Kutoa ajira kwa waliofeli divisheni 4 tena kuanzia point 28 mpaka 31 ni kutuharibia jamii

Kufeli ni kupata division four au kupatao one isiyo kupa kipato?

Je tukiajiri div one pekee hawa wenye four tuwaweke wapi?

Ni dhamu ya wenye four, nyie wenye one subirini kazi za proffession zenu.
 
Kama sikosei tumeambiwa Uhamiaji litakuwa jeshi kamili.Na kama tujuavyo siyo kazi nyingi za jeshi zinahitaji waliosoma sana.Kugundua na kukamata wahamiaji haramu haihitaji elimu kubwa sana ya darasani.
Kuhusu Mrema alipopendekeza wafungwa kutengeneza SGR siyo jambo la ajabu.
Inasemekana kama sikusahau au sikosei hata wachina walipojenga reli ya Tazara walitumia wafungwa wao kujenga! Kutumia wafungwa kujenga,mbali na kukosesha ajira watu,inapunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa aijili ya maendeleo.
 
Kuna chuo kikuu na chuo. Huyo aliyefeli anaweza kufundisha chuo na siyo chuo kikuu. Kwasababu kuna chuo cha mapishi, cha mapenzi, mabaunsa, muziki n.k
Chuo kikuu hakuna mwenye GPA mbovu yupo pale anafundisha. GPA zote ziwe zinaruhusu kusoma Masters. 2015 UDOM walikuwa wanashinikiza wakufunzi wote wawe na masters
Kwahiyo hujui na au huamini kuwa hakuna walimu wa vyuo waliofeli??
 
Mama anaupiga mwingi....ajira nje nje. Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu amzidishie hekima na busara.
 
Umeelezea,na umeweleweka,utaona wengi wanasema aliyepata Division 4,amefeli,hii ni sheria au ni vipi,hata shule nyingi za binafsi zinazojitangaza,kupata wanafunzi,huwa wanasema hatuna division 4.
 
Lengo ni kupata askari wa malindo na Doria!

Kwani hiyo inahitaji shahada!?

wakihitaji wataalam au wasomi watatutangazia
 
Hatari sana, ndiyo maana jeshi la polisi linaongoza kuwa na watu wasiojitambua, sababu ni haya haya mambo. Unakuta na polisi ukimsikiliza hadi unaona aibu wewe.
 
Kesho la polisi liko hovyo kwa sababu ya kuchukua failures. Kama ufaulu wa darasani sio hoja, basi tusifanye mtihani ili kila aliyesoma apate fursa sawa na mwingine, otherwise mitihani ni lazima ili kutafuta competence.
 
Samahani mkuu!

Nadhani ungetafiti kwanza ujue ni kwanini wanachukuliwa wa aina hiyo kisha utoe ushauri wako.
mkuu majibu yako wazi ni kutafuta jinsi ya kuibua aina fulani ya tabaka kimkakati ili pia tujipange vizuri kwa uchaguzi 2025
 
Hakuna mtu hua anafeli mtihani hapa bongo tatizo lipo kwenye mfumo wa Elimu mbovu yaani mtu unasoma miaka 7 +4+2 halafu unakuja pewa mtihani mmoja ndio unaamua hatma ya Elimu Yako hiyo ni mbaya Sana sababu Kwa wale wenye uelewa wa taratibu itawagharimu tu mwisho wa siku wanaonekana kufeli kumbe Kuna vitu na maada specifically wanazielewa ila ndio utakuta hata kwenye mtihani hazipo sababu mtihani wenyewe imekaa zig zag balaa Hivyo Ili kuuwezea inahitaji mbinu mbadala!

Elimu ni mbovu bongo!

Elimu! Elimu! Elimu!
 
Ukiona hivyo, mtoa tangazo ana mbumbumbu wake kubao nyumbani. Matatizo yanayolipata jeshi la polisi kwa sasa ni kuwa na askari wengi wenye elimu ndogo. Uhamiaji mna iga? Kuzolota kwa elimu nchini lililetwa na kozi ya ualimu kuwachukua 'waliobaki' baada ya kuengua wa kuendelea na masomo na kozi zingine. Kuna walio faulu zaidi ya div 4 wamekosa nafasi kuendelea A level au vyuo wapo mitaani, kwa nini wazuiwe kuomba? Kuwa na failures uhamiaji ni sifa?
 
Tanzania wasomi wanachukiwa sana coz wengi wa watz ni failures in both side angalia MUSUKUMA kila akilala anawaaza watu wenye degrees and above huyu ana represent milions of tanzanian wanaoamini huwezi kupata kitu bila kumwangusha aliyejuu
 
Mtoa mada hujaelimika hata kama umefika chuo kikuu unaweza zidiwa na hao div 4.
Aliekwambia div 4 ni failure nani?
NECTA ndio wana eleza kuwa div4 ni failure au wizara ya elimu?
Kamsome plato upya jinsi ya kupanga makundi ya watu kuanzia Gold mpaka Silver.
Huna lolote kichwani, jeshi huwa linatoa special chance kwa graduate.
Umesoma mpaka chuo bado unawivu na vinafasi vya watu wa chini.
Anzisha kampuni uajiri wahitimu wenye digrii lakin usiipangie serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…