Hata Kikwete DHAIFU alikuwa na hoja yenye mashiko. "Nitaipitia tena mikataba ya madini ili kuhakikisha ina maslahi kwa nchi yetu" "Ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya" "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana" lakini alipoingia Ikulu akaweka kipaumbele kwenye ufisadi, kupokea pesa toka kwa marafiki zake AKA rushwa, kuwa VDG kiguu na njia na kuweka rekodi ya Rais aliyesafiri nchi nyingi za kigeni na pia aliyekuwa nje ya nchi yake kwa muda mrefu kuliko Rais yeyote yule duniani, kuwakingia kifua wezi, wapokea rushwa, wauza unga, majangili na kuwa na matanuzi makubwa ndani ya Ikulu. Kumbuka huyu kuna wakati aliitwa mpaka chaguo la Mungu kumbe si lolote si chochote naye ni fisadi tu. Watanzania tusirudie makosa ya 2005 ya kusikia hizi ahadi nzuri nzuri ambazo ni hewa na wakishaingia Ikulu ahadi zao wanaziweka pembeni kabisa. Ndani ya MACCM hakuna yeyote yule, narudia hakuna YEYOTE yule anayestahili kuliongoza Taifa letu.