Kuteuliwa na mamlaka za nchi ni heshima kubwa, anayekataa basi kuna maovu anataka kuficha kwenye nafasi aliyo nayo

Kuteuliwa na mamlaka za nchi ni heshima kubwa, anayekataa basi kuna maovu anataka kuficha kwenye nafasi aliyo nayo

Akili za machawa bhana kwahyo unstaka akale heshima jiongeze uongozi una mabano mengi kama wapo wenye sifa zaidi wateuliwe wao basi
 
Boss una mawazo mazuri sana: Ila nakukumbusha uzingatie hizi principle mbili,
1:Boss hakosei
2:Endapo boss akikosea rejea principle namba 1.
Kwahiyo hao ndg zetu wanaweza kupoteza vyote kwa pamoja. Mfano tu mdogo mimi nimpe kazi ya kufanya mwanangu halafu akatae aniambie mimi hiyo kazi sitaki nina kazi nyingine na wakati huo kazi zote ziko chini ya mamlaka yangu, sitakubali, huo ni utovu wa nidhamu wa kiwango cha juu
Boss hakosei hata akiiteua maiti?

I mean these people don't even call to see if the appointees are still breathing.

Come on man.

Mfano wako ni mbaya, serikali si baba wa Watanzania.

Na hata mtoto wako anaweza kuwa na sababu nzuri za kukukatalia kufanya kazi fulani kama unambambikia tu kazi bila kusikilizana naye kwanza.

Mtoto ana pumu inayokuwa triggered na vumbi, wewe unamwambia afagie uwanja wenye vumbi. Hiyo si kazi, hiyo ni child abuse.

Mtoto ana haki ya kukataa kazi kwa sababu za kiafya.

Sasa hawa wateule hata kama wana sababu za kiafya, hawapewi nafasi za kukataa kazi.

Halafu wakishindwa kufanya kazi tutalalamika ma DC hawana ufanisi?

Wakati kazi wanalazimishwa kuzifanya, hawajataka kwa utashi wao wenyewe.
 
Kama umeteuliwa ni kwamba umekidhi vigezo kwa maana una sifa stahiki lakini pia umepewa heshima kubwa na Mamlaka iliyokuteua.

Jiulize kuna Watanzania wangapi wenye sifa zaidi yako lakini hawakupewa nafasi hiyo?

Vyombo vya habari vimetoa taarifa kuna Watu wamekataa Heshima waliyopewa na Mamlaka ya Uteuzi.
Itoshe kusema watu hawa kama ni kweli wapo hawana chembe ya uzalendo hata kidogo, umetumwa ukawatumikie Watanzania ukiwakilisha Mamlaka ya Uteuzi unakataa na bado unataka uendelee kwenye nafasi yako ya sasa?

Kuna mambo yanatakiwa kutiliwa shaka kwa watu hawa ikiwa ni pamoja na

1. Yawezekana nafasi walizopo sasa kuna maovu mengi wamefanya hivyo wanaogopa kuachia ghafla mengi yataibuka.

2. Yawezekana kile wanacholipwa ni kikubwa sanaa kuliko wanavyostahili, Wote tunajua Waajiri wao ni Wanachama. Je Wanacholipwa kama Mshara na Stahiki nyingine zinalingana na Waajiri wao?

3. Waajiri wa hawa watu (Wanachama) Je, ni kweli wanawapima utendaji wao kwa Maana ya Investment zinazofanyika chini ya Chama Chenu? Tutakuwa na Michango isiyokoomaa au tutafute uwezekezaji wenye tija na tupunguze michango?

Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

View attachment 2501128
Inashangaza kwamba rais hafanyi mazungumzo na watu kabla ya kuwapa nyadhifa mbali mbali! Kwanini umshtukize mtu uwaziri kabla ya kuongea naye kuona kama yupo tayari au hapana? Tunalalamika suala la kukosekana uhuru Tanzania ndio mambo kama hayo sasa. Tuache kulazimisha mambo. Mbowe aungwe mkono katiba mpya ipatikane mapema.
 
Mkuu,

Hili ni jambo la msingi, msingi, msingi kabisa.

Kwa nini Watanzania wengi wanalichukulia poa poa tu?

A simple phonecall kumjulia hali mteule na kumuuliza kama atakubali uteuzi ingemuonesha courtesy mteule, na ingemuondolea aibu ya kukataliwa publicly rais.

Ikulu imeshindwa hata hili?
 
Sekta binafsi mna tambo
Utadhani huko boss wako hawezi kukupangia kituo
mkuu inasikitisha ila unaonekana umeweka imani yako na future yako kwa Gov sana...but maisha ni zaidi ya kufanya kazi Gov..siku ukitoka kwenye hilo gereza utaona life is full of enjoyable things kuliko kuwaza ajira na teuzi za Gov.
 
1. Yawezekana nafasi walizopo sasa kuna maovu mengi wamefanya hivyo wanaogopa kuachia ghafla mengi yataibuka.
Hii ndio sababu kubwa, wanachezea sana 2% ya contribution ya waalimu; kuna ubadhirifu mkubwa sana upo chini ya uongozi wa hao watu.....sijui vyombo vya usalama viko wapi kujua hilo, in anyhow haiwezekani watu wa kutoka sehemu moja wote wagomee uteuzi......impossible something very wrong!!!
 
Kama umeteuliwa ni kwamba umekidhi vigezo kwa maana una sifa stahiki lakini pia umepewa heshima kubwa na Mamlaka iliyokuteua.

Jiulize kuna Watanzania wangapi wenye sifa zaidi yako lakini hawakupewa nafasi hiyo?

Vyombo vya habari vimetoa taarifa kuna Watu wamekataa Heshima waliyopewa na Mamlaka ya Uteuzi.
Itoshe kusema watu hawa kama ni kweli wapo hawana chembe ya uzalendo hata kidogo, umetumwa ukawatumikie Watanzania ukiwakilisha Mamlaka ya Uteuzi unakataa na bado unataka uendelee kwenye nafasi yako ya sasa?

Kuna mambo yanatakiwa kutiliwa shaka kwa watu hawa ikiwa ni pamoja na

1. Yawezekana nafasi walizopo sasa kuna maovu mengi wamefanya hivyo wanaogopa kuachia ghafla mengi yataibuka.

2. Yawezekana kile wanacholipwa ni kikubwa sanaa kuliko wanavyostahili, Wote tunajua Waajiri wao ni Wanachama. Je Wanacholipwa kama Mshara na Stahiki nyingine zinalingana na Waajiri wao?

3. Waajiri wa hawa watu (Wanachama) Je, ni kweli wanawapima utendaji wao kwa Maana ya Investment zinazofanyika chini ya Chama Chenu? Tutakuwa na Michango isiyokoomaa au tutafute uwezekezaji wenye tija na tupunguze michango?

Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

View attachment 2501128
UZI WA CHAWA WA MAMA
 
Mkuu,

Hili ni jambo la msingi, msingi, msingi kabisa.

Kwa nini Watanzania wengi wanalichukulia poa poa tu?

A simple phonecall kumjulia hali mteule na kumuuliza kama atakubali uteuzi ingemuonesha courtesy mteule, na ingemuondolea aibu ya kukataliwa publicly rais.

Ikulu imeshindwa hata hili?
Kabisa! Rais aache kufikiri kuwapa watu vyeo ni kuwapa chakula au kuwainua kimapato. Kuna watu hawahitaji hayo mambo. Sio kila mtu anapenda cheo!
 
Kama umeteuliwa ni kwamba umekidhi vigezo kwa maana una sifa stahiki lakini pia umepewa heshima kubwa na Mamlaka iliyokuteua.

Jiulize kuna Watanzania wangapi wenye sifa zaidi yako lakini hawakupewa nafasi hiyo?

Vyombo vya habari vimetoa taarifa kuna Watu wamekataa Heshima waliyopewa na Mamlaka ya Uteuzi.
Itoshe kusema watu hawa kama ni kweli wapo hawana chembe ya uzalendo hata kidogo, umetumwa ukawatumikie Watanzania ukiwakilisha Mamlaka ya Uteuzi unakataa na bado unataka uendelee kwenye nafasi yako ya sasa?

Kuna mambo yanatakiwa kutiliwa shaka kwa watu hawa ikiwa ni pamoja na

1. Yawezekana nafasi walizopo sasa kuna maovu mengi wamefanya hivyo wanaogopa kuachia ghafla mengi yataibuka.

2. Yawezekana kile wanacholipwa ni kikubwa sanaa kuliko wanavyostahili, Wote tunajua Waajiri wao ni Wanachama. Je Wanacholipwa kama Mshara na Stahiki nyingine zinalingana na Waajiri wao?

3. Waajiri wa hawa watu (Wanachama) Je, ni kweli wanawapima utendaji wao kwa Maana ya Investment zinazofanyika chini ya Chama Chenu? Tutakuwa na Michango isiyokoomaa au tutafute uwezekezaji wenye tija na tupunguze michango?

Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

View attachment 2501128
Kabla hujametua mtu wasiliana nae kwanza
 
Naona mmemcharua Kiranga, amechafukwa hatari!
Hapana. Ni mazungumzo ya kawaida tu.

Ulofa ni matatizo sana.

Mimi nimeanza kuranda corridors za Ikulu tangu nipo tumboni mwa mama yangu.

Enzi za Joan Wicken na Julius Kaizari mwenyewe.

Enzi hizo ukipewa uteuzi wa Ikulu, mpaka mjumbe wako wa nyumba kumi anakuandikia barua ya kuelezea tabia yako mtaani. Faili lazima lipitiwe na vijana wa kazi maalum wa Dr. Mahiga.

Leo nashangaa Ikulu standards zimeshuka kuliko ligi ya mchangani.
 
Kabla hujametua mtu wasiliana nae kwanza
Naam mkuu.

Kwa nini jambo rahisi na la msingi kabisa kama hili linakuwa mgogoro mkubwa sana Tanzania? Tena katika teuzi za sehemu nyeti kama Ikulu?

Kuwasiliana na wateule kabla kungewapa nafasi ya kukubali au kukataa na kuondoa aibu kubwa ya rais kukataliwa publicly.

One almost gets the feeling kwamba, teuzi hizi zinalazimishwa kwa watu fulani, kwa sababu fulani, na wanasukumiwa teuzi serikali ikijua wakishateuliwa hawawezi kukataa, halafu wanakuja kukataa na serikali inabaki na aibu.
 
Hapana. Ni mazungumzo ya kawaida tu.

Ulofa ni matatizo sana.

Mimi nimeanza kuranda corridors za Ikulu tangu nipo tumboni mwa mama yangu.

Enzi za Joan Wicken na Julius Kaizari mwenyewe.

Enzi hizo ukipewa uteuzi wa Ikulu, mpaka mjumbe wako wa nyumba kumi anakuandikia barua ya kuelezea tabia yako mtaani. Faili lazima lipitiwe na vijana wa kazi maalum wa Dr. Mahiga.

Leo nashangaa Ikulu standards zimeshuka kuliko ligi ya mchangani.
Nimecheka sana ulipoandika "utovu wa nidhamu wameanza ikulu kwa kuwatangaza watu kwenye teuzi bila hata ya kuwasiliana nao"

Nikacheka tena uliposema kuwa je kama mtu anaichukulia serikali iliyopo kuwa si ya halali?"

Yote kwa yote jamani anayoyaandika Kiranga ni ya kweli sana ukiyatafakari mfano swala la mtu kukataa tunaweza kuingiza tafsiri ya bwana Kiranga hapo kwamba haikubali serikali iliyomteua ndomana amekataa, na yet kwanini serikali iteue mtu ambae hakubaliani na serikali hiyo, ina maana hawakumjua mapema?

