Kutoka Algeria: MC Alger 4 - 0 Young Africans

Na mnaohitaji ' updates ' za mechi ya Yanga FC huko Algeria ni kwamba hadi hivi sasa ni dakika ya 21 Yanga FC ameshafungwa ' Kimoko ' yaani goli 1. Kwa mnaotaka kuufuatilia huu mpira just tune in to 94.5 Mhz Sibuka FM wanautangaza. Goli la MC Algiers limefungwa dakika ya 15 na Mchezaji aitwae Mohammed.
Asante kwa taarifa jombaa
 
Kidogo kwa Comment hii nitajifariji kwa yaliyotokea leo kanda ya ziwa

Asante mkuu...!

Yanga FC kafungwa Goli la 2 dakika ya 36 tu ya Kipindi cha Kwanza ya mchezo. Poleni sana wana Yanga FC ila kwa jinsi mpira unavyochezwa naona kuna dalili za Yanga FC hata kufungwa Goli 4 au 5 kama Yanga FC wasipokuwa makini na kuacha kumlalamika Mwamuzi kila mara. Yanga FC wanachezewa sana! Vicent Dante na Geofrey Mwashiuya wanataka kuingia.
 
Ni kweli simba tumechemsha leo. Na huko algeria mpaka sasa 2-0 . Kipindi cha pili yena wanapigwa 2 wanarudi kuyafuta yena ubingwa wa nyumbani.
 
مباشر - مولودية الجزائر × يانغ افريكانز التنزاني …:
 
Mechi ya ubingwa mmechemsha Mwanza...jumanne mnapokwa points za kagera..Yanga bingwa tena 2017 kwa mara ya tatu mfululizo
2b690ff055ff49e5478cdc0ee50172e2.jpg
 
Yanga FC kafungwa Goli la 2 dakika ya 36 tu ya Kipindi cha Kwanza ya mchezo. Poleni sana wana Yanga FC ila kwa jinsi mpira unavyochezwa naona kuna dalili za Yanga FC hata kufungwa Goli 4 au 5 kama Yanga FC wasipokuwa makini na kuacha kumlalamika Mwamuzi kila mara. Y
Asante kwa taarifa jombaa

Haina noma ' Jombaa ' na mpira sasa ni mapumziko huku Yanga FC ikiwa imeshafungwa Goli 2 kwa 0. Tatizo nililoliona kwa Yanga FC ni kuanza kuhamaki na kutoka mchezoni mapema kitu ambacho kinawapa sana faida wenyeji MC Algiers. Labda niseme tu kwa hizi Timu zetu za Tanzania sasa zijitahidi sana ziwe zinaajiri Wataalam wa Saikolojia ambao watakuwa wanawajenga kimtazamo kila mara Wachezaji wetu ambao na wao kwa bahati mbaya mno hata ' uelewa ' wao tu ni mdogo sana.

Mpaka sasa Yanga FC imefungwa mno Kisaikolojia na siyo ki mpira na hofu yangu ni kwamba kwa jinsi Nadir Haroub ' Cannavaro ' na mwenzake Kelvin Yondani wanavyocheza kwa hasira huku kila mara wakimlaumu Mwamuzi kama wasipojirudi kipindi cha pili nisiwaficheni wana Yanga FC naziona Goli 4 au 5 leo huko Ugenini mlipo.

Nimeweka ' Utani ' wetu pembeni na sasa nachambua kama ' Mdau ' wa kutukuka wa Mchezo wa Soka ( Kandanda ) nchini Tanzania.
 
Shida ya timu zetu zinacheza vizuri sana kwenye magazeti.
 
Back
Top Bottom