopewa taarifa unakuwa bado unaangaliwa.
2. Mimi naona kama vyeo wanataka kuviongezea thamani, basi wateule wangepata hata ka simu tu ka kutoka Ikulu, si lazima itoke kwa rais, mfanyakazi tu wa kawaida wa Ikulu anaweza kupiga simu ku verify kwamba mteule mzima, na rais angependa kujua mtu huyo akipewa heshima ya kulitumikia taifa katika nafasi ya ukuu wa wilaya atakubali?
Majority ya watu wangefurahi sana kupata simu hiyo na inge wa motivate sana kwenye kazi. Ikulu ime miss opportunity kuwa motivate watu hapo.
3. CWT teuzi zimetumika kumaliza migogoro, nimelitaja hapo juu (post #57 na #60). Hili jambo baya kwa sababu kama nafasi ya ukuu wa wilaya ina umuhimu, tunaifanya kama chaka la kumalizia migogoro tu. Kama haina umuhimu isiwepo kabisa.