Hilo la kuwasiliana, kwakuwa uteuzi ni mchakato na unahusisha watu wengi (si raisi peke yake) basi baadhi yao wawe wanachukua jukumu la kuwasiliana na mteuliwa ili ajue kama anakataa aseme ili ateuliwe mwingine na kama anakubali aanze kujipanga kwa maisha mapya. Tena katika hili Kuna waliotolea mifano kwa mwalimu na mwajiri wake (yaani DED) kwamba eti mkataba unasema "na majukumu mengine atakayopangiwa na mwajiri". Well hatukatai lakini walimu wenyewe mashahidi zile barua za teuzi zinakuwaga Siri kiasi kwamba hata muda mwingine wakuu wako wa kazi wanachelewa kujua (hasa mwalimu mkuu) na ukishapewa Kuna siku unapewa za maandalizi mpaka tarehe fulani, hapo kwenye hizo siku tumeshuhudia walimu mara kadhaa wakiitwa halmashauri kwa kukataa uteuzi japo wamepata tabu sana lakini kazi zao wanazo na wengine walipata teuzi kwa muda walipokuwa tayari kuzikubali. Point kuu ni kwamba hawatangazwi kabla ya kuteuliwa na kuarifiwa kwa barua tofauti na ikulu ambapo wanatangazwa kwenye media moja kwa moja
 
Nimeona Mwagama kasema watashughulikiwa
 
Nimecheka sana ulipoandika "utovu wa nidhamu wameanza ikulu kwa kuwatangaza watu kwenye teuzi bila hata ya kuwasiliana nao"

Nikacheka tena uliposema kuwa je kama mtu anaichukulia serikali iliyopo kuwa si ya halali?"

Yote kwa yote jamani anayoyaandika Kiranga ni ya kweli sana ukiyatafakari mfano swala la mtu kukataa tunaweza kuingiza tafsiri ya bwana Kiranga hapo kwamba haikubali serikali iliyomteua ndomana amekataa, na yet kwanini serikali iteue mtu ambae hakubaliani na serikali hiyo, ina maana hawakumjua mapema?

Hilo la kuwasiliana, kwakuwa uteuzi ni mchakato na unahusisha watu wengi (si raisi peke yake) basi baadhi yao wawe wanachukua jukumu la kuwasiliana na mteuliwa ili ajue kama anakataa aseme ili ateuliwe mwingine na kama anakubali aanze kujipanga kwa maisha mapya. Tena katika hili Kuna waliotolea mifano kwa mwalimu na mwajiri wake (yaani DED) kwamba eti mkataba unasema "na majukumu mengine atakayopangiwa na mwajiri". Well hatukatai lakini walimu wenyewe mashahidi zile barua za teuzi zinakuwaga Siri kiasi kwamba hata muda mwingine wakuu wako wa kazi wanachelewa kujua (hasa mwalimu mkuu) na ukishapewa Kuna siku unapewa za maandalizi mpaka tarehe fulani, hapo kwenye hizo siku tumeshuhudia walimu mara kadhaa wakiitwa halmashauri kwa kukataa uteuzi japo wamepata tabu sana lakini kazi zao wanazo na wengine walipata teuzi kwa muda walipokuwa tayari kuzikubali.
Mimi nafikiri hawa watu wa Ikulu, na rais, si wajinga kabisa. Ingawa wana ujinga fulani hivi.

Kuna logic fulani wanaifuata, ila logic yao bado ina ujinga.

Haiwezekani iwe hawajui umuhimu wa kuwasiliana na wateule kabla ya uteuzi.

Ila, nafikiri teuzi zinatumika kisiasa.Kwa mfano, hapo CWT kuna migogoro kibao, kwa hivyo teuzi zinatumika kumaliza migogoro. Watu wanatolewa hapo na kupewa ukuu wa wilaya, ili kumaliza migogoro yao hapo.

Yani badala ya migogoro kumalizwa kwa mazungumzo, serikali inataka kutumia njia ya mkato ya teuzi kumaliza mgogoro. Ukuu wa wilaya inakuwa ni chaka la kumalizia migogoro na kuzawadia makada, si kazi ya watu wenye sifa za ukuu wa wilaya.

Sasa, katika mazingira kama hayo, ukimtaarifu mtu kabla, anaweza kutoa udhuru.

Ndiyo maana serikali haitaki kutoa taarifa, inafanya teuzi za kivamizi, unazisikia kwenye redio.

