Kutoka Butiama: Exclusive news


nimeinama, nimeinuka, nimeokota kidude .......sawa nimekusikia, sasa tuongelee mada na si mchangia mada !
 
CCM ni sawa na nyumba iliyojaa wadudu, na mbaya zaidi mwenye nyumba anaamini wadudu hao wataruka na kuondoka wenyewe!! Kwa mtaji huo kila kukicha wanazidi kuzaliana ...

duh, post ya kwanza tu umemquote kada ! nadhani nitakukumbuka hapa think BIG ! karibu yakhe !
 

kuweka maua sio bigi deal, pengine (sina uhakika) walifanya hivyo mara ya mwisho hivyo picha hawakupigwa, it just happened kwamba kikao hiki kinafanyika butiama, hivyo wakaamua kwenda kumkumbuka muasisi wa chama chao !
hata wewe unaweza kwenda kuweka maua, na SIDHANI KUWEKA MAUA KATIKA KABURI LA NYERER NI UNAFIKI ! NAKATAA ! ebu kama utaweza kuikuza hiyo picha naomba ufanye hivyo halafu nitajie mafisadi unaowaona wewe katika hiyo picha ! Picha hiyo hiyo uliyoweka !

(Najua mafisadi wengine watapigwa picha wakiweka maua hizo labda zaweza kutoka siku 1-2-3 from now) lakini kilichokufanya mainly uandike ni hiyo picha, so plz call out a few names ya hao unaowaita wanafiki !

yule wa kati kati kafanana na kinana, sijui kama ni yeye !
 
Kamanda tulia, naona unajihami ili Mnyika asiitwe hapa
 

Ni unafiki kwa sababu maadili ya Mwalimu yote kama uongozi bora, kuwajali Watanzania, kutokuwa na tamaa ya utajiri, kuwa mkweli kwa wananchi mambo ambayo Mwalimu aliyaenzi sana sasa hivi katika hii CCM ya mafisadi hayamo. Sasa kama mambo ambayo muasisi wa chama aliyoyatukuza sana na CCM leo hawayafuati, halafu eti kwa kuwa wako Butiama basi kila fisadi anataka kuweka ua kwenye kaburi la Mwalimu! wakati huo huo mafisadi wa EPA bado wanatesa mtaani hata kutajwa wanaogopa eti wakitajwa nchi italipuka, mafisadi wa Richmonduli bado wanatesa mtaani sasa huo kama siyo unafiki nini. Sina haja ya kuwataja mafisadi kwani CCM inajulikana kama ni chama cha mafisadi, wanashindana nani atakuwa tajiri zaidi kuliko mwingine, wakati wananchi wanaumia.

Enzi za Mwalimu wote hao angeshawasweka lupango na mali zao kutaifishwa mara moja bila hata kukawia na wala nchi isingelipuka
 

hold hold hold on ! wewe, uchafu wa wapuuzi wachache haimaniishi wote ni wachafu, na ndio maana nikakwambia niambie ni wangapi katika hiyo picha ni mafisadi, naona jii kimya ! Najua umetumia kigezo cha hiyo picha ya "watu safi" na kusema chama kizima ni kichafu. Lakini hiyo siyo, unajua ccm ina viongozi wangapi ?? kati ya hao ni wangapi wachafu ? na wangapi ni safi ? hata half haifiki, which is not even to make a conclusion kwa chama kizima ! CCM INA VIONGOZI ROUGHLY 7,000(sina uhakika). Kati ya hao naweza kusema pengine ni 120 ni mafisadi hodari na waliobobea, 400 mafisadi wadogowadogo (hawa kesi zao sana sana serikali za mitaani, sijui michango ya nyumba hadi nyumba) na hao wengine wooooooooote ni safi ! upo hapo !
Hayo maadili ya Nyerere hayafuatwi na viongozi wa ccm wangapi ? Najua ni wachache na sio wote, so kusema chama kizima thats totally ridiculous !
Hata mimi ningekuwa na hayo mamlaka ningetaifisha mali za mafisadi wote na kuwasweka lupango lakini chama chao ningewaachia na kutokikejeli maana najua wengine watakuja na kuendeleza hayo unayoita maadili ya nyerere !
Uongozi ni ubinaadamu, hata hayo maadili ya nyerere ni ubinaadamu ! So, tunataka viongozi watakaolinda maslahi/haki ya mwanadamu !
Kwa nini wewe usifanye msaada wa kutaja mafisadi wa EPA ili usaidie taifa ? wengine hatuwajui ! ila najua mimi simo !
 

