Hii nimeipata kutoka kwenye gazeti la RA ...
Kumekucha Butiama
na mayage s. mayage,butiama
KARIBU wajumbe wa NEC Musoma Bila CCM madhubuti nchi itayumba. Hayo ni miongoni mwa maneno yaliyoyapamba mabango ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), yaliyotapakaa katika mji wa Musoma na vitongoji vyake, kuashiria kuanza kwa Kikao cha Halmashauri Kuu leo kijijini Butiama.
Kwa kuyaangalia mandhari tu ya mabango hayo, ni wazi yanaongeza hofu juu ya hatima ya chama hicho kuweza kugawanyika kufuatia tofauti za wazi kujitokeza kutokana na hali halisi ilivyo ndani ya chama hicho tawala.
Kikao cha NEC kinachoanza leo kimetanguliwa na vikao viwili, kile cha Sekretarieti ya chama hicho iliyokutana katika Ofisi ya CCM mjini Musoma jana, chini ya Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba na Kamati Kuu iliyoongozwa na Mwenyekiti, Rais Jakaya Kikwete, kijijini Butiama jana jioni.
Kamati Kuu (CC) ya chama hicho ilipangwa kukutana jana jioni. Hata hivyo, kikao hicho hakikufanyika na badala yake, wajumbe walipewa makabrasha wakayasome ili washiriki kikamilifu kikao cha CC, ambacho kinaanza leo asubuhi, baada ya kuahirishwa jana jioni.
Pamoja na agenda za NEC kutajwa wazi kuwa ni pamoja na kuzungumzia hali ya kisiasa na muafaka wa kisiasa kati ya CCM na CUF, bado wajumbe wa kikao hicho wameelezwa kuwa na mambo mazito vifuani mwao wanayotarajia kuyaibua watakapopewa nafasi ya kuchangia ama kuuliza maswali.
Hali hiyo imeelezwa kuelemea zaidi katika hali tete ya kisiasa ambayo imetokana na matukio ya kashfa za ufisadi kuhusishwa kwa viongozi wa juu wa serikali na watendaji wao na hatua kuchukuliwa na Bunge na baadaye serikali, bila chama kuchukua hatua.
Kashfa mbili nzito zilizoitikisa CCM na serikali yake, ni ile ya mradi tata wa umeme wa dharura uliokabidhiwa kwa kampuni ya Richmond Development LLC na ile ya Akaunti ya Fedha za Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), zote zikiihusisha kwa karibu mno serikali na chama tawala kupitia watendaji na wafadhili wake. Sakata la Richmond lilisababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, na mawaziri wawili, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha, ambao wote kwa kupishana waliongoza Wizara ya Nishati na Madini, iliyotekeleza upatikanaji wa mradi huo tata ambao umekua wimbo kwa wananchi.
Rais Kikwete alilazimika kuunda upya baraza lake la Mawaziri, likiongozwa na Mizengo Pinda, ambaye aliunda timu ya wataalamu kutekeleza mapendekezo ya Kamati ya Bunge iliyochunguza mradi wa Richmond, wataalamu ambao wamekwisha kumkabidhi ripoti yao.
Habari kutoka katika vyanzo kadhaa vya ndani ya CCM, zinasema ripoti hiyo ya wataalamu wa Pinda, huenda ikajadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu cha jana jioni, hoja ambayo inaweza kuibua mjadala ndani ya vikao hivyo vya CCM, ambavyo kwa mara ya kwanza vinafanyika kijijini Butiama, alikozaliwa na kuzikwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Kufanyika kwa kikao hicho Butiama kumeibua hisia kutoka kwa baadhi ya wajumbe ambao katika mazungumzo yao yasiyo rasmi hapa mjini Musoma, wanasema kwamba Mwalimu Nyerere aliwakataa baadhi ya watu ambao sasa ndio wamesababisha kuchafuka kwa chama chao na serikali yake, na kwamba ni lazima chama kichukue hatua za haraka kujisafisha.
Kauli za Mwalimu Nyerere zimekuwa zikirejewa na baadhi ya wajumbe wa NEC na wananchi, ikiwamo hiyo iliyotapakaa katika mabango katika barabara iendayo Butiama, ya kwamba Bila CCM madhubuti, nchi itayumba. Hiyo tu inaonyesha kwamba yapo mambo mazito yanayoweza kuibuka ili kukirejesha chama hicho kwenye misingi iliyoachwa na mwasisi wake.
Ukiacha hatua ya Katibu Mkuu, Yusuff Makamba kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kufafanua ajenda na sababu za kufanyia kikao hicho Butiama, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, alikaririwa na magazeti jana akisema moja ya masuala yatakayojadiliwa ni maadili ya viongozi wa chama. Hilo halikuwa moja ya ajenda zilizotajwa na Makamba.Kwa ujumla kumekuwa na hali ya kutoaminiana miongoni mwa wana CCM na viongozi wao na kampeni za chini kwa chini zimekuwa zikifanyika ama kwa nia ya kuwamaliza baadhi ya watu au kuwabeba na kuwaokoa wana CCM waliotuhumiwa.
Wasiwasi huo unafuatia kuwapo tetesi za baadhi ya wana CCM kupendekeza kwa chama kuwachukulia hatua wale wote waliotajwa au kuhusishwa na ufisadi ili kukitenga chama na tuhuma hizo ambazo zinaelekea kuhatarisha mshikamano wa chama hicho.
Viongozi wote wa juu wa CCM, akiwamo Rais Kikwete na Waziri Mkuu Pinda, walikwisha kuwasili Butiama jana mchana tayari kwa vikao hivyo, huku kukiwa na taarifa kwamba kama ilivyo kawaida ya vikao vya NEC, waandishi wa habari hawataruhusiwa kuwamo ndani ya ukumbi wakati wa kikao.
Source: Mtanzania
Kumekucha Butiama
[*]Wajumbe waficha siri kubwa moyoni
[*]Mijadala yanguruma hata kabla ya kikao
[*]Kikao cha NEC kinafanyika leo, kesho
[*]Nukuu za kauli za Nyerere kila mahali