Kutimiza ahadi kwa kiongozi ni taswira ya heshima yake: Ahadi ya mama ya goli moja sh 10M kwa Simba

Mkuu mambo mengine kama hukuelewa ni bora tu ukakaa kimya!! Kuliko kuji expose hivi na kuonekana HAMNAZO!! msigwa alitumia kiswahili kabisa hukumuelewa, daaa!!! Kwani teknolojia si ipo katafute ile clip uisikilize tena!! "KILA MECHI MTAKAYOSHINDA"
 
Uhusiano wa kiswahili na Dar ni kwamba asili ya Kiswahili kwa Tanzania ni ukanda wa pwani.
Ukimuona mkazi wa Dar hajui kiswahili huyo sio mswahili atakuwa mhamiaji.
Kwa taarifa yako pwani wanaojua kiswahili ni Tanga na wazaram wa bagamoyo,wamakonde,wandengereko, wazaram wa kisarawe,mkuranga wanaboronga kiswahili...radi wanaitwa Radu,korosho-koroshi
 
Dawa ya deni nikulipa.

kibu denis alivyokimbia bila kutumia akili asipate ata soda jamani., mpaka imefikia hatua chama anaenda kuomba juice kwa waarabu kweliiii?

mama wape makolo mil 30 yao wazee wa kufa kibabe, wakija kupigwa na mashujaa kwenye mshono kabla kidonda hakijapona wawe na mil 30 yao.
 
Timu ikiwa timu imeshinda ndilo tamko la mwisho la mama. Nililisikia.

Kwa kuwa umepata goli tu, bila ushindi wa mechi hiyo ulipwe? Ujinga huo.
Mbona Uto walilipwa hako kagoli kamoja japo walifungwa? Hiyo ndiyo akili au?
 
Msigwa alisema toka siku ya kwanza, kila goal la ushindi
Sawa, inabidi nikuamini. Msigwa alisema hivyo!! Ila kumbuka Yanga alilipwa japo alifungwa!! Hapo tuseme ni upendeleo au?
 
Vigezo na masharti kuzingatiwa!
 
Maza naye ni mpenda sifa sn
 
Kwa lile pira papatu papatu almanusura... nadhani mlistahili viboko walau 10 kila mmoja kwa kulitia hasara na kuaibisha taifa.
 
Nyie ndio hua mna fail mitihani umeambiwa kati ya maswali 5 jibu mawili kwa kiherehere chako unajibu yote, siku ile ya Simba day Rais Samia alisema anatoa hela kwa kila goli kwenye mechi ya ushindi
 
Tafuta clip ya msigwa itazame tena zaidi ya mara 10 alafu uje ufute ujinga wako
 
wacheni mchezo na pesa za umma shindeni mechi..madunduka nyie
 
Aliyeahidi ni Msigwa na aliyekuja kusema hawalipi sababu hawajashinda ni Msigwa sasa wewe unatokaje Namtumbo huko kumwambia alikosea. Kwanini usiahidi wewe za kwako alafu uwape Simba wakifungwa, wakishinda au hata wakitoka draw?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…