Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Kwanini Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Mwe unafikiri itapata uteuzi wa ile nafasi iliyo wazi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kwamba corona haipo, ila watu wapuuzi wanatumia njia hio kutisha watanzania na kuongea vitu ambavyo vingine hata havina mantiki, hivyo mheshimiwa kuagiza dawa ni sahihi kabisa hajakosea hilo nampongeza. Binafsi hatuna mawazo tofauti juu ya "mabeberu", leo hii WHO wamekataa dawa ya Madagascar na nilijua watakataa kwa ajenda zao za siri na ovu kwa dunia hii, ila sisi tutazileta na zikionesha mafanikio tutaitumia watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aiseeee 🤣🤣🤣🤣🤣


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wala sio mambo ya dawa, mimi nahitaji ANITEUE tu niwe karibu naye, kwa mambo mbalimbali, naamini nitajifunza mengi kupitia yeye na pia naye atajifunza mengi kupitia mimi na elimu yangu "ndogo"

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo unayetaka kukaa karibu naye ni mgonjwa...
The old man is a psychopath and a bigot!
Hana cha kujifunza kutoka kwako...
He knows it all!!
 
Mnawasingizia tu mabeberu ,WHO ni shirika la Afya duniani kama wao anajua mabeberu wanafanya hivyo lini umesikia Mmarekani au Mchina au Mwingereza amesimama na kusema habari ya Corona ya TZ .Mkishindwa kufanya kazi yenu mnawasingizia mabeberu .Kama viongozi wa Africa wangekuwa smart ikiwemo yeye kama mwenyekiti wa SADC na EA wangekuwa na kitenge chai cha afya na sio kutegemea WHO mnaowaita Mabeberu.Ujauguliwa na mgonjwa hivi karibuni ndio tutajua system ya Afya Tz ilivyombovu.Sasa hivi mochwari zimejaaa na vitanda hospitalini .Juzi tumezunguka na mgonjwa mpaka tumekoma.Alipofariki ndio tuliomaliza zaidi watu walikufa na maiti mpaka kuanza kutoa harufu.Yeye angeongea mambo ya msingi jinsi serikali ilivyojipanga na issue za CORONA .
 
Inawezekana sikusikia vizuri, hivi leo ametoa update ya waliopona korona wangapi so far au hata waliopona pia kuna mkono wa mabeberu?
 
Nimemsikiliza Magufuli kwa makini, lakini sijaona la maana kwa taifa.
 
Kuna siku waTanzania watamkumbuka sana Magufuli na hawata mpata tena

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Wakuu Salaam;

Nipo nasikiliza tena mida hii hotuba ya Rais aliyoitoa leo wakati akimwapisha Waziri mpya wa Katiba na Sheria kupitia youtube.

Mheshimiwa katikati ya maongezi anakohoa. Nikafikiri ni hali tu ya kawaida.

Akakohoa tena, halafu akaendelea kuzungumza.

Akakohoa tena halafu akanyamaza kidogo halafu akaendelea kuzungumza.

Hii hali inaleta mashaka kwa afya ya Mkuu. Raisi muda wote afya yake inatakiwa kua imara na isiwe na dalili zozote za mashaka. Watanzania tunapenda Raisi wetu awe na afya imara wakati wote.

Madaktari mnaoiangalia afya ya Rais hakikisheni Mkuu wetu ana afya njema kila wakati. Anaposimama kutoa hotuba kusiweko na dosari yoyote kama ilivyoonekana leo.

Madaktari zingatieni hilo, Afya njema kwako Mheshimiwa.

Mods; uzi upo kwa nia nzuri tu.
 
Leo kakasirika sana kuna watu wamemuuzi kiongozi wetu
 
"Inawezekana hivi vipimo vyenyewe sio salama, vimetengenezwa kwamba vikipima watu 30 mmoja lazima akutwe na Corona.

Mimi ni mwanasayansi naelewa ninachosema. Natoa wito kwa nchi za Afrika zianze kufanya uchunguzi kuhusu hivi vipimo (test kits) maana hatujui nia ya waliovitengeneza.

Wapime hata wanyama, au wachukue hata sample ya ukuta, wataprove haya ninayoyasema (ukuta unaweza kukutwa na Corona). Waziri Nchemba nenda kachunguze hili".

“Tulifanya mambo kadhaa ili kujua ubora wa Maabara tukapeleka sampuli za wanyama, ndege na vitu vingine bila wao kujua, tukazipa majina ya Watu, tumepeleka sampuli ya mbuzi akawa positive, kondoo Negative, mapapai nayo positive, maana yake mbuzi,mapapai yote yana corona”.

“Oil ya gari tuliipa jina Jabir Hamza miaka 30 ikawa Negative, fenesi tuliita Sarah Samwel, Papai tulilipa jina la Elizabeth Anne mwenye miaka 26 likakutwa lina corona, kware Positive, mbuzi positive, kondoo negative, maana yake mapapai yote yapelekwe karantini!?, ajabu hii, maabara zina matatizo zichunguzwe”.

“Tusitishane, kama sampuli maabara inasema papai na fenensi yana corona, inawezekana papai lingekuwa na masikio lingeoza kwa uoga, Waziri Nchemba kachunguze, inawezekana hivi vifaa vimetengenezwa kwamba vikipima Watu 30 anayefuata ana corona, tuwe makini hata na hivi vifaa”.

“Waziri Mwigulu Nchemba nimekuapisha hapa uende mkacheki vizuri Maabara inayohusika na upimaji corona kuna vitu vingi haviko sawa, kulikuwa kila siku ni positive positive, namshukuru sana Katibu Mkuu mpya”

“Kama tunapeleka sampuli za wanyama zinakutwa Positive inawezekana wafanyakazi wa Maabara wanatumika na Mabeberu, kama mapapai, mbuzi yana corona WHO wanapaswa kufanya kazi kubwa ya ziada, kwa hili lililotokea lazima kuna Watu wameambiwa wana corona wakati hawana”.

“Mbuzi awe na corona, fenesi liwe na corona, ndege kware awe na corona, lazima tujiulize inawezekana kuna kitu fulani hakijaeleweka Tanzania na hata Duniani hakijaeleweka, natoa wito Wanasayansi Nchi nyingine wachukue sampuli za wanyama, ukuta na yoyote wataamini nachosema”.

“Wengine wanasema nipo Chato, kwani waliambiwa Chato sitakiwi kuwepo?, hapa si ndio nilipozaliwa na hata nikifa nitazikwa hapa kuna ubaya gani nikiwa Chato? Nikienda Moshi watasema nipo Moshi nimekimbia sijui wapi!, tuache siasa za ajabu” -JPM

“Wengine wako Dar es Salaam wanasema Watu wasiende Bungeni, na nimeagiza wasilipwe posho maana utalipwa kwa kazi uliyofanya, kuna mambo ya ajabu yanafanyika, sina imani na Mkuu wa Mabaara ya Taifa maana haiwezekani tupeleke sampuli za papai zioneshe zina corona”

“Kwahiyo natoa wito kwa Watanzania tusiogope, tuchape kazi, Wanasiasa waache kutumia corona kuleta manenomaneno, wanasema nifunge Dar es Salaam, sifungi nishasema”.

“Mtu anazungumza funga Dar es Salaam, funga Tanga, SIFUNGI! Ni lazima Watanzania tuendelee kuishi, na kiukweli hata siku za mbeleni nafikiria hata kuruhusu ligi iendelee,”

“Mambo ya kucopy na kupaste Nchi hii hatuwezi kuyafanya, wapo wenzetu waliofunga mipaka na shughuli za kiuchumi mnaona wanavyoteseka, sisi mpaka sasa tuna vifo vya corona 16, huu ni wakati wa kuwapima Watu imani hata Viongozi wa Dini, unawazuiaje Watu kwenda kuabudu na Msikiti au Kanisa haujajenga wewe!”

“Mkuu wa Mkoa wa Mtwara nikamuona siku moja anazungumza kwamba Mkuu huyu wa Wilaya (Evod Mmanda) amefariki hatuwezi kusafirisha atazikwa hapahapa, ilinisikitisha sana, haiingii akilini, kama Madaktari wanakwenda kuwaona wagonjwa wakiwa wamevaa PPE ili kujilinda na corona walishindwaje Viongozi wa Mtwara kuifunga maiti PPE na mwili ukasafirishwa DC akaenda kuzikwa kwa heshima kule kwao Moshi!?”

“Viongozi tusilichukue hili kwa papara, naamini corona ipo lakini sio kwa kiwango hicho na jinsi tunavyoichukulia Watu wanaweza kuzikwa hata mchana kwa umakini, mwingine nilisoma kwenye WhatsApp anasema funga masoko nikasema huyu Mtu ana akili kweli? masoko yakifungwa atakula wapi? na wabaya wetu wanataka tufanye hivyo”

John Pombe Magufuli
Rais wa Tanzania

#JPMChato

NOTE: Hii si mara ya kwanza kwa vipimo vya kupima COVID-19 kulaumiwa kuwa na dosari katika uwezo wake wa kupima Corona Virus.

Mataifa kama Afrika Kusini, Canada, Marekani, India na sasa Tanzania kwa nyakati tofauti yametilia shaka vipimo hivi kutoka China.

Nini maoni yako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…