Kutoa ajira kwa waliofeli divisheni 4 tena kuanzia point 28 mpaka 31 ni kutuharibia jamii

Kuna vichwa havitakiwi kupewa nafasi ya kuamua kwa ajili ya taifa.

unapotoa kipaumbele cha ajira kwa div 4 point 28 mpaka 31 na ukawaacha kuanzia pointi 27 kushuka chini na wengi wako mtaani hawana ajira unapeleka taarifa gani katika jamii kuwa kusoma sana hakuna maana? kwamba kufaulu siyo justification ya utendaji sasa kufeli ndiyo justification?

kwa nini wasiseme tunaajiri kidato cha nne na wale wa kidato cha nne wote walioko mtaani wajitokeje kugombania na wao wawachambue kulinganisha sifa mbalimbali ikiwemo elimu, lakini hawa wamekwisha wabagua wenye ufaulu mzuri kwa kuwaonyesha hawana sifa. kama mtu ana div 4 ya pointi 26 au 27 hana sifa.

mimi sielewi kama mnajua mnachokitetea au wale wenye maslahi na hili?
 
unachokiandika kinakubaliana na hoja yangu ila hata wewe hukielewi unakaa kubisha tu. mimi hoja yangu ni wawaite vijana wote waliohitimu kidato cha nne miaka ya nyuma .

kama kuna divisheni 1, 2 mpaka 3 ambao walibahatika kuendelea na kidato cha tano lakini matokeo ya kidato cha sita yakawa mabaya hawakuendelea huyo ataomba. kuna wenye ufaulu mzuri lakini kombinesheni ziligoma na wazazi hawana uwezo wa kuwaendeleza nao wataomba, kuna wengine wana 4 za pointi chini ya 28 lakini hawakwenda popote nao wataomba pamoja na hao wa pointi 28 mpaka 31.


wakiomba hawa watachambuliwa kwa kutumia vigezo vingine pamoja na elimu zao.

kama unasema elimu haionyeshi utendaji wa mtu sasa mtuambie ni kigezo gani kinatumika kuchagua hawa divisheni 4 ya pointi 28 mpaka 31 na kuwaacha wengine?

hawa wenye fikra za hivi itakuwa hata kwenye mafunzo yao wanawatunuku waliofeli ndiyo wanaopewa nishani na promosheni

huwezi kukataa kutambua mifumo ya kupima ufaulu au juhudi za wanafunzi katika kufutailia kile wanachoelekezwa kufanya
 
Kwa hiyo unatuaminisha kwamba 1-3 Wana teknolojia ya wa kulipua makombora 50 yakirushwa?? Elimu ya bongo ni mwenye uwezo wa kukariri ndo anafaulu braza ukijibu kwa ufahamu unafeli. Kuna watu wamesoma hadi PhD lakini ni weupe hamna kitu zaidi ya karatasi la Cheti. Na kama ishu ni hayo makaratasi hata mtu wa division 4 anaweza kuanza certificate Hadi level yoyote. Kumbuka Kuna watu Wana degree na PhD zao ila o-level walikuwa na division four kama hizo ulizozitaja.


Na vilevile ww mwenye division one au 2 unachomzidi division four ni msuli wa kukariri tu yaliyoandikwa ila Kwa mfano mnaweza mkapewa social based interview akakuzidi upeo na kujiamini. Na kuhusu matumizi ya teknolojia, sio kila mwenye elimu kubwa anaweza hiki kitu, Kuna watu Wana degree ila hata kuwasha kompyuta hawajui, ila Kuna form four wa division 4 anachezea kompyuta utadhani aliitengeneza yeye.
 
Siyo wote walio feli hawana akili hapana wengine walifeli kwa sababu za kibinaadamu ikiwemo maradhi kuukamia mtihani na maandalizi mabovu ya mtihani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…