Kutoka Butiama: Exclusive news

Kutoka Butiama: Exclusive news

Kikao kimeanza, Gavana Ndullu anawasilisha ripoti ya hali ya uchumi.

Waandishi na watu wote wasiokuwa wajumbe wanatakiwa kutoka nje ya eneo la mkutano tena nje kabisa ya fensi na baadhi ya waandishi wanaanza safari ya kurudi Musoma.

More updates to follow
 
Kama nilivyoahidi: Wajumbe wamewasili muda si mrefu tokea Musoma, kikao kimeanza na JK anatoa hutuba fupi sasa

Points to note are as follows:

Mkapa, Mwinyi na Sumaye hawajahudhuria katika kikao hiki Butiama.

Dr. Shein kafiwa hatoweza kuwepo katika kikao hiki.

More info to come

Mkuu Mimi inanisumbua hawa wanene kutohudhulia kikao hiki.SUMAYE niko nae kwenye ndege na tunashuka Boston saa sita mchana huu kwa masaa ya USA.Leo na mimi mshamba wa majita nimepata zali la kupanda ndege,sijui nitaota!!Ok ngoja nijivute nikamdodose mkuu kama hatojali anambie nini kimemsibu hasiende kule Butiama.
 
Rudi kwenye mada yangu ya "Butiama Kumewiva"... msiwe na wasiwasi nzi wa KLH News haendi kokote kajibanza kwenye kuta zao...
 
Note JK's message in Butiama (a few seconds ago):

"NEC kwa kawaida huwa ni kikao kizito na kinachotoa maamuzi mazito; kwahiyo wanaofikiria kuwa kuna maamuzi mazito yatatokea hawajakosea. Lakini hayatakuwa maamuzi ya kubadili maamuzi ya kisera na kiitikadi katika uchumi au kisiasa; hatutabadili na kuanza kutaifisha mali au kubadili na kufuta siasa ya vyama vingi."

Sasa kazi kwenu kuutafsiri usemi huo

Tatizo Kikwete is Full of words than actions. Unaweza kusikia maamuzi magumu yenyewe makada wa sisiem wamehamishwa vituo kutoka wilayani kwenda mikoani.

Mimi bado siamini maneno yake hadi nitakaposikia YONA, MKAPA, LOWASA, KARAMAGI, MRAMBA, CHENGE, na wengine wamenyang'anywa uanachama
 
Note JK's message in Butiama (a few seconds ago):

"NEC kwa kawaida huwa ni kikao kizito na kinachotoa maamuzi mazito; kwahiyo wanaofikiria kuwa kuna maamuzi mazito yatatokea hawajakosea. Lakini hayatakuwa maamuzi ya kubadili maamuzi ya kisera na kiitikadi katika uchumi au kisiasa; hatutabadili na kuanza kutaifisha mali au kubadili na kufuta siasa ya vyama vingi."

Inaonekana upinzani unamkosesha usingizi na kuna siku huwa anaota kufuta mfumo wa vyama vingi. Ajabu ni kwamba inaelekea anafikiri NEC ya chama chake ina uwezo wa kufuta mfumo wa vyama vingi! cha kujiuliza, kama wanakaa huko siku zote na kusababisha watu kuhangaika nchi nzima na hapa JF watu kufungua thread na thread, halafu wanasema hawajaenda kubadili maamuzi ya kisera,maanake ni nini kama sio kwamba this is business as usual. Waingereza wangeweza ku-summarise yote hii kwa neno moja tu: incompetence. Uzuri kuna watu bado waanamini kwamba kufukuzana watu wawili watatu ni maamuzi mazito kwa nchi, kwa hawa wote tunawatakia kila la heri na mategemeo yao kwenye mkutano huu!
 
