Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Hapo kwenye red hapo umechemka, sidhani kama ndivyo ilivyokuwa, utatutia mashaka kama na wewe ni team makundi mkuu... tunataka genuine nutral analysis.
 
Heshima iwe kwenu wadau.

Baada ya kumsikiliza mtangaza nia namba 3 kutoka CCM ndugu Mwigulu Nchemba nimeingiwa na wasiwasi kidogo.

Kwa wale waliofuatilia na kumsikiliza mh. naibu waziri mtagundua kuwa Mwigulu alikuwa anaongea kama vile yeye si sehemu ya serikali.

Lakini cha ajabu zaidi mtakumbuka kuwa Hoja alizokuwa anaziongelea leo ni zile zile zilizokuwa zikiongelewa na wapinzani bungeni na yeye kuamka kuzipinga kwa kuwakejeli.

Kwa lugha nyepesi tunaweza sema kuwa Mwigulu katumia hoja za wapinzani kujinadi wakati ndye aliyekuwa mstari wa mbele kuzicrash hadi akasifiwa na Mwenyekiti wa chama na kupewa unaibu katibu mkuu bara pamoja na unaibu waziri kwa hiyo kazi.

Kwa lugha yepesi Mwigulu Nchemba tunaweza kumuita Chichidodo (Ndege mnafiki anayechukia kinyesi wakati chakula chake kinatokana na kinyesi)

Na hapa ndipo ninapopata wasiwasi kujua hasa nimwamini Mwigulu Nchemba yupi?!

1) Yule aliyekuwa anazipinga hoja za wapinzani?!

Au

2) Huyu aliyetumia hoja za wapinzani kutangaza nia?!
 

Sioni tatizo katika tamko la Mchemba kuhusu madawa ya hospitali yanayopashwa kuweko katika hospitali za serikali kukutwa katika maduka binafsi ya madawa. Ni ukweli usipingika kwamba maduka mengi ya madawa yaliyojengwa karibu na hospitali za umma yanauza madawa ya serikali. Ni aibu kwa serikali kwamba mgonjwa anaenda hospitali na kuelekezwa akanunue dawa zenye nembo ya serikali katika duka la jirani ambalo aghalabu ukiuliza mmiliki uataambiwa ni dakitari anayefanya kazi katika hospitali ya umma. Ni aibu namuunga mkono Mwigulu kwamba ikithibitika mahakamani kwamba dawa zilizokamatwa ni za serikali, duka lililohusika lifungwe na mmiliki apelekwe jela.
 
Kwanza..huyu jamaa...alikuwa..hana...mtiriko mzuri....kataka hotuba yake...alikuwa...analalamika...huku alikuwa mshauri wa Rais...nikagundua..ana tatizo la intellectual myopia ...anashindwa..kutupa..national interest itakuwa nn..??Amegeuka mlalamikaji....
 
Watanzania bwana!! Urais siyo kuongea vizuri. Kuongea vizuri kunaweza kumsaidia mgombea kuwaaminisha watu kuhusu uwezo wake especially kama hammfahamu. Kwa bahati nzuri hawa watu tunawafahamu vizuri sana, uwezo wao na mapungufu yao. Sasa badala ya kuwa assess kwa hayo tumeamua kutumia hotuba zao za leo ambazo hatuna hata uhakika kama ni wao wenyewe wamezitayarisha. Hivi kesho Lowasa akiongea vizuri kuliko Mwigulu kuna watu watabadili misimamo yao!?
 
Watu wanapotea sehemu moja tu...Mwigulu yuko kwenye serekali na wanalijua hilo wameshindwa nini kudhibiti hilo. ..kama sio kutuona majuha.

Issue ya MSD na deni wanalodai serikali anaijua vizuri..na pia anajua kwa nini hospitali dawa hazitoshelezi. ..yeye kuja hapa na kusema dawa zinaibiwa ni kujitoa ufahamu na kusema uongo.


In any rate mwananchi atie akili hamna jipya hapo hao wanalinda mfumo uliopo huwez kuendelea kuchagua ccemu alafu utegemee mabadiliko katika kuendesha serikali.

