Kuteuwa Wakurugenzi nje ya Utumishi wa Umma hakupaswi kufumbiwa Macho

Mtoa hoja amesema sifa ya mkurugenzi anatakiwa atoke kwenye manegarial position yaani awe aliwahi kuwa mkuu wa idara fulani, kama ni elimu basi awe amekuwa mkuu wa moja ya idara za elimu na sifa nyingine hatakiwi kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Rejea wakurugenzi walioteuliwa kipindi cha utawala wa rais Kikwete uliona mkurugenzi mwana ccm? Magufuli alikuwa anakiuka sheria na taratibu za utumishi wa umma na Samia naye anaendeleza yale yale, matokeo yake ukurugenzi wa halmashauri, wilaya na mikoa wamekuwa wakiteuliwa kwa misingi ya uchama na sio kama taratibu za utumishi wa umma zinavyotaka. Mtu anayeshabikia ccm na uongozi wake na hana akili timamu.
 
Sikatai kwamba kuna walio teliuwa ambao hawakufikia vigezo alivyo sema lakini tusijumuishe kila mteuliwa aliyetokea CCM hana hizo sifa.
Kwa mfano huwezi kuniambia mwalimu wa amejiendeleza kielimu na yupo kazini miaka kadhaa atashindwa hiyo kazi.
Huwezi kuniambia mtu msomi yupo CCM lakini amewahi kuajiriwa na kushika uongozi kwenye taasisi binafsi zenye operation nyingi na department nyingi, mbunifu, mchapa kazi, muadilifu na mwenye busara atashindwa kuwa mkurugenzi mzuri. Sababu pia kuna idara zenye viongozi chini yake ambao ndiyo wasaidizi na watekelezaji wa kazi za kila siku.

Hakuna maajabu kwenye hiyo nafasi sema hapa ni wivu na kuona wanapewa outsiders ulaji,
The keyword here is SELFISHNESS.
Pia watu wako conservative sana wanaogopa mabadiliko ya kuachana na ukiritimba, ubadhirifu na rushwa.

Magufuli alikuwa anataka kuleta watu wapya ambao hawajakuzwa kikazi serikalini katika mazingira niliyo kutajia hapo juu. Lengo kubadili mazoea ya tabia mbaya.
 
Kwa ufupi nafasi za ukurugenzi ni kwa waajiriwa walioko serikali na wenye sifa zinazokidhi vigezo vya utumishi wa umma. Ukurugenzi ni kama nafasi ya kupanda daraja sio ajira mpya na ndio maana muundo wa utumishi ukaweka masharti ya mtu kuwa mkurugenzi lakini ccm wamedharau taratibu za kiutumishi wameamua kugeuza vyeo vya ukurugenzi kuwa ajira za machawa wao ambao si waajiriwa wa serikalini.
 
Huu ujinga aliuanzisha marehemu.umeleta hasara kubwa mnooooo.
Pitia report ya CAG,utafahamu hasara hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…