Rev.Kishoka,
Katiba ya CCM inaweka Chama mbelena si Taifa, Katiba inasema mwanachama na kiongozi wajibu wake na uaminifu wake ni kwa Chama kwanza na si Taifa
Mkuu hii ni hatari kubwa sana, naomba sana tuijadili bila kujali tofauti zetu ktk mitazamo ya vyama.
Katiba inayosema maslahi ya chama mbele ya Taifa inatisha sana!...tafadhali naomba nukuu ya kifungu hicho mkuu.. duh! sikuwahi kuiona.
 
Mimi hii ya kuwatimua waandishi ndo imenifanya nipige mluzi!

Hili ndio kawaida ya mikutano mikubwa ya CCM, kuanzia enzi za Nyerere, ilififia kidogo wakati wa Mwinyi, ikarudi sana wakati wa Mkapa. Kwa hiyo mzee this is rather a platitude!
 
Rev.Kishoka,

Mkuu hii ni hatari kubwa sana, naomba sana tuijadili bila kujali tofauti zetu ktk mitazamo ya vyama.
Katiba inayosema maslahi ya chama mbele ya Taifa inatisha sana!...tafadhali naomba nukuu ya kifungu hicho mkuu.. duh! sikuwahi kuiona.

Sijasoma katiba ya CCM kwa muda sasa, lakini naamini hii ni exaggeration of the highest order!
 
Note JK's message in Butiama (a few seconds ago):

"NEC kwa kawaida huwa ni kikao kizito na kinachotoa maamuzi mazito; kwahiyo wanaofikiria kuwa kuna maamuzi mazito yatatokea hawajakosea. Lakini hayatakuwa maamuzi ya kubadili maamuzi ya kisera na kiitikadi katika uchumi au kisiasa; hatutabadili na kuanza kutaifisha mali au kubadili na kufuta siasa ya vyama vingi."

Sasa kazi kwenu kuutafsiri usemi huo

Jamani kuuliza si ujinga::

Kikao ndio kwanza kinaanza na kina wajumbe 200, sasa JK amejuaje kuwa maamuzi yatatokea kabla wajumbe wa NEC hawajamua au kuvote??
Hawa wajumbe ni rubber stamp au??

Kuhusu Mkapa tuliwaambia siku nyingi kuwa hawezi kuhudhuria mkutano.

Leakage za CC zinaconfirm kuwa kama tulivyosema mwanzo maamuzi ni kuhusu CUF/CCM only na kutakuwa na blah blha nyingine lakini nothing serious unless wanataka kutushangaza.

Wajumbe tuleteeni latest
 
Yale yale ikitajwa CCM basi tuje negative...

Kwa hakika NEC ya CCM iiendelee kuwaalika Gavana, CAG, AG, PCCB bosi etc... pale wanapoona wanataka na wao wapate details kutoka kwa watendaji moja kwa moja kuliko kutoka kwenye secretatiat yao..

Hili ni jambo zuri sana... kwa taifa letu.

Mikutano ya NEC inaanza kuwa makini zaidi.

Kwa hakika pia taratibu naona tutaelekea kule ambapo watendaji hawa wataweza kukalishwa chini kwenye kitimoto na Bunge la Jamhuri moja kwa moja, tuache CCM wawatumie baadaye tuwaambie kama yawezekana kwa NEC ya CCM kwanini isiwezekane kwa Bunge la Jamhuri... I can see some light from the tunnel
 
Just curious, why do we always appear to be obsessed and overwhelmed by these CCM meetings? Do we expect anything different from their usual ways doing things: cover up, mockery, manipulation of truth and lies, n.k? It seems like some people are expecting some CCM gurus to be fired, have you asked yourself for what and how will that help JK ovecome his shameful incompetence? Do you still doubt that the root of our problems is systemic rather than a problem of a few unscrupulous individuals in CCM? And finally, what makes it good for Mkapa, Mwinyi and Sumaye not to have attended this business as usual CCM meeting?

Thanks Kitila, there will be nothing new from the pretenders, as I said it before.
 
