Uzoefu unaonyesha kuwa endapo jambo lolote likienda kujadiliwa bungeni na ukaona wa bunge wa CCM wanaliungana mkono japo kwa hoja dhaifu na hoja za msingi zikawa zinatolewa na wabunge wa vyama vya upinzani na jambo hilo likapitishwa; majibu yake ni kwamba jambo hilo halina tija na maslahi mapana kwa watanzania walio wengi, ni mwendelezo wa dharau kwenye jukwaa la kimataifa, kwa maana nyingine halina tija kwa taifa letu zaidi wanaonufaika ni watanzania wachache na wageni.
Hii ina maana kuwa, CCM, wabunge wake, na viongozi wake pia hawana nia nzuri na nchi hii na ndiyo maana tangu tumepata uhuru hadi hivi sasa bado tuko kwenye kundi la nchi masikini LDCs wakati jirani zetu Kenya na Rwanda wamekwisha toka huko kitambo na sisi pamoja na rasilimali nyingi tulizonazo bado hazitusaidii tu; ni aibu kweli kweli, budget ya nchi hadi hivi sasa bado ni tegemezi.
Bado hadi muswada kama huu wenye mapungufu kibaoooo tena ya msingi halafu umepitishwa!! Yaani hawa jamaa ni hovyo kabisa sijapata ona katika dunia hii ya sasa.