Kuteuwa Wakurugenzi nje ya Utumishi wa Umma hakupaswi kufumbiwa Macho

Rais wetu aliahidi mabadiliko ila Sasa anachofanya ni tofauti. Kamuweka mkwe wake kuwa mkuu wa TAMISEMI ili asimamie vizuri ushindi wake. Licha ya hivyo kaanza kuweka mwenyekiti wa CCM kuwa Mkurugenzi akafanye ukada.
 
Tufikie Mahali tuache kulalamika.

Tuhakikishe haufanyiki uchaguzi wowote 2024/2025 kabla ya kupatikana Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi.

Amen.
Shida vyama vyetu havina msimamo, huo muda ukifika wanaenda kushiriki. Inabidi wawe wamoja sio kumuogopa CCM .
 
Mbarali CDM ilisusia,

Uchaguzi ujao wa MITAA na mkuu, hakuna kususia,

Tuhakikishe haufanyiki Kwa maandamano Hadi ipatikane Tume huru ya Uchaguzi Kwa kubadili vipengele kadhaa kwenye Katiba iliyopo.
CDM ikishiriki nitashangaa Sana. Acha hao ACT na washirika wenzake wa CCM washiriki.
 
Shida vyama vyetu havina msimamo, huo muda ukifika wanaenda kushiriki. Inabidi wawe wamoja sio kumuogopa CCM .
Kuna chama kingine Cha upinzani Tanganyika zaidi ya CDM?

Ushirika na wasaliti hautofanikiwa, wakitangaza kushiriki, wanawekwwa kundi moja na CCCm!!
 
KIFUPI NAFASI ZA WAKURUGENZI ZITANGAZWE WATANZANIA WENYE SIFA ZAO WAOMBE
KISHA WALIOCHAGULIWA RAIS AWATEUE
UKADA UNALIGHARIMU TAIFA KODI ZA MASIKINI WANANCHI ZINALIWA NA HAWA MAKADA
 
Umeongea point tupu tatizo wanatuona manyani
 
Waliokosa ubunge akawapa uded
Ubalozi umekuwa deal ya wakubwa kwenda kupunzika na kuwa acha career diplomats wakisugua mabench
Nasikia hata ujaji una harufu hiyo hiyo. Je tutafika?
 
umeumia 🤣
una ajira ya kudumu tena unapewa ajira nyingine na wasio na ajira wafanye nini?

Acha gubu watu wengine nao wapate ulaji pia khaaaa
 
Kada wa chama anakuwaje DED ambayo ni purely position ya kiutendaji katika utumishi wa umma, tangu lini majukumu ya DED yakawa ni pamoja na kufanya siasa? nchi imeshafika mahala pabaya sana na likija swala la katiba mpya wanaendeleza danadana ili waendelee kubaki na mamlaka yaliyopitiliza kiwango...​
 
Ccm imeharibu hii nchi,ila kuna wapuuzi wanagalagala,abusrd
 
Haijalishi mtu anateuliwa kutoka wapi, kikubwa watu wateuliwe kwa kuzingatia weledi wao unaendana na maeneo wanayopelekwa na uwezekano wa wao kuleta mabadiliko chanya kwa kutegemea uzoefu na mambo aliyowahi fanya anaeteuliwa . Hizi teuzi zenye msukumo wa kisiasa hazitatufikisha popote kama taifa.
 
Magufuli aliamua “kutengua” nguvu ya utumishi wa umma, kuwaondolea watumishi ile hali ya kujiamini kwamba wako kikatiba na kisheria kutumikia umma na badala yake wajue wanatumika kwa ridhaa na huruma yake. Wasahau dhana ya kutumikia umma (public service); badala yake wajue kwamba kipaumbele ni kumtumikia yeye binafsi. Kwamba he can hire and fire them anyway, anyhow as it pleases him. Akatupilia mbali miongozo yote ya schemes of service.

Rais wa awamu ya sita naye kagundua huo ni mkakati wenye manufaa sana kwake; hivyo kaushikilia. Unampa uhuru wa kuchezesha watumishi wa umma kama kete za draft watumikie maslahi yake. Pia unamwezesha kugawa fursa za ajira kwa vijana wake, ndugu, jamaa, marafiki na machawa bila vikwazo. Hata kijana anayemaliza chuo tu anaweza kupewa ukurugenzi! Indeed, civil service is virtually dead and buried in Tz.

Hapa ndipo jeuri ya viongozi wa CCM ilipofikia tangu walivyorithi madaraka makuu ya uRais (absolute presidential power) toka kwa Nyerere ambayo hawana mpango wa kuyaachia.

Tawala za kidikteta hushamiri pasipo na sheria wala kanuni za haja.
 
Uko sahihi kabisa na umeliweka vizuri jambo hili.
Utumishi wa umma umegawanyika katika makundi mawili: civil service na millitary service. Civil servants na millitary servants ni uttumishi wa kudumu (permanent) na unaongozwa na kanuni kuu (principle) ya kwamba watakuwa watiifu kwa mwanasiasa yo yote atakayekuwa madarakani. Wao civil servants na millitary servants hawaruhusiwi kuwa wanasiasa wala kuwa wanachama wa chama cho cho chote cha siasa.

Utumishi wa kisiasa (polititical servants) aka wanasiasa, ni utumishi wa kuwakilisha matakwa ya watu/umma. Uongozi katika utumishi wa kisiasa hupatikana kwa kuchaguliwa na umma au chama cha siasa. Utumishi huu wa kisiasa si wa kudumu na hauna pensheni.

Tatizo ni kwamba wanasiasa wameanza kuyachanganya haya makundi. Wanasiasa wamekuwa wakichukua uongozi wa civil service kwa kofia ya kuteuliwa na rais badala ya civil service commission kama ambavyo sheria ya utumishi wa umma inavyoelekeza. Ni wakuu wa wilaya na mikoa pekee huko wilayani na mikoani ndiyo wanapaswa kuteuliwa moja kwa moja na raisi kama wawakilishi wake wa kisiasa
 
Chawa wanakula shavu 10 then wanajitokeza 10,000 wakidhani watateuliwa. Ni mbinu ya kuwashika akili.
 
Jambo jingine, Mkurugenzi kupewa jukumu la kusimamia uchaguzi ni kwa sababu kikatiba mkurugenzi hapaswi kuwa kada wa chama chochote cha siasa. Sasa unamuweka kada, anawezaje kutenda haki?
Wasipofanya hivyo 2025 hawarudi
 
T
Tunaposema Katiba Mpya ni MUHIMU SANA Sasa kupatikana muwe mnatuelewa. Katiba Mpya siyo suala la Wanasiasa peke yao bali ni suala linalowahusu Raia wote waliopo kwenye nchi hii.
 
Kuna kitu hukijui au unakisahau.
Siyo kila kiongozi wa CCM hajapitia utumishi wa umma kabla ya kupewa uongozi CCM.
Sasa siku akirudishwa serikalini huwezi kusema hana uzoefu kwenye utumishi wa umma.
Mfano kuna katibu wa CCM mkoa fulani wa kaskazini alikuwa mwalimu serikalini kwa miaka mingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…