Jamani kuuliza si ujinga::

Kikao ndio kwanza kinaanza na kina wajumbe 200, sasa JK amejuaje kuwa maamuzi yatatokea kabla wajumbe wa NEC hawajamua au kuvote??
Hawa wajumbe ni rubber stamp au??

Mambo mengine ni rahisi kuelewa, hivi kuna jambo kubwa laweza kutokea lisokuwa ndani ya Ajenda!!!

Kama wajumbe waki-raise kitu kwa hakika kitakuwa kwenye AOB... na kitaambiwa kitajadiliwa kwenye kikao kingine... so if u understand logic... Utaelewa kabisa kwamba hakuna maamuzi makubwa yatatokea kwenye kikao hiki.
 
Yale yale ikitajwa CCM basi tuje negative...

Kwa hakika NEC ya CCM iiendelee kuwaalika Gavana, CAG, AG, PCCB bosi etc... pale wanapoona wanataka na wao wapate details kutoka kwa watendaji moja kwa moja kuliko kutoka kwenye secretatiat yao..

Hili ni jambo zuri sana... kwa taifa letu.

Mikutano ya NEC inaanza kuwa makini zaidi.

Mikutano "makini" lakini utekelezaji SIFURI! Ile ripoti ya BoT tangu ikabidhiwe wengi wetu tulitegemea kwamba wahusika wote watasweka lupango mara moja na kufunguliwa mashtaka bila kujali nyadhifa zao za sasa au zilizopita, lakini kinachoendelea ni usanii tu. Sasa kuna umuhimu gani wa kuwa na mikutano ya NEC ambayo ni "makini" kuimba nyimbo nyingi za kujipongeza kwamba wao ni nambari na wameshika "hatamu" halafu ikija kwenye utekelezaji ni SIFURI.

Tuambie chochote kile ambacho CCM kama chama ambacho wamekifanya ni positive katika miaka ya karibuni, kingekuwepo wananchi wasingeanza kuwazomea watendaji wa juu wa CCM pale wanapotaka kuendeleza usanii.
 
Sijasoma katiba ya CCM kwa muda sasa, lakini naamini hii ni exaggeration of the highest order!

Inawezekana kabisa katiba ya CCM haisemi hivyo lakini utendaji wao unaonyesha dhahiri kabisa kwamba siku zote maslahi ya CCM yatapewa kipaumbele kuliko yale ya nchi. Si katiba hiyo hiyo inasema sera za CCM ni za kijamaa? Hivi nani anaamini kwamba Tanzania ya leo inaendeshwa katika sera za kijamaa?
 
FMES,


Katiba ya CCM inaweka Chama mbelena si Taifa, Katiba inasema mwanachama na kiongozi wajibu wake na uaminifu wake ni kwa Chama kwanza na si Taifa. Hili ni kosa, ndio maana nasema nakuwa vigumu kwa Bunge kuwa na nguvu kuliko NEC! Ndio maana unaona watu wengine hukimbilia kugombea NEC na si Ubunge!

Rev. KIshoka,

Ni kifunga gani hicho cha katiba ya CCM kinasema hivyo? Katiba iko online, ingelikuwa vizuri kama ungecheck kwanza kabla ya kuja na dai kubwa kama hilo.

Katiba ya CCM na pia vyama vingine vya siasa Tanzania hazina kitu kama hacho.

Nakushauri uisome tena. CCM wana makosa mengi sana lakini inabidi tuwafunge kamba kwa facts na sio kuweka hata mambo ambayo hayapo. Tukifanya hivyo na sisi tunageuka na kuwa sawa na hao CCM
 
Rev. KIshoka,

Ni kifunga gani hicho cha katiba ya CCM kinasema hivyo? Katiba iko online, ingelikuwa vizuri kama ungecheck kwanza kabla ya kuja na dai kubwa kama hilo.

Katiba ya CCM na pia vyama vingine vya siasa Tanzania hazina kitu kama hacho.

