FATHER OF HISTORY
JF-Expert Member
- Aug 15, 2012
- 915
- 638
View attachment 1009987
ASASI isiyo ya kiraia ya Alliance For Democratic Organization (ADO) imewapongeza wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa huku ikiwataka baadhi ya wanasiasa kutoka vyama vya upinzani kuheshimu maamuzi hayo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa asasi hiyo Habib Mchange, alisema kupitishwa kwa Muswada huo ni hatua kubwa kwa siasa za Tanzania na zaidi wanachama wa vyama hivyo na wananchi kwa ujumla.
Alisema anaamini hatua hiyo italeta mabadiliko makubwa na hasa katika kuweka uwazi na uwajibikaji katika uendeshaji wa vyama vya siasa na kuondoa kila aina ya ubabaishaji aliodai umekithiri ndani ya siasa za Tanzania tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi. “Kwa dhati kabisa niwapongeze wabunge wote waliokuwa mstari wa mbele kuhakikisha muswada huu unapita ili uweze kuleta mabadiliko ya kweli katika siasa za Tanzania tukiamini kuwa sote lengo letu ni moja kuijenga nchi hii,” alisema Mchange. Aidha alisema endapo Muswada huo utasainiwa na Rais na kuwa sheria, mapendekezo yake kwa serikali ni kwamba isiishie kubadili vipengele vilivyomo ndani, bali inapaswa iende mbali na kuwachukulia hatua watu wote watakaokwenda kinyume na sheria husika.
How, tapeli ni nani. Habibu si yule wa CCM. NGO hii kaianzisha lini?Ha ha ha ha ha ha ha matapeli hawaishi mjini!
Inasikitisha sana.
Hali tete mkuu,Ha ha ha ha ha ha ha matapeli hawaishi mjini!