Kwa kushindwa kupambambanua mambo watanzania wataendelea kuburuzwa tu mpaka akili ziwakae sawa.
 

wewe na LIZABORN toka ile insu ya ESCROW mume kuwa wa uvugu vugu sana.mnashindwa muwe upande upi.
 

hivi huyu makongoro ni yule aliyewahi kuishi arusha? mwanasheria? sijui aliwahi pia kuwa mbunge? kama ndo huyo basi mwigulu ni bora mara 20
 
Duuu,haya bwana,ila mi nimeuona ni jembe sana,anafaa kuwa kiongozi wangu na namkaribisha kwa moyo wote aje kwetu Mvomero atangaze nia kwa mara nyingine,anajua sana

ile kushindwa kudhbiti sarafu against dollar ni udhaifu mkubwa
 
Tuache utani, na ushawishi Mwigulu hafai kwa lolote, hata uwaziri wenyewe unampwaya. Ni mtu hatari kwa umoja wa kitaifa: mtu ambaye yuko tayari hata kuua, ambaye hamuungi mkono. Kumbuka mauaji ya Arusha alipokuwa ameweka kambi, na kupoteza majimbo yote. Kwa ushauri wangu, Mwigulu apewe nafasi zaidi ya kuchunguzwa, atajifunua wazi jinsi alivyo.
Kwa maoni yangu anafaa kuwa jasusi, ajiuunge nao kama bado.
Watu tunaridhika tu akituimbiwa wimbo wake kuwa katoka familia maskini, kwani nani hakutoka huko?
Yupo ndani ya serikali iliyotufukarisha, na inaendelea kufukarisha anafanya nini cha msingi isipokuwa kutuhadaa na hadithi zake kuwa katoka familia maskini?
Tatizo tunasahau haraka.
 
So far katika wote wanaogombea, Upinzani na CCM kwa ujumla wake, naelekeaelekea kwa Mwigulu.

Ngoja nimsubirie na Mzee wa Utendaji, Magufuli.

huyu abaki tu kwenye utendaji, uongozi hauwezi.
 
Kwa hiyo kila jema likiongelewa na CCM ni idea ya upinzani?

Mwigulu ni jembe na ni kiboko ya upinzani, lazima mpanick..

Kwa wenye akili za kushikiwa ni wazi ataonekana jembe la mkono (la kuwekwa makumbusho)...

Ila wenye akili timamu lazima wahoji... Mbona mara nyingi anafanya personal cum criminal attacks hoja hizo hizo zikizungumzwa na upinzani..??

I really hate those who don't commit to use atleast 0.5% of their brains in as much as I disrespect politicians who deceive common wananchi....Hypocrites who can't walk their talk...!!
 

Mwigulu yuko sawa mkuu hili swala la madawa labda wewe ndo hulijuwi na mimi nilifikiria mwigulu ataenda mbali zaidi kwa adhabu na siyo kuishia jela tu.

Hizo chapa za MSD wewe tu ndo unazifahamu ukienda ospital ukiambiwa nunua dawa nje apo ni asilimia 0.0001% wanaolichunguza hilo la MSD. mara nyingi wanaoenda hospital za kawaida za serikali na kuamriwa kununua dawa ni wanyonge maskin ata elimu ya kusoma hiyo MSD hawana.

Binafsi nishaenda hospitali ya Serikali nikaelekezwa niende chumba katika vile vile vyumba vya milango ya mule hospital nigonge ntamkuta daktari ataniuzia dawa niliyoandikiwa nikafanya hivyo na kwa taarifa yako sasaivi mahospital karib yote ya Serikali bei za kununua dawa zimebandikwa katika milango ya hospital tunanunua dawa ndani ya jengo la hospital yaani ukiikuta hospital ya Serikali unanunua dawa duka lipo nje ya hospital saivi ni nadra haya mambo mkuu hayafichiki tena saiv ni waziwazi Mwigulu ameliona hili nimefurai kwamba ameahidi kulifanyia kazi akipata ridhaa.
 
Mwigulu ni mtu nae mwamini kuliko mtu yoyote, nikimwangalia kwa kimoyo naona anastahili % 100, nikimwangalia kimacho ni mtu ambae anania ya dhati kuijenga Tanzania tunayoitaka wananchi wa Tanzania. Binafsi nimekuwa nikimwangalia bungeni ni mtu ambae kwenye swala la wananchi ata kama limetoka upinzani nilimwona akiunga hoja kwa mwili na kimoyoni hata kama alikuwa pengine kimya. Kwenye ukweli tuwe wakweli Mwigulu anastahili kwa %100 kuwa Raisi wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania. Mungu akubariki usonge mbele.. haya ni maoni yangu na mtazamo wangu, na endapo akipitishwa na CCM ntampigia kampeni kwa jamii inayonizunguka kwa sababu nina ushawishi. Narudia tena Mungu akubariki ndugu Mwigulu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…