Nakushauri uisome tena. CCM wana makosa mengi sana lakini inabidi tuwafunge kamba kwa facts na sio kuweka hata mambo ambayo hayapo. Tukifanya hivyo na sisi tunageuka na kuwa sawa na hao CCM


Mtanzania kujua maneno ya Rev.Kishoka si lazima uende Dodoma ama Butiama bali matendo yao kuanzia JK na wote .Kila wakisimama hata Bungeni wote wanaongelea CCM yao na si Tanzania yetu .Hadi wameona aibu sasa Spika kasema wapunguze majigambo na kupongezana na kurukia point.JK majuzi anatangaza baraza la Mawaziri alimaliza kwa kusema Kidumu Chama chao na si Mungu tubariki watanzania na Tanzania .

Kila siku watu wanakuja hapa na kudai kwamba hii forum ni wana Upinzani wote kwa kuwa hawasemi vyema mambo ya CCM na Serikali na majibu yangu ni kwamba ni CCM na Serikali yao wanajenga chuki kwa Watanzania sisi kwa matendo yao ya kutugeuza watoto waodogo ndiyo maana watu waa hasira na CCM na wao kuishia kununua kura toka kwa watu masikini .

CCM kama kweli wanataka heshima basi wakubali mapitio ya Katiba na kubadili vipengele muhimu ambavyo vina lalamikiwa hapa .Wachukue maamuzi mazito kuleta mageuzi na kubadili maisha ya Mtanzania waone kama sisi hatuwezi kuwapa suppoprt zetu. Lakini mambo ya Ngereja na muswada wa Umeme unadhani tunaweza kuwaelewa Serikali na CCM yao ? Kuwapa watu mchele mbovu wakai wa shida , Makamba kwenda kupiga debe kwa walio vunjiwa nyumba na huku anaonya kwamba jambo hili lisiwe la kisiasa .Ujinga mtupu.
 
Rev. KIshoka,

Ni kifunga gani hicho cha katiba ya CCM kinasema hivyo? Katiba iko online, ingelikuwa vizuri kama ungecheck kwanza kabla ya kuja na dai kubwa kama hilo.

Katiba ya CCM na pia vyama vingine vya siasa Tanzania hazina kitu kama hacho.

Nakushauri uisome tena. CCM wana makosa mengi sana lakini inabidi tuwafunge kamba kwa facts na sio kuweka hata mambo ambayo hayapo. Tukifanya hivyo na sisi tunageuka na kuwa sawa na hao CCM
Inawezekana kifungu hicho cha katiba hakipo..lakini ni wazi kwamba party influence is absolutely unquestionable!Nenda kawaulize wabunge wa upinzani watakueleza kuwa nani mwenye respect kati yao na wadau wa CCM na utagundua kuwa psychologically...its more likely to find a comfort zone within the rulling party rather than being in the zone of national interests where you might find yourself in big troubles like you've never even imagined before!(THE LIKES OF ZITTO BEING EXPELLED/SUSPENDED FROM THE PARLIAMENT DUE TO THE RULLING PARTY'S INFLUENCE RATHER THAN CONSIDERING THE NATIONAL INERESTS)You will therefore come to the conclusion that..THE RULLING PARTY HAS MORE INFLUENCE THAN THE PARLIAMENT?
 
Mkuu Wangu Kishoka,

Heshima mbele mkuu, maneno yako hapo juu mengi ni kweli isipokuwa tu hujasema tatizo lilipoanzia mpaka tukafikia hapa tulipo. Toka tulikotoka TANU/CCM kilikuwa ni chama kilichokuwa chini ya uongozi wa kiongozi mmoja, viongozi wengine wote walikuwa wameaminishwa kuwa hawakuwa na uwezo wa kuweza kuwa viongozi wa kufikiri independently, wananchi wote tulikuwa tunafuata idea za huyu kiongozi mmoja, bila ya kuuliza wala kukataa, sasa siku alipoondoka ulitegemea itokee miujiza?

