Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Kwanini Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Kiuhalisia ni president working from home. Na ni jambo la kawaida tu hata Usa huwa wanafanya ukifuatilia utapata jibu.
 
JPM awa mbogo. …… …… Ati nipo Chato, Chato ndio nitazikwa . ….. .. kila kitu mnafanya siasa, Mbatia huwa ananitumia message, amempongeza. …….. Wabunge wa Chadema wasiokwenda Bungeni kwa kususia hawatalipwa posho, wakalipwe na Mabeberu.

JF wachangiaji wengi wacheni wivu, Chadema inawapoteza.
 
Sitarajii kusikia mbinu za kupambana na gonjwa hili
Sitarajii kusikia mikakati ya kuhakikisha uchumi hauyumbi
Sitarajii kusikia lolote la faraja kwa Wahudumu wa afya walio front line
Sitarajii kusikia faraja au mikakati ya kusaidia waliopoteza ajira/ biashara kwa janga la corona
Sitarajii jema lolote toka kwa huyu kiumbe.
 
Mungu Ni mkubwa ,nimesikia live ,mubashara ...Rais anasema ,tumeshaishinda Korona.
Hii Ni katika hotuba ya kumwapisha Mwigulu Nchemba!
Wajinga watamsikiliza lkn matokea yatawapa majibu!
 
Matusi gani tena ?
Tunasubiri nukuu na video tuone na tusikie, labda masikio yetu hayakuwa kwenye hotuba wakati anahutubia.
 
Mkulungwa mtu wa kuangalia line sana yani. Baada ya kuzinyaka taarifa na nini tayari kashatuma mwewe akachukue dawa.
 
Nimeona nyuma ya mwigulu kuna viti kama vya baa, hili tukio limefanyika sehemu ya starehe? I mean Bar au Hotelini? Pia nimeona kitu kama swimming pool
 
Nimeangalia kupitia Channel ten, kifupi nimegundua huyu ni jasiri kweli kweli katika kushindwa.
 
Kiukweli watu wanaweza kubisha lakini ukweli unabaki kuwa ukweli kuwa Rais Magufuli ni chaguo la Mungu.

Ujasiri wa Dr Magufuli ni wa kinabii na kitume na hili naliona katika vitabu mbalimbali vya kiimani na inahitaji nguvu ya Roho mtakatifu kulielewa hili.

Naomba Mungu aendelee kumlinda Rais Magufuli ili aweze kuisaidia Dunia hasa katika wakati huu mgumu ambao viongozi wote duniani wanaiogopa Corona.
Naamini kabisa Tanzania ndio nchi ya ahadi.

Mungu mbariki Magufuli

Mungu ibariki Tanzania.
 
Mzee anavyoongea utadhani yeye sio Rais wa hii nchi.. yaani as if yeye ni mpinzani yuko anaikosoa serikali ya nchi ili apewe madaraka yeye.

Sasa huo utopolo wa maabara, hio si maabara ya serikali na yeye si ndio Rais sasa anatulalamikia sisi tumsaidie nini?
Jamaa kama nchi imemshinda aniachie hata mimi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…