Wanafanya hivyo wakiamini kwamba ukishasikia teuzi redioni au gazetini, utaona aibu kutoa udhuru.

Sasa, wanakutana na watu bado wanatoa udhuru, halafu Ikulu inaaibika.

Watu tunaishangaa Ikulu.

Tunajiuliza, inakuwaje Ikulu inafanya teuzi bila kuwasiliana na wateule?

Kama kawaida yetu Tanzania, kila kitu ni kwa mtindo wa kuwindana.

Mpaka teuzi za kuwindana.
 
Hapana. Ni mazungumzo ya kawaida tu.

Ulofa ni matatizo sana.

Mimi nimeanza kuranda corridors za Ikulu tangu nipo tumboni mwa mama yangu.

Enzi za Joan Wicken na Julius Kaizari mwenyewe.

Enzi hizo ukipewa uteuzi wa Ikulu, mpaka mjumbe wako wa nyumba kumi anakuandikia barua ya kuelezea tabia yako mtaani. Faili lazima lipitiwe na vijana wa kazi maalum wa Dr. Mahiga.

Leo nashangaa Ikulu standards zimeshuka kuliko ligi ya mchangani.
Una hoja muhimu na kimsingi nakubaliana na wewe ila tukumbuke mambo kadhaa wakati tunalitafakai hili:

1. Mambo ya watu kuteuliwa na kutangazwa kabla hawajaambiwa hayajaanza leo. Nakumbuka kwa mbali story ya John Malecela kupewa taarifa ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu. Serikali za Tanzania kubadilisha tararibu zake za kufanya kazi huwa ni ngumu sana ndiyo maana mpaka leo tunakalishana barabarani masaa kusubiri viongozi wapite bila kujua dunia imebadilika, idadi ya raia pia imeongeeka mno kwa hiyo utaratibu huo unaleta karaa kuzidi zamani.

2. Vyeo vya Mkuu wa Wilaya na Mkoa ni purely vya kisiasa, wanateuliwa kisiasa na wanakwenda kufanya kazi za kisiasa. Kwa muktadha huo kuna watakaokwambia Rais hawezi kujishusha na "kujikomba" kwa mtu ambaye kimsingi anakwenda kuwa mwakilishi wake katika wilaya au mkoa. Kuna suala hapa la nani amsujudie mwenzie. Hilo unalosema nadhani linafanyika pale mteuliwa anapotolewa kwenye sekta binafsi au ni jobless ila kama tayari uko ndani ya mfumo wa ajira serikalini sioni mfumo wetu ukiadapt hilo unalopendekeza (ingawa kiungwana linatakiwa kufanyika kama unavyosema). Kuna hali ya Serikali kujaribu kuviongezea thamani hivi vyeo vilivyopitwa na wakati mfano kwa kuwa na hizi "elements of surprises" wakati wanavyoteuliwa. Wewe hauoni jinsi Nyuzi za Teuzi zinavyokuwaga maarufu humu? Watanzania kwa ujumla wetu tunathamini sana vyeo.

3. Wengi tunajua CWT imekuwa compromised muda mrefu sana na ni kama wamekuwa wanatimiza matakwa ya Serikali badala ya kusimamia maslahi ya waalimu. Kuwatoa viongozi wao kwa mkupuo ni ama serikali ilianza kupoteza ushawishi ndani ya CWT wakataka kufanya mabadiliko ya haraka (labda hawa hawakuwa watu wao) au Serikali ilishawachukulia poa CWT wakajisahau tu wakijua "hawa ni wanetu".

Nadhani issue kubwa hapa ni kwa nini Serikali haikuzingatia nyazfa za hawa wateule ndani ya CWT na kwamba wana majukumu makubwa ambayo kimsingi ni kuisimamia serikali kuhusiana na masuala ya waalimu. Kuwatoa pale tena kwa mkupuo kunaweza kutafsiriwa kama njia ya kuidhoofisha CWT. Wangekuwa waalimu tu wa kawaida ingekuwa story nyingine.
 
Back
Top Bottom