Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Kwanini Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

“Ugonjwa mpya unapoingia Watu huwa na uoga, UKIMWI ulipoingia kupitia Kagera ilikuwa ukikutana na Mtu mwenye UKIMWI unamkwepa, kulikuwa na Surua wakati inaingia ukiwa na Surua hakuna anayekuja kukutazama, kwahiyo niwahikikishie Watanzania ugonjwa huu utapita, tupunguze hofu”-Rais Magufuli baada ya kumuapisha Waziri Nchemba Chato
• •
“Waziri Mwigulu Nchemba nimekuapisha hapa uende mkacheki vizuri Maabara inayohusika na upimaji corona kuna vitu vingi haviko sawa, kulikuwa kila siku ni positive positive, namshukuru sana Katibu Mkuu mpya” - JPM
• •
“Tulifanya mambo kadhaa ili kujua ubora wa Maabara tukapeleka sampuli za wanyama, ndege na vitu vingine bila wao kujua, tukazipa majina ya Watu, tumepeleka sampuli ya mbuzi akawa positive, kondoo Negative, mapapai nayo positive, maana yake mbuzi,mapapai yote yana corona”-JPM

“Kama tunapeleka sampuli za wanyama zinakutwa Positive inawezekana wafanyakazi wa Maabara wanatumika na Mabeberu, kama mapapai, mbuzi yana corona WHO wanapaswa kufanya kazi kubwa ya ziada, kwa hili lililotokea lazima kuna Watu wameambiwa wana corona wakati hawana”
 
HIYO DAWA JAMANI INATIBU JE ANA USHAHIDI KAMA INATIBU!!! VIPI KUHUSU SIDE EFFECTS??
KAMA NI DAWA KWELI BASI NI JAMBO LA HERI
Tatizo hawapi ushirikiano WHO tutaisha kwa ujuaji
 
Hiyo maabara ya kupimia corona sio mali ya serikali, zimetengenezewa huko huko nje.
 
Mwambie atoke Chato, najua muziki wa corona ndiyo maana amejichimbia Chato! Anajua akitoka tu akakutana na watu amekwisha! halafu unasema bila aibu eti ni shujaa, Mwoga kama kunguru
 
Meko kanikumbusha yule spokesperson wa Iraq wakati US ilipovamia Iraq. Alikuwa akiitwa Tariq Aziz nadhani.

Marekani anawaua wairaq lakini Tariq anasema "tumewashinda wamarekani, hawatuwezi hata kidogo".
 
Una umri gani???
Inaonyesha chama chenu kinaendesgwa na watu waliokosa malezi stahiki utotoni...!!
Wewe ndio ulipeleka sampuli za mipapai kupima covid-19?
 
Kuna maswali mengi sana ambayo yanahitaji majibu.

Huu mhimili wa 4 (vyombo vya habari) ungekuwa huru, naamini majibu yangepatikana.
Swadaqta!

Ameminya uhuru wa vyombo vya habari. Nashindwa hata kumuelezea! Wallahi huyu jamaa wallahu aalam.
 
Brazilian President Bolsonaro rejects calls for coronavirus lockdown, says "we're all going to die one day"

Coronavirus: Brazil reports over 1,000 deaths

Nakumbusha tuu [emoji115]


I'm on that good kush and alcohol
 
Kuna mambo mengi ya kushangaza kuhusu Corona!. Kwanini watu wasizikiwe kwao?.
Kwanini Evod Mmanda amezikwa Mtwara kwa lazima ambao sio kwao!.
P

Hapa pana point kubwa sana.

Wafiwa wamzike ndugu yao walipoamua .lakini iwe chini ya usimamizi wa serikali.
Siyo kulazimishwa na serikali mahali pa kuzika.
 
Hv hizo sampuli za papai zilizopelekwa maabara zilikuwa kwenye damu au kwenye nini. Maana nadhani sampuli zote ziwe ni damu.

Yawezekana papai ikawa na damu pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…