Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

jana sikupata bahati ya kusikiliza kwa makini hotuba ya Lowasa, lakini leo asubuhi nimesikiliza hotuba ya wasira.. ki ukweli sikutarajia kama wasira angeweza kuja na hotuba nzuri (imekaa kiproffessional) so nikajua nchemba kwa kuwa yeye ni msomi wa kisasa, kijana na ameshaona makosa ya wenzake angekuja na hoja za maana na nzito kwa hiyo nikawa nasubiri kwa hamu sana na nikamsikiliza kwa makini.. but sikutarajia nilichokisikia... ameonesha udhaifu mkubwa kabisa hasa ukizingatia yeye ni msomi na kijana

1. Jambo la kwanza nililoliona toka mwanzo yule mc wake anaanza ni kuwa inaonekana nchemba hana kitu tangible cha kujivunia alichokifanya katika utendaji wake serikalini.. ndio maana wakawa wanazungumzia historia ya umasikini wake akiwa mdogo

2. kosa kubwa sana aliloanza nalo hakua amefocus kwenye sera na hoja zake.. akatumia muda mwingi kuwajibu wakosoaji wake kuwa hana uzoefu, na umri wake mdogo. nk
 
Chifu, hayo mabadiliko husiyategemee ndani na chini ya CCM.

Unawazungumzia vijana wanaokuja na sheria za kugandamiza freedom of speech? Unawazungumzia vijana wanatumia mbinu za kikomunisti kugandamiza upinzani? Vijana wanaotumia ofisi na mali za umma kujinufaisha wenyewe na familia zao? Vijana wanaotegemea kudra za wengine (a** licker) kupata nafasi za ubunge?!

Hamna vijana hapo! Ni vijana kwa sura na umri, ila wazee kwa fikra na matendo yao.

Vyama vyote haviwapi nafasi vijana wagombea wa CUF ni Maalim Seif na Lipumba,ukija CHADEMA ni Dr Slaa hawa wote wameshafikisha miaka 60.Bado mfumo wa vyama vya siasa za Tanzania hauwapi nafasi vijana kugombea nafasi nyeti
 
Hata ingawa mtu huwezi kuwa mahiri wa kila fani, kwa matangazi nia huyu inaonyesha kuwa ni hambiliki. Kama angelikuwa na busara na akili timamu, hotuba yake angeithibitisha na watu wa fani zote kabla hajaleta kwa umma. Lakini kwa sababu yeye ni hambilki, hataki ushauri kupata kwa watu ambao siyo fani yake. Raisi ambaye hambiliki hatufai
 
Hajasema uongo kwani madaktari huwa wanauza dawa za serikali. Na hiyo nembo ya MSD si inakaa kwenye makasha ya vidonge?? we umekula maharage ya wapi? So far Mwigulu amenishawishi kwa hotuba yake sio kama ma mvi ambaye haeleweki.
 
alikuwa anatafuta support ya wajinga ,mambo mengi aliyoongea ni ya kusadikika
TUTAWANYANG'ANYA LESENI, TUTAWAFUNGA JELA.

'Hakika usilolijua ni kama usiku wa giza" Nimeshangazwa sana na kauli ya Mh Mwigulu ambaye ni naibu waziri wizara ya fedha.
Ameonesha wazi hajui ni dawa gani zinazoruhusiwa kuuzwa kwenye maduka ya madawa ya binadamu katika nchi yake.

Siwezi kushangaa sana japo kanisikitisha kuona kiongozi mkubwa wa kitaifa hajui tofauti ya Dawa zinazokuwepo hospitalini na zile ambazo wamiliki wa maduka wanauza.

Kabla hajalizungumza hili kama mtia nia alitakiwa kujiuliza kwa wadau wa Afya wampe tofauti lakini pia hili jibu kuwa wao hawatibiwi hapa kwetu bali ni ughaibuni

Eti "Tutawanyang'anya leseni na kuwafunga" japo hao wamesomeshwa kwa kodi za wa Tanzania hawa si wengine ni madaktari, najiuliza huyu jamaa kala maharage ya wapi hadi anashindwa kuelewa dawa zinazomilikiwa na serikali zina nembo ya MSD na hizi haziuzwi katika la madawa kamwe.

Namshari afuatilie namna dawa hizi zinavyotolewa huko mahospitali na ajiulize kwanini madaktari wanawaonesha wagonjwa sehemu ya kununua kuliko kukurupuka.
Shame on u Mwigulu

Msema kweli haogopi kufungwa wala kufa

Dr Kilawa the Iron
 
Naomba Moderator wa Jamii Forum, arestrict lugha ya matusi. Sina tatizo kuchangia hoja hata kama siipendi. Tatizo langu ni wachangiaji wachace kupenda kutumia lugha ya matusi zaidi kuliko kuchangia hoja. Hili linafanyika kuhalalisha au kuponda jambo mahsusi kama vile kutangaza nia kwa wana CCM nje ya sehemu walikozaliwa. Sentensi zenyewe moja au mbili tu, na zote ni matusi. Technologia ipo ambayo ukipost hoja yenye contents za matusi, system inaireject mojakwa moja. Kwa wapenda maendeleo na uhuru wa kutoa mawazo jamii forum mmeifanyia jamii ya kitanzania jambo jema sana. Lakini hebu wekeza zaidi kwa kuongeza software application yenye uwezo wa kuchuja matusi. Google wanayo hii software. Inatumika kwenye nchi nyingi kama vile Japan, US na kwingineko.
Naomba nieleweke hapa. Matusi si mchango mzuri kwenye jamii.
Nenda huko japan
 
TUTAWANYANG'ANYA LESENI, TUTAWAFUNGA JELA.

