Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Kwanini Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Kwanini Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Kweli kabisa ni makini ila umakini zaidi ungehakikisha hizo hujuma hazitokei in the first place..., pia tuhakikishe mashine sasa hivi haisemi negative, negative, negative wakati ni positive
 
“Ugonjwa mpya unapoingia Watu huwa na uoga, UKIMWI ulipoingia kupitia Kagera ilikuwa ukikutana na Mtu mwenye UKIMWI unamkwepa, kulikuwa na Surua wakati inaingia ukiwa na Surua hakuna anayekuja kukutazama, kwahiyo niwahikikishie Watanzania ugonjwa huu utapita, tupunguze hofu”-Rais Magufuli baada ya kumuapisha Waziri Nchemba Chato

“Waziri Mwigulu Nchemba nimekuapisha hapa uende mkacheki vizuri Maabara inayohusika na upimaji corona kuna vitu vingi haviko sawa, kulikuwa kila siku ni positive positive, namshukuru sana Katibu Mkuu mpya” - JPM

“Tulifanya mambo kadhaa ili kujua ubora wa Maabara tukapeleka sampuli za wanyama, ndege na vitu vingine bila wao kujua, tukazipa majina ya Watu, tumepeleka sampuli ya mbuzi akawa positive, kondoo Negative, mapapai nayo positive, maana yake mbuzi,mapapai yote yana corona”-JPM

“Kama tunapeleka sampuli za wanyama zinakutwa Positive inawezekana wafanyakazi wa Maabara wanatumika na Mabeberu, kama mapapai, mbuzi yana corona WHO wanapaswa kufanya kazi kubwa ya ziada, kwa hili lililotokea lazima kuna Watu wameambiwa wana corona wakati hawana” -JPM
#MillardAyoCORONATZ
#JPMChato

Sent using Jamii Forums mobile app
akili ya kujificha kuogopa corona?
 
Hammaz,
Yaani mtu anadanganya hata kwenye Mambo dhahiri? Kwamba yeye Ni mtu wa kulaumu kila kitu kinachofanywa na wasaidizi wake, hivi kweli huyo ni rais wa nchi hii kweli? Mbona Kama hajui kinachoendelea?
 
Rais ni mjanja sana, kwenye maziko ya jaji kulikuwa na utitiri wa watu na yeye wala hakuhudhuria kwenye huo msongamano ila kwenye kuapishwa kwa Mwigulu ambapo yeye yupo kuna watu wawili tu![emoji2211][emoji2211][emoji2211]
 
Tulifanya mambo kadhaa ili kujua ubora wa Maabara tukapeleka sampuli za wanyama, ndege na vitu vingine bila wao kujua, tukazipa majina ya Watu, tumepeleka sampuli ya mbuzi akawa positive, kondoo Negative, mapapai nayo positive, maana yake mbuzi,mapapai yote yana corona”-JPM
Huwa hatuweki majina ya watu, huu ni uongo! Maabara do not deal with names they deal with sample lab numbers.
 
.
tapatalk_1588447293763.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mambo mengi ya kushangaza kuhusu Corona!. Kwanini watu wasizikiwe kwao?!.
Rais Magufuli amemshangaa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kutangaza kumzika Evod Mmanda Mtwara badala ya kwao Moshi, akauliza kwanini Evod Mmanda amezikwa Mtwara kwa lazima ambao sio kwao?!. Rais akasema hata kama ni kweli mtu amekufa kwa Corona, kwanini mwili usihifadhiwe vizuri na PPE kisha ndugu zake wapewe mwili wa ndugu yao wakazike?!.
P

Hahahahaha, dah.
 
DURACEF, It's well noted by everyone herein,so this imply that nothing pertaining his Excellency you will concern about, I thank you for your decision,well! But unfeigned, psychologists advice!!

Don't take decision while you're in a happier mood eg you're deadly alcoholized ,

Also avoid taking actions or any while you're in baddest mood eg,someone hurt you,

It's my hope that none of the two above you're!!

This is an alarm to your decisions, I eulogize!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe unawashwa na nini kama nikionewa au nisipoonewa.. kama nimevunja katiba si uende ukafungue kesi au siku hizi mtu akifanya kosa anaulizwa kwanza kama anasema ameonewa au la.
Basi jiandae.....
 
Hana lolote anajaribu kuwatupia lawama watu wengine, kiufupi jamaa amefeli sana kwenye nafasi tuliyompa. Watu anaopambananao (wanaomtia hasira na ghadhabu muda wote) ambao sijui ni akina nani?, madhara yake yanawapata watanzania wote kiujumla.
 
“Ugonjwa mpya unapoingia Watu huwa na uoga, UKIMWI ulipoingia kupitia Kagera ilikuwa ukikutana na Mtu mwenye UKIMWI unamkwepa, kulikuwa na Surua wakati inaingia ukiwa na Surua hakuna anayekuja kukutazama, kwahiyo niwahikikishie Watanzania ugonjwa huu utapita, tupunguze hofu”-Rais Magufuli baada ya kumuapisha Waziri Nchemba Chato
• •
“Waziri Mwigulu Nchemba nimekuapisha hapa uende mkacheki vizuri Maabara inayohusika na upimaji corona kuna vitu vingi haviko sawa, kulikuwa kila siku ni positive positive, namshukuru sana Katibu Mkuu mpya” - JPM
• •
“Tulifanya mambo kadhaa ili kujua ubora wa Maabara tukapeleka sampuli za wanyama, ndege na vitu vingine bila wao kujua, tukazipa majina ya Watu, tumepeleka sampuli ya mbuzi akawa positive, kondoo Negative, mapapai nayo positive, maana yake mbuzi,mapapai yote yana corona”-JPM

“Kama tunapeleka sampuli za wanyama zinakutwa Positive inawezekana wafanyakazi wa Maabara wanatumika na Mabeberu, kama mapapai, mbuzi yana corona WHO wanapaswa kufanya kazi kubwa ya ziada, kwa hili lililotokea lazima kuna Watu wameambiwa wana corona wakati hawana”

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii maabara inayozungumziwa na rais ni ya private au insmilikiwa na serikali hii hii anayoiongoza? Au sample huwa zinatumwa nje ya nchi?je hivyo vifo 16 amejuaje Kama vimesababishwa na corona? Je kwanini asitangaze tu kuwa Tanzania hakuna corona badala yake anaagiza miti shamba toka Madagascar,sasa hiyo miti shamba atskunywa Nani wakati maabara haiaminiki?
 
Back
Top Bottom