Hawa ni sawa na Fisi aliyejigunisha pembe za mbuzi na kuvamia mkutano wa nyumbu nyati na mbawala.

Unajua nini kitamwumbua?

Jua likizidi gundi inayeyuka, hapo ana uchaguzi, atoke Benz au ashikilie pembe zake zisidondoke. Kwi kwi kwi kwi.

Mungu kamwe hawafichi wanafiki.
 

Samaki mmoja kati ya wengi wanaoshare mchuzi kwenye chungu kaoza, waliobaki wazima kweli? MmmH!
 
Samaki mmoja kati ya wengi wanaoshare mchuzi kwenye chungu kaoza, waliobaki wazima kweli? MmmH!

swadakta yakhe ! utakaochacha ni mchuzi, samaki watakuwa fresh hata siku 2 zaidi, ila mchuzi ndio utakaowafanya samaki wanuke, na "waafrika" tutadhani samaki wote wamechacha yakhe ! kwa hiyo mie sikulaumu ! acha nkachokoe chaza mie !
 

Wote ni mafisadi tu ndio maana wamekaa kimya bila hata kuguna wakati mafisadi wa BoT na Richmonduli wakiendelea kutesa. Utakuwaji msafi halafu hata usigune na kuuliza jamani kulikoni? mbona hawa mafisadi waliokupua mabilioni ya pesa bado wameachwa mtaani wakiendelea kutesa na pesa zao walizokupua? Kwanini wasitupwe lupango wakati uchunguzi ukiendelea? Inakuwaje mkuu wa polisi nchini anasema hawa mafisadi ambao wamevunja sheria za nchi wakitajwa nchi italipuka? Wao ni nani hasa katika serikali ya Tanzania mpaka waogopewe hata Rais akivunja sheria za nchi inabidi aswekwe lupango? Lakini njemba za ufisadi zimekaa kimyaaaaa kama kila kitu ni shwari zimeweka mbele maslahi yao wenyewe na yale ya CCM wakati nchi inaangamia halafu zinadai eti zinaweka maua katika kaburi la Mwalimu eti kumuenzi Mwalimu! Watanzania sio wajinga kiasi hicho! unafiki wenu unatia kichefuchefu!
 

unajua tajiri hii mada ni nzuri sana kuliko wengi wanavyodhani au pengine vile wewe hukutegemea ! Na hadi hivi sasa mjadala ni mzuri na nafikiri utakuwa mzuri zaidi pale utakapotaja wangapi wa hao unaowaita mafisadi wameweka maua kwa kutumia picha hiyo uliyosema ! SIPINGI YALE ULIYOSEMA KWAMBA MAFISADI WAPO, TENA MITAANI WAKITANUA, lakini ukweli lazima utasimama na nitausimamia, !! Swali simpo nimekuuliza, maana najua umetumia hiyo picha ili kuleta hii mada, na isingekuwepo hiyo picha sidhani kama hii thread pia ingekuwepo, ndio maana nikasema wataje au tutajie idadi ya "hao mafisadi waliomo kwenye hiyo picha uliyotumia kuandika hii thread".

Mafisadi ni watu wabaya sana, tena sana !
Lakini huwezi kutumia ubaya wa hao mafisadi na kuwapaka wengine rangi ya mafisadi ! Wao kukaa kimya haimaanishi kwamba nao ni mafisadi, unaweza ukapiga kelele bungeni kwa kuwakemea mafisadi ILI HALI WEWE MWENYEWE FISADI VILE VILE ! So, kimya kisikushitue mzee, kobe akiinama chini ujue....................... !!

Nia yangu sio kutetea mafisadi, ila isipokuwa mwenzetu umeona kwa kuwa wamevaa mashati ya kijani kibichi basi ukajua nao wamo, kumbe hawamo ! Maana najua hao watu maskini ya watu wameenda kwa nia njema, and from nowhere out the ordinary, mtu anawaita fisadi, ufisadi huo ni kwa kuvaa shati la kijani na kuweka maua katika kaburi au ufisadi upi huo ? na kama wa EPA, ni yupi kati ya hao alishiriki ? au ufisadi wa buzwagi ? nani kati yao alishiriki ? au Richmond ? yupi kati yao alishiriki ? I GUESS ITS NONE ! Sasa kama unataka kudeclear kwamba kuvaa shati la kijani ni ufisadi, COUNT ME IN !
 

sasa kama unajua kada ni fisadi, mbona wewe na wenzako (ambao "tunaendesha" kampeni ya kuadhibu mafisadi) mnaniachia iwapo mnajua mimi ni fisadi ? basi hata kutoa taarifa TAKUKURU unashindwa ? aah yakhe, tufanyie favor bana, ebu nenda TAKUKURU waambie waje wanikamate haraka sana ili nisipete mitaani ! Na itabidi mapesa yote niyarudishe ! teh teh, hata hiyo JF sijui kama ningekuwa naijua iwapo ningekuwa na hiyo mihela. Ningekuwa nalala brunei, naamka malaysia, lunch bukoba dinner sauzi !
 


Nikakujibu hivi, Utakuwaji msafi halafu hata usigune na kuuliza jamani kulikoni? mbona hawa mafisadi waliokupua mabilioni ya pesa bado wameachwa mtaani wakiendelea kutesa na pesa zao walizokupua? Kwanini wasitupwe lupango wakati uchunguzi ukiendelea? Inakuwaje mkuu wa polisi nchini anasema hawa mafisadi ambao wamevunja sheria za nchi wakitajwa nchi italipuka? Wao ni nani hasa katika serikali ya Tanzania mpaka waogopewe hata Rais akivunja sheria za nchi inabidi aswekwe lupango? Lakini njemba za ufisadi zimekaa kimyaaaaa kama kila kitu ni shwari zimeweka mbele maslahi yao wenyewe na yale ya CCM wakati nchi inaangamia?

Eboo! usitake kuniingizia maneno kinywani mwangu, eti kuvaa shati la kijani ni ufisadi!, kwani wako wana CCM mafisadi wengi hawavai hizi rangi za kijani na bado ni mafisadi wakubwa tu

Hivi hao waliokuwa wasafi ndani ya CCM hawasikii kelele za Watanzania kila kona ya nchi yetu wakasimama kidete ili kukisafisha chama hicho? 😕
Kama wapo mbona hatuwasikii wanaogopa nini kusema yale yanayopigiwa kelele na Watanzania kila kukicha. Kimya chao hao wasafi ndani ya CCM kinaashiria nini? Kumbuka kimya kingi kina MSHINDO!
 


mkuu kipengele cha 13 hadi 21 mbona hujaviorodhesha?


jengine si lazima kikao hiki kiangalie vipao mbele ulivyovitaja kuna mengi ya kujadiliwa.

subiri uone au unataka useme mie niliwahi kusema?


na jua pia ikiwa kinyume watu watakucheka na kushusha
 
bana wewe naona umekuwa mgumu kuelewa, nimekwambia kupigia kelele ifisadi isikusumbue, kwani EL hakupigia kelele huo ufisadi ? Naaam, see you get it now ! Hivyo ndivyo ninavyomaanisha, kukaa kimya haimaanishi kwamba unaunga mkono ufisadi, la hasha ! si unakumbuka hata wengine walidiriki kusema "hata angekuwa mume wangu ningemtaja"......tooooo late, baada ya kujua bunge litakuwa sucked up ! Anyway, watu wanapigia sana kelele kuhusu ufisadi !

Kumbuka: Kupigia domo ufisadi haimaanishi wewe sio fisadi ! ref: EL & MBOWE)
 
kuna picha kwa michuzi, nimeshindwa kuziweka hapa ! wekeni jamani !
 
yote ni sehemu ya uchambuzi wa habari Mtu wa Pwani, kwani nani kasema tuko katika mashindano? Tatizo ni nyinyi ambao mnasubiri mwanakijiji aboronge ili mumshushue lakini akiwa sawa mnapata kigugumizi. Well, nimejifunza kuishi na pande zote mbili za maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…