I mean, matatizo tuliyonayo sasa as a nation, ni yetu wenyewe lakini unapotaka kwenda deep as of your analysis kwa maoni yangu ni we have to go deep pia kutafuta why tupo tulipo, kabla ya kutafuta solution. Ukweli ni kwamba matatizo yetu ni vivuli vyetu wenyewe taifa zima no one to be spared. Baada ya kututawala for about 23 years chini ya chama kimoja, one day the kiongozi akaamua kutoka, akatuchagulia wa kumrithi ambaye wa all know kuwa hakuwa na uwezo wa kutosha kama tulivyoambiwa, lakini haikutosha kiongozi akatuchagulia tena kiongozi mwingine, huyu sasa ndiye hasa aliyechangia big time kutufikisha tulipo, lakini na yeye pia akatuchagulia kiongozi tuliye naye sasa, OH my God!

Now here we are, a confused nation with absolutely no idea tunachofanya, then comes wananchi kama wewe na ku-act as if you are from the Mars, kwamba haya matatizo tuliyonayo yameanza jana au juzi, kumbe unajua ukweli kuwa ni malimbikizo ya uongozi mbovu toka tulipopata uhuru, na wananchi tusioelewa kitu kuhusu nchi yetu wenyewe! Idea ya kuiweka CCM mbele kuliko taifa be honest mkuu viongozi wetu wameitoa wapi kama sio kwa waliowatangulia? Wakati hizi tabia zinapandiwa mbegu wananchi tulikuwa so happy about it bila ya kujua kuwa zilikuwa ni mbegu mbaya sana kwa our nation's future, kuna waliojaribu kuonya lakini wakatupwa na tukaambiwa ni viongozi wabaya sana na hawafai, sasa kwa sababu alisema tuliyemuamini na taifa letu ikawa amina, we never questioned the leader, I mean haiwezekani kuwa viongozi kuanzia Kambona, Karume, Bibi Titi, Eli Anangisye, Kassanga Ntumbo, Chief Fundikira, Bakari Seif, Seif Hamadi, Aboud Jumbe, Dr. Masha, walikuwa hawana vision au akili ya kujua kuwa baadhi ya maamuzi yaliyokuwa yakifanywa huko nyuma yalikuwa na madhara mbele ya safari,

Mkuu I can go on and on, lakini the messaage is the same kuwa hatuko hapa kwa bahati mbaya, na wote yaaani taifa zima tumehusika kwa njia moja au nyingine kufika tulipo, sasa tunahitaji kutafuta njia za kujitoa tulipo, lakini still either hatuelewi how, au hatuaminiani kiasi kwamba tuko radhi kuwaacha hao hao waliohusika kwa karibu kutufikisha hapa tulipo waendelee na uongozi, I mean CCM ni chama cha siasa sio cha dini au charity, so is Chadema au CUF, sasa kama kila anyeeenda kuingia kwenye uongozi anaishia kuwa sawa na wale wa zamani, inasema nini kuhusu sisi wananchi?

Mkuu ninakubaliana sana na analysis yako nzito kuhusu CCM, isipokuwa tu nina tatizo kuwa hukuangalia deeep kuona matatizo ya viongozi wetu ndani ya CCM yametokea wapi, na pia hutoi mapendekezo ya kutosha of what to do next, maana nina wasi wasi kuwa hiyo inaweza kutufanya wote tukawa part of the very problem we are trying to address, kwa sababu hatutoi applicable solution ambazo ni fit kwa mazingara yetu kijamii na kisiasa, na pia hatusemi na kukubali kuwa tumefikaje tulipo.

Sikusema kuwa CCM inachofanya ni sawa, isipokuwa nimesema kuwa tuwapewe nafasi kwanza, maana recently angalau wameonyesha kuanza kubadilika pole pole, as opposed na kasi ambayo tungependa wawe nayo kwenye kubadilika.