'Hakika usilolijua ni kama usiku wa giza" Nimeshangazwa sana na kauli ya Mh Mwigulu ambaye ni naibu waziri wizara ya fedha.
Ameonesha wazi hajui ni dawa gani zinazoruhusiwa kuuzwa kwenye maduka ya madawa ya binadamu katika nchi yake.

Siwezi kushangaa sana japo kanisikitisha kuona kiongozi mkubwa wa kitaifa hajui tofauti ya Dawa zinazokuwepo hospitalini na zile ambazo wamiliki wa maduka wanauza.

Kabla hajalizungumza hili kama mtia nia alitakiwa kujiuliza kwa wadau wa Afya wampe tofauti lakini pia hili jibu kuwa wao hawatibiwi hapa kwetu bali ni ughaibuni

Eti "Tutawanyang'anya leseni na kuwafunga" japo hao wamesomeshwa kwa kodi za wa Tanzania hawa si wengine ni madaktari, najiuliza huyu jamaa kala maharage ya wapi hadi anashindwa kuelewa dawa zinazomilikiwa na serikali zina nembo ya MSD na hizi haziuzwi katika la madawa kamwe.

Namshari afuatilie namna dawa hizi zinavyotolewa huko mahospitali na ajiulize kwanini madaktari wanawaonesha wagonjwa sehemu ya kununua kuliko kukurupuka.
Shame on u Mwigulu

Msema kweli haogopi kufungwa wala kufa

Dr Kilawa the Iron

Mkuu labda na Mimi kama mdau wa biashara halali ya dawa za binadamu naomba niongezee kitu hapo!
Dawa nyingi zinazouzwa kwenye maduka ya madawa ni zile ambazo wamiliki hununua kwenye maduka ya jumla,yapo maduka na makampuni makubwa ambao huuzia wateja wao hawa ambao ni wamiliki wa maduka haya, Tena kwa sasa haya maduka ni modern na yenye dawa za kisasa kabisa kuliko hata hizo za hospitalini,Ukitaka kulijua hilo waulize wafanyakazi wa bima ya afya! Mara nyingi wagonjwa wanaoudumiwa na bima ya afya hukosa dawa wanazoandikiwa na madaktari na kuelekezwa kwenye maduka ya dawa yenye mkataba na bima ya afya kuwahudumia wagonjwa wao, Kwahiyo ingekua hizo dawa ni za serikali isingewezekana bima wakaingia nao mkataba wa kuwahudumia wateja wao, Dawa zote za serikali zizonapelekwa kwenye mahospital,vituo vya afya na Zahanati za serikali zina nembo ya MSD kitu ambacho ni rahisi sana kumkamata muuzaji wake.
Pia ieleweleke kwamba tabia ya kuuza dawa za serikali ni ya kizamani sana na kama ipo basi ni kwa wale wa vijijini ndani kabisa kwa watanzania wasiofaham lolote, Ukikuta mfanyakazi anafanya biashara kwa kuuza dawa za serikali basi ni njaa njaa tu zinzazomsumbua, mtu kama umeamua kufanya biashara kwanini uuze kwa kuficha ficha? Kwanini uuze kisicho halali?
Kwa maana hiyo tusiwalalamikie madaktari kuwapa maelezekezo wagonjwa wakanunue dawa mahali flani! Waende wapi wakati hospitalini hakuna dawa?
Ni jambo la kuwashukuru wamiliki wa maduka ya dawa maana ni msaada mkubwa sana katika jamii na sio kuwalalamikia wamiliki wa maduka ya dawa.Tuulaumu mfumo unaofanya dawa zisipatikane mahospitalini.
 
TUTAWANYANG'ANYA LESENI, TUTAWAFUNGA JELA.

'Hakika usilolijua ni kama usiku wa giza" Nimeshangazwa sana na kauli ya Mh Mwigulu ambaye ni naibu waziri wizara ya fedha.
Ameonesha wazi hajui ni dawa gani zinazoruhusiwa kuuzwa kwenye maduka ya madawa ya binadamu katika nchi yake.

Siwezi kushangaa sana japo kanisikitisha kuona kiongozi mkubwa wa kitaifa hajui tofauti ya Dawa zinazokuwepo hospitalini na zile ambazo wamiliki wa maduka wanauza.

Kabla hajalizungumza hili kama mtia nia alitakiwa kujiuliza kwa wadau wa Afya wampe tofauti lakini pia hili jibu kuwa wao hawatibiwi hapa kwetu bali ni ughaibuni

Eti "Tutawanyang'anya leseni na kuwafunga" japo hao wamesomeshwa kwa kodi za wa Tanzania hawa si wengine ni madaktari, najiuliza huyu jamaa kala maharage ya wapi hadi anashindwa kuelewa dawa zinazomilikiwa na serikali zina nembo ya MSD na hizi haziuzwi katika la madawa kamwe.

Namshari afuatilie namna dawa hizi zinavyotolewa huko mahospitali na ajiulize kwanini madaktari wanawaonesha wagonjwa sehemu ya kununua kuliko kukurupuka.
Shame on u Mwