Kutoa ajira kwa waliofeli divisheni 4 tena kuanzia point 28 mpaka 31 ni kutuharibia jamii

Yaah mkuu now jeshi limevamiwa na wasomii
 
Mfungwa halipwi,we umesahau kuwa mrema ni mchaga,na sifa yao kuu hupenda vya bure
 
Chuki ni mbaya acha....mnalilia ajira zikitolewa mnavimba mpaka mnataka kupasuka...kama ajira zinawahusu four div 28-31 wewe si usubiri zikitoka za 1&2 ukaombe mkuu.
Halafu hao necta wanapopanga madaraja ya ufaulu hawajawahi kusema kwamba div four ni failure acha kupotosha umma,unaweza kufaulu sana lakini ukafeli katika utendaji wa kazi.
Wameamua kutoa ajira kwa form 4 huku wakijua nyie wasomi mpo cha msingi subiri zikitoka zinazowafaa wasomi wetu.
 

jeshini pia kuna vyuo vyao kwa kiwango walichopima hata aliepata dv 4 ya 28 anaweza kumudu masomo yao pia inapofikia jeshi kuhitaji masuala makubwa huwatumia wanasayansi wakubwa ktk vyuo vikuu vya inchi hiyo nao si wanajeshi alietengeneza bom la atomic hakua mwanajeshi waliotengeneza virusi vya ukimwi hawakua wanajeshi.
 
Taifa haliendelei kwasababu ya fikra kama hizo. Kuthamini sana ujuzi wa kwenye makaratasi (vyeti) kuliko kuwapima vijana kwa uwezo wao wote. Binadamu wana uwezo wa kukariri aliyofundishwa, kugundua mambo mapya na uwezo wa kukubalika kwenye jamii kutokana na kipaji alichonacho.
Kupata Divesheni 4 kwenye mtihani - sio kwamba huyu kijana hana akili. Nao wapewe nafasi kwenye ajira.
 
Mambo yamebadilika ndugu yangu. Yale mambo ya kutumia nguvu yameshapitwa na wakati. Sasa hivi nchi zinazojitambua kila kitu wanatengeneza wenyewe (wanajeshi wenyewe)
Hawa dvn 4 ndiyo wale wanavunja matofali kwa kichwa, mara analala, gari inapita juu yake. Ukitupiwa bomu nalo utalipiga kwa kichwa?
Tunataka tuone jeshi linatenda haki, watu wamevumbua bunduki, drone, gari n.k
Chukulia makambora 50 yamerushwa kwenye nchi yako, unatumia teknolojia gani kuyalipua yote kabla hayajatua kwenye ardhi yako? Wanaotakiwa kwenda jeshi ni 1-3 hawa utawaendeleza mpk watakuwa na PHD
Jeshi linahitaji madaktari, marubani, wanaIT (teknolojia), wanasaikolojia n.k ukiaangalia ni wasomi ndiyo wanaohitajika.
 
Badala kupigana kugombania ajira tufikirie kuongeza ajira..., Cha maana ni utendaji kazi na uwezo wa mtu kufanya kazi husika, sio cheti chake kinasema nini.

Hivi hujawahi kusikia mtu anaambiwa overqualified ? Sometimes ni bora uchukue mtu average na kumpa training kuliko mtu anayejiona ni qualified na anajua kila kitu kwahio huwezi kumfundisha (theory zimejaa na much know)
 
Sekta kama magereza, uhamiaji, polisi na jeshi walitakiwa waajiriwe watu wenye elimu kuanzia form 6, diploma, degree na kuendelea.
Lengo la kuwajiri waliofeli ni kuendelea kutumika kisiasa leo hii jeshi la polisi limekuwa la kisiasa.

embu taja tasisi moja yenye wasomi wasiotumika.
 
Baadaye huyu form IV wa point 31 anapanda cheo hadi kuwa kamishna wa uhamiaji.
 
Baadaye huyu form IV wa point 31 anapanda cheo hadi kuwa kamishna wa uhamiaji.
Inategemea hio baadae ni muda gani, hivi unadhani wewe hapo na elimu yako ya chuo hakuna jambo ambalo mtu uliyemkuta kwenye kazi husika kwa miaka 15 anaweza kuelewa kukushinda?

Ogopa watu waliopanda from bottom up hakuna cha kuwadanganya wanajua organisation culture inside out (sadly watu tunaangalia shuleni fulani alifanya nini na sio utendaji wake akiwepo kazini) yaani results oriented
 
Nafasi ya uongozi, hata wa ofisi, inahitaji mtu mwenye uelewa mpana na anayeweza kubadilika kulingana na mazingira, si huyu aliyebobea kwenye urasimu wa taasisi. Uhamiaji unahusu ndani yake uchumi, Afya nk.

Mtazamo kama wako ndiyo maana tunazalisha watu wa kusema "Hatufanyagi hivyo." Na ndiyo maana hadi leo wapo wa kusema "Nyerere angefanya hivi na vile."
 
Sasa wakichukua waliofauli nani ataanza cheo cha chini jamani lazima jeshi liwe na watumishi kwanza mengine baadae. Jeshi linaakili sana hawa waliofaulu kwanza wengi hawakai wanakimbia kimbia so jeshi lalitaki hayo mambo sasa
 
Kazi za jeshi hakuna mambo ya division maana wanataka wapiga kazi sio wanaotaka mishahara mikubwa mkuu.
Twendeni kwa Zama ,sera zakuajiri watu wa levo hizo ili kukidhi haja za mishahara imepitwa na wakati kila siku ccm inadai uchumi umekua haya matakataka Yann kwazama hizi...
 
Ishu ya mlema kutaka wafungwa watumike kujenga SGR,ilikuwa kwa sababu ya cheap labour,mfungwa asingelipwa posho tofauti na kijana wa uraiani.
Kwa hili la uamiaji kutaka vijana wenye ufaulu hafifu ni mwendelezo wa upuuzi mwingi unaoendelea kwenye utumishi wa umma.hata jeshini JWTZ ukiwa jeshini n una taaluma fulani kuanzia kiwango Cha diploma,kupata nafasi ya kwenda kusoma uofisa cardet ni mbinde sana ukiuliza unaambiwa vijana wasomi wakipata vyeo wanakimbia jeshi kwahiyo suruhisho ni kuajiri vijana wa kidato Cha sita na kuwapa kipaumbele kuwa maofisa.Jamaa zangu walikuwa na diploma wakajiendeleza Tena kwa mkopo wa serikali wakapata shahada,masters lakini kupewa nyota ikawa mbinde,jeshi likataka wabaki kama private,wakaona uzushi wakapiga jeshi chini.
Alisema Prof Assad asilimia 60 ya watumishi wa umma ni vilaza!!harafu leo Bado wanasisitiza kuingiza vilaza zaidi!!
Miaka kadhaa iliyopita kuna mwamba alisisitiza kwa vile kibaha ajari za magari zimeongezeka basi serikali ijenge hospitari ya mifupa karibu kuwasaidia majeruhi!!hii Kwake aliona ndio ufumbuzi wa tatizo la ajari?!!!!!
 
Duh mpaka Chuo cha mapenzi Kipo?
 
Hali Ya Maisha Mkuu.... Mtu anaona Liwalo na liwe..
Nshapiga degree yangu moja nipo mtaani mwaka wa tatu inatokea nafac ya jeshi... Haikua kazi ya malengo yangu ila kutokana na ugumu wa maisha najitupa tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…