Ahsante Mkuu

Mkuu FMES,

Historia inasema dhahiri tuliburuzwa, je ni mpaka lini tutalia "utumwa" wa mawazo bila kuamka na kufanya mageuzi? Hata kama tulikulia katika "utumwa na unyonge" wa mawazo, ni vipi basi kila aliye kiongozi wa CCM ana kaugonjwa hako?

Mbaya zaidi ni kule kudanganyika kwa umma na unachokisema kuwa tumelelewa na "utumwa na unyonge wa mawazo", lakini CCM ya sasa inajua wazi kuwa FMES na wale 80% bado wanaamini kuwa wao ni "watumwa na wanyonge" wa mawazo hivyo tutumie vigezo hivyo hivyo kuhalalisha uharamia na ubabe wa chama kwa kujenga hofu kwa yule ambaye atakikosoa chama au kutishia usalama wa nchi kwa kuwaambia hawa "watumwa na wanyonge" kuwa mkichagua mwingine ambaye hana "baraka" zetu, mtaangamia!

Kina Kisori, Butiku, Iddi Simba, Anna Kilango, Mwakyembe na wengine ambao ni CCM ambao wameamka na kuanza kuhoji yale matumizi ya uonevu ya uongozi wa CCM wa kufanya kila mtu ni lazima awe "mtumwa na mnyonge" wa mawazo au kauli ni dalili wazi kuwa kuna mwamko mpya na ndio huu naushangilia.

Ni kweli hata Butiku na kelele zake zote si mtu kamili asiye na walakini, lakini kutoka kwake mekoni na kutamka wazi udhaifu wa chama ni swala la kupongezwa na si kukehebehiwa. Ilhali ni sawa na Mama Kilango au Kisori ambao sasa wanapata nguvu na sauti na kugundua kuwa "Utumwa na Unyonge" ulikuwa ni wa kujitakia na ulikomaa kutokana na mazingira ya awali.

Tulishafika pabaya, jahazi likagota mchangani, lakini wengine tumeamka na tunadai kwa Sauti za juu, tena kali zikiandamana na vinubi,baragumu na zumari, tunasema "enough is enough! Ndio maana hata nikatoa hoja kwa Kikwete kumsema kuwa "kosa ni kurudia, kulinda na kuendeleza makosa"!

Mimi sikimbilii historia tena au kuuliza fupa lililomshinda Mwalimu, Mwinyi na Mkapa eti limshinde Kikwete. Infact sasa hivi, kwa sauti zetu na uzalendo, tunampa Kikwete na wenzake wa CCM (hata upinzani) nyenzo za kutosha sana kuleta mageuzi ambayo yatamkomboa Mtanzania katika Utumwa na Unyonge ambao umemdumaza na kumfanya aendelee kunyanyaswa na Umasikini, Ujinga na Maradhi.

Swali kwao walioko Butiama, je pamoja na kasi yenu ya kudai mjisafishe na kuwa waadilifu, je mko tayari kubadilika na kuwa wenye mambo endelevu kwa maslahi ya Taifa na si maslahi ya Chama chenu?

Nitamjibu Kitila na Mkandara; Katiba ya CCM, Ilani zake za Uchaguzi, Miongozo na hata madniko na sera nyingi, zina kipa Chama kipaumbele kabla ya Serikali. Ndio maana nimehoji NEC na CC kuwa na nguvu kubwa kuliko Bunge! Kila tamshi wanalotoa CCM ni kuhusu Chama chao, its about them, only them and nation comes second!

That attitude needs to change and it is only the CCM leadership will be able to change such mentality and attitude. If they make those changes and stick to them, you will start seeing progress being made, Serikali will become Serikali ya Wananchi na si ya CCM na uwajibikaji kwa mujibu wa Katiba na Sheria za NCHI utarudi.

As of now, loyalty ya watendaji wa CCM na nidhamu yao ni kwa kuogopa vikao hivi viwili vinavyofanyika sasa hivi Butiama!
 
Mkutano Butiama: Agenda ya ufisadi yaigawa CCM
* Wenyeviti wa mikoa wataka ijadiliwe NEC, wengine wapinga
* Kikwete akiri kikao chao kitatoa maamuzi mazito


Na Theodatus Muchunguzi, Musoma


WENYEVITI wa Mikoa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walikutana juzi usiku mjini hapa kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) jana mchana katika kijiji cha Mwitongo, Butiana mkoani Mara likiwamo la kuwachukulia hatua wanachama wanaotuhumiwa kuhusika na kashfa ya ufisadi.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa katika kikao hicho, zinaeleza kuwa wenyeviti hao walitofautiana kuhusiana na suala la chama kuwachukulia hatua za nidhamu baadhi ya viongozi ambao wanahusishwa katika kashfa za ufisadi.

Kundi moja lilitaka viongozi hao wasichukuliwe hatua na badala yake wapewe kalipio wakati kundi lingine linataka waadhibiwe.

Baadhi ya wenyeviti walitaka kikao hicho kiweke msimamo wa kuishinikiza NEC

kuwatimua wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamehusishwa na kashfa hizo, ikiwemo ya kushindwa kuwajibika kutokana na serikali kuipatia kwa upendeleo kampuni ya kitapeli ya Richmond kwa ajili ya kuzalisha umeme wa dharura.

Hata hivyo, alipoulizwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara, Charles Makongoro Nyerere, ambaye alikuwa mwenyekiti wa muda wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mativila, kuhusiana na ajenda hiyo, alisema hapakuwepo na ajenda hiyo isipokuwa kuna baadhi ya wajumbe walitaka suala hilo la mafisadi lijadiliwe na kuweka msimamo mmoja.

Alisema yeye kama mwenyekiti wa muda aliikataa ajenda hiyo na kuwaeleza wenyeviti wenzake kuwa ajenda ya kikao ilikuwa moja, ya kuwachagua viongozi wa umoja wao na kuwahi kumaliza kikao hicho ili kwenda kushiriki katika harambee ya kukichangia fedha CCM Mkoa wa Mara juzi usiku, iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete mjini Musoma.

Licha ya kusema kuwa aliizima ajenda ya kushinikiza mafisadi kuchukuliwa hatua, Makongoro alisema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakieneza habari kuwa yeye alikuwa anaendesha vikao kwa ajili ya kushinikiza watuhumiwa wa ufisadi wang'olewe katika chama hicho, akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ambaye alijiuzulu kufuatia kashfa ya Richmond.

Alisema wanaofanya hivyo wana lengo la kumchonganisha na viongozi hao na kuongeza kuwa yeye anamheshimu sana Lowassa.

Mwenyekiti huyo wa Mkoa wa Mara amesema kuwa msimamo wake ni kuwa kama kuna viongozi waliohusika na ufisadi hawezi kuwatetea wasichukuliwe hatua.

Kikao hicho pia kilichagua Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Ali Mchopa alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa wenyeviti hao, akijaza nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pancras Ndejembi ambaye alistaafu mwaka jana.

Kikao hicho pia kilimchagua Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Lucas ol Mkisi kuwa katibu wao.

Katika hatua nyingine kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC) ambacho kilianza juzi jioni katika kijiji cha Mwitongo, Butiama mkoani Mara, kiliendelea kwa siku ya pili jana asubuhi katika ukumbi wa Mikutano wa Mkoa wa Mara na kusababisha kuchelewa kuanza kwa kikao cha siku mbili cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).

Kwa mujibu wa ratiba, CC ilitarajiwa kukutana juzi wakati NEC ilitakiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia jana hadi leo kijijini Butiama.

Kikao cha CC kilianza juzi jioni na kuahirishwa kwa ajili ya wajumbe wake kuhudhuria hafla ya uchangiaji fedha kwa ajili ya chama hicho Mkoa wa Mara, iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.

