Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Kwanini Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Kwanini Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Kwani Mufti ana uwezo wa kutoa amri kwamba waislam tusifunge?? Hiki ni kituko. Eti kamuhakikishia waislam wataendelea kufunga - does he have a clue what is he talking about?
BAKWATA yenu imeshapakatwa siku nyingi.
 
Nimeona nyuma ya mwigulu kuna viti kama vya baa, hili tukio limefanyika sehemu ya starehe? I mean Bar au Hotelini? Pia nimeona kitu kama swimming pool
Sasa point yako nini?
Unaacha kufata vitu vya maana unashughulika na ujinga.
 
Mzee anavyoongea utadhani yeye sio Rais wa hii nchi.. yaani as if yeye ni mpinzani yuko anaikosoa serikali ya nchi ili apewe madaraka yeye.

Sasa huo utopolo wa maabara, hio si maabara ya serikali na yeye si ndio Rais sasa anatulalamikia sisi tumsaidie nini?
Jamaa kama nchi imemshinda aniachie hata mimi.
Ukifunguliwa mashtaka ya uhaini utasema unaonewa?
Muwe na kiasi katika hizo bakuli zenu, hamu umii kuona wenzenu wakina Melo wakienda mahakamani kwa ajili yenu?
 
Hapa pana point kubwa sana.
Wafiwa wamzike ndugu yao walipoamua .lakini iwe chini ya usimamizi wa serikali.
Siyo kulazimishwa na serikali mahali pa kuzika.
Mkuu Chakochangu, kiukweli kuna mambo mazuri sana ya rais Magufuli, that makes sense, kiukweli mimi nimemkubali sana Magufuli na baada ya Corona naendelea kumsaka Polepole.
P
 
Isije kuwa ni mwendelezo wa kumislead wananchi na kuwapa matumaini hewa ili wasiamini vipimo vinavyotolewa na maabara.

Maabara yetu ni Biosafety Lab level 3. Haiwezi kuwa na madudu hayo anayosema. Hiyo sio maabara ya Huruma dispensary kule Bagamoyo au Isimila iringa.

Huyu jamaa sio wa kumwamini kabisa.
Mkuu kumbuka aliyesema ni rais? Rais anatuambia kuwa serikali anayoiongoza haiwezi ikafanya chochote Cha maana kwa watanzania unless niwe kinafanywa na Magufuli mwenyewe otherwise kitakuwa madadu matupu so tusikiamini
 
“Ugonjwa mpya unapoingia Watu huwa na uoga, UKIMWI ulipoingia kupitia Kagera ilikuwa ukikutana na Mtu mwenye UKIMWI unamkwepa, kulikuwa na Surua wakati inaingia ukiwa na Surua hakuna anayekuja kukutazama, kwahiyo niwahikikishie Watanzania ugonjwa huu utapita, tupunguze hofu”-Rais Magufuli baada ya kumuapisha Waziri Nchemba Chato


“Waziri Mwigulu Nchemba nimekuapisha hapa uende mkacheki vizuri Maabara inayohusika na upimaji corona kuna vitu vingi haviko sawa, kulikuwa kila siku ni positive positive, namshukuru sana Katibu Mkuu mpya” - JPM


“Tulifanya mambo kadhaa ili kujua ubora wa Maabara tukapeleka sampuli za wanyama, ndege na vitu vingine bila wao kujua, tukazipa majina ya Watu, tumepeleka sampuli ya mbuzi akawa positive, kondoo Negative, mapapai nayo positive, maana yake mbuzi,mapapai yote yana corona”-JPM

“Kama tunapeleka sampuli za wanyama zinakutwa Positive inawezekana wafanyakazi wa Maabara wanatumika na Mabeberu, kama mapapai, mbuzi yana corona WHO wanapaswa kufanya kazi kubwa ya ziada, kwa hili lililotokea lazima kuna Watu wameambiwa wana corona wakati hawana” -JPM
#MillardAyoCORONATZ
#JPMChato

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom