Garama za SWIFT Transfer (Bank Transfer) ni kubwa mno kiasi kuanzia $10 - $700 ni $15.
Kuanzia $701 na kuendelea wana charge 1.5%.
Sasa hapo walio wengi ni ngumu kifikisha zaidi ya $700 labda uwekeleze pesa mpaka zifike $701 ndipo utoe kwa bank transfer.
Njia ambayo huwa naona ni nzuri.
1. Omba virtual card ya EUR, kisha exchange pesa kutoka USD to EUR nadhani wana charge 1.5%
Baada ya hapo tumia Binance USDT kudeposit kwa card ya virtual. Kisha nenda P2P sell USDT zako kwa Mobile Money.
2. Unaweza tumia Paxful au crypto exchange yoyote ile ambayo Ina traders wanao pokea pesa kwa Payoneer kisha weka offer yako na watumie USD zako wao watakupa USDT kisha sell kwenda Mobile Money. Japo njia hii itahitaji Payoneer account yako iwe ilisha wahi kupokea kiasi kisicho pungua USD 500, ndipo watakupa access ya kutumia pesa kwa Payoneer account nyingine kwa muamala uupendao.
Ni hayo tu ndugu.