Yanga FC kafungwa Goli la 2 dakika ya 36 tu ya Kipindi cha Kwanza ya mchezo. Poleni sana wana Yanga FC ila kwa jinsi mpira unavyochezwa naona kuna dalili za Yanga FC hata kufungwa Goli 4 au 5 kama Yanga FC wasipokuwa makini na kuacha kumlalamika Mwamuzi kila mara. Y
Haina noma ' Jombaa ' na mpira sasa ni mapumziko huku Yanga FC ikiwa imeshafungwa Goli 2 kwa 0. Tatizo nililoliona kwa Yanga FC ni kuanza kuhamaki na kutoka mchezoni mapema kitu ambacho kinawapa sana faida wenyeji MC Algiers. Labda niseme tu kwa hizi Timu zetu za Tanzania sasa zijitahidi sana ziwe zinaajiri Wataalam wa Saikolojia ambao watakuwa wanawajenga kimtazamo kila mara Wachezaji wetu ambao na wao kwa bahati mbaya mno hata ' uelewa ' wao tu ni mdogo sana.
Mpaka sasa Yanga FC imefungwa mno Kisaikolojia na siyo ki mpira na hofu yangu ni kwamba kwa jinsi Nadir Haroub ' Cannavaro ' na mwenzake Kelvin Yondani wanavyocheza kwa hasira huku kila mara wakimlaumu Mwamuzi kama wasipojirudi kipindi cha pili nisiwaficheni wana Yanga FC naziona Goli 4 au 5 leo huko Ugenini mlipo.
Nimeweka ' Utani ' wetu pembeni na sasa nachambua kama ' Mdau ' wa kutukuka wa Mchezo wa Soka ( Kandanda ) nchini Tanzania.