Siyo kweli katika sekta ambayo inahitaji wasomi na wanasayansi ni jeshi, polisi, magereza na uhamiaji.
Kila siku technolojia mpya inaibuka, huyu aliyefeli anaweza kupewa kazi ya ujasusi? Huyu aliyefeli anaweza kutengeneza website au virus au software yoyote kulinda taarifa zisiharibiwe na virus?
Wasomi wanahitajika sana, sasa hivi siyo km miaka ile ya 1945 ya vita ya pili kutegemea bunduki.
Sasa hivi mtu 1 au 5 wanaweza kuingamiza nchi na mkafa wote. Watu wanaingia laboratory wanatengeneza virus kisha watuma kwenye nchi yako kisha wanatengeneza na dawa. Unakufa huku unamtajirisha adui
Zama za nguvu zishapitwa na wakati sasa hivi watu wanatumia akili nyingi nguvu kidogo