Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Kwanini Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Kwanini Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Hakika kaongea vitu muhimu na ni wenye akili pekee ndio watatambua hilo
 
Imagine kula mbuzi alie kula papai
tapatalk_1545118502599.jpg
 
Aisee nimekaa nimefikiria sana kwa alichokifanya leo Rais Magufuli.
Nimekuja kugundua kuwa siku ile alipowaita wakuu wa vyombo vya usalama hakukosea maana aliwasisitizia kwamba kagueni vitu vyote vinavyotoka nje hata ziwe stick za meno kagua ili mradi tujue vinatoka wapi na tujue kama vipo salama, leo hii tunaambiwa vifaa vilivyopelekwa India vya kupimia Covid-19 vinafanya kazi kwa asilimia tano tu na wameamua kutokuagiza tena vifaa hivyo kutoka China.

Kitu kingine ambacho kimenifanya niwaze sana ni jinsi Magufuli alivyoamua kuutumia uwana Sayansi wake kwa kuamua ku-prove kweli kama majibu yanayotoka ni sahihi au tunachezewa kwa kupeleka maabara sample za vitu mbalimbali kama matunda na n.k Kwa akili ya kawaida huwezi kufikiria kama jamaa angefanya hivyo na hii inamaanisha nini ni kuwa jamaa kafikiria sana.

Mwisho: Watanzania wenzangu Wahindi sio wajinga mpaka wakatae vifaa vya wachina sasa inawezekana kwa wahindi kilichotokea ndo kama huku kwetu.
Hongera JPM
 
Hao anaodai hawana corona aliwapima yeye na kwa maabara zipi?
 
Mimi naelewa kwa nini Rais Magufuli anaweza kuwa frustrated sasa hivi, hata ungekuwa wewe nadhani hata ungepata uchizi.

Imagine umetumia miaka minne, umepambana we, ukatumia nguvu zote hadi za ziada kufanya kila utakacho, umefanya miradi mikubwa, wakati mwingine umeumiza hata wengine huku ukisema ni kwa maslahi mapana ya taifa, leo hii kanakuja ‘kaugonjwa’ tu kanataka kupukutisha yale yooote uliyotaka kufanya. Niambie kati yenu, nani asingekuwa frustrated?

Anyway, nimeona picha hii ya leo ya kuapishwa kwa Bwana Nchemba, nikasema hii ni social distance kabisa ya kiwango cha 5G!

64CE1F92-74CE-49E2-A182-780B14779367.jpeg

Na tena nasikia shughuli imefanyika hotelini, pembeni tu ya jiko, hakutaka hata mgeni afike nyumbani kusalimia? Anyway, mgeni mwenyewe alikuwa Bungeni juzi, hatujui atakuwa amebeba nini, nadhani tahadhari ni muhimu kuliko hatari. Hata mimi ningefanya hivyo, je wewe?

Watanzania, kusikia hamsikii, hata picha hamuoni?
 
Nakumbuka Mh.Mwigulu Nchemba alipo tumbuliwa alikuwa safarini na baada ya kutangazwa kuwa ametumbuliwa alinyang'anywa Gari njiani.Leo Baada ya kuapishwa ameambiwa aanze kazi hata huko barabarani.
Wadau imekaaaje hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naandika nikiwa na mahaba makubwa sana na furaha nyingi sana jinsi gani unaweza kua jemedari haswa katika kua mstari wa mbele kabisa kutuongoza katika mapambano ya hilo gonjwa.

Na sio gonjwa hili tu, yapo mengi ambayo umekua mstari wa mbele kukaa kama komandoo wa kivita na kua na msimamo thabiti, hata ulipokua unayumbishwa na wapige kelele umekua hauyumbi katika misimamo yako.

Ninaomba kwa dhati kabisa ya moyo wangu niwe angalau mshauri wako wa mbali, si karibu, najua labda wapo ambao watakidhi vigezo vya kua washauri wa karibu sana, ila mimi naomba niwe wa mbali tu angalau. Nadhani kwa elimu yangu ndogo hii naweza kushauri ama kufanya mambo mbalimbali kwa ajili yako na nchi ya Tanzania ili tuendelee kua mstari wa mbele kuinua uchumi wetu.

PM yangu iko wazi kabisa kwa ambaye atanikonekti na President wajameni, pia naomba ajue nampongeza kwa dhati hatua aliyochukua ya kuwasiliana na Nchi ya Madagascar kwa ajili ya dawa ya Corona, pia nampongeza kwa dhati kwa kuendelea kua POSITIVE juu ya hili jambo, nimegundua kweli watu wanatishana tu ukifungua media huko ni upuuzi tu unaandikwa yani watu wanawapanikisha watu bila sababu za msingi, lazima ifike mahali tuwe na msimamo thabiti na tusiyumbe, tuendelee kua focused na Mh Rais tunaendelea kuchukua mimi nikiwa mmoja wapo njia ya kujifukiza ambayo imeleta mapinduzi makubwa na naamini hili gonjwa litatoweka muda sio mrefu.

Asante sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ameongea point za msingi sana wanaobisha waje na tafiti kupinga majibu ya utafiti wa mzee
 
Back
Top Bottom