Kikao hicho kiliendelea jana asubuhi na kusababisha kikao cha NEC kilichotarajiwa

kuanza saa 4.30 asubuhi kuahirishwa hadi saa nane mchana, na wakati kinaendelea watu wa vyombo vya usalama waliondolewa karibu na ukumbi, hali iliyotafsiriwa kuwa ni kudhibiti habari zisivuje.

Akifungua kikao cha NEC, Mwenyekiti wa CCM, Kikwete alifafanua zaidi sababu za mkutano huo kufanyika Butiama, lakini akakiri kuwa kitafanya maamuzi mazito ambayo hayatahusu mageuzi ya kisera wala kiitikadi.

"Kwenye kikao hiki, yatakuwepo maamuzi muhimu yatakayofanyika. Lakini napenda kusema kuwa maamuzi hayo hayatahusu mageuzi ya kisera au kiitikadi. Nalisema hili kwa sababu wapo watu wanaotumaini au wenye hofu kuwa hapa Butiama kutatokea tamko la kurudia tena kutaifisha mali na kuziweka njia kuu za uchumi mikononi mwa dola. Wapo pia wanaodhani tutatoa tamko la kulirudisha nyuma gurudumu la mageuzi ya kisiasa yaliyoleta demokrasia ya vyama vingi na uhuru mkubwa wa watu kutoa maoni yao.

Rais Kikwete alifafanua kuwa kikao hicho kitatafakari hali ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama katika chama na Taifa na kuwa katika kuzungumzia mambo hayo, yapo masuala makubwa yatakayojitokeza na kufanyiwa maamuzi.

Katika kikao hicho mambo lingine linalotarajiwa kutingisha ni suala la mwafaka wa Zanzibar kati ya CCM na Chama cha Wananchi CUF.

Waandishi wa habari walipomtaka Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba muda mfupi kabla ya kuendelea kwa kikao cha CC jana asubuhi kuhusu mambo yaliyojadiliwa na kikao hicho juzi jioni, Makamba alisema hana cha kueleza kwa sababu CC ina kazi moja tu ya kuandaa ajenda za kujadiliwa na NEC.

"Sina cha kuwaeleza kwa kuwa chama chetu kina utaratibu. Jukumu la Kamati kuu ni kuandaa ajenda za kupeleka kwenye NEC. Hata baada ya kikao hiki kumalizika, hatutakuwa na cha kuaeleza, taarifa zote zitatolewa baada ya NEC," alisema Makamba huku akivilalamikia vyombo vya habari kuwa vimepewa ajenda za NEC lakini vinaripoti masuala ya Karamagi, Msabaha.

Badala yake Makamba alisema kikao hicho kiliwateua makatibu 10 wa wilaya, ambayo hata hivyo majina yao yatapelekwa NEC kwa ajili ya kupitishwa.

Habari za ndani zinasema wakati wa kikao hicho, agenda hizo zilijadiliwa na kuangalia jinsi ya kupenyeza agenda za ufisadi wa akaunti ya nje ya Benki Kuu (EPA) na kashfa ya Richmond.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, kikao hicho ndicho kingebadili mwelekeo wa agenda na kupenyeza agenda hiyo.

Habari zaidi kutoka ndani ya chama zinasema hata mpango wa kumuita gavana wa benki kuu kutoa semina kwa wajumbe jana, kuhusu hali ya kiuchumi ilikuwa inalenga pia kutoa ushauri nini kifanyike katika suala zima la EPA ambalo limekitia chama cha mapinduzi doa kubwa.

Wakati huo huo, Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein jana alilazimika kuondoka kuelekea kwao Pemba kutokana na kufiwa na mama yake mzazi.

Dk Shein alitoka nje ya kikao na kusindikizwa na wajumbe wa CC baada ya kupata taarifa hizo, muda mfupi baada ya kuanza kwa kikao hicho mjini Musoma.
 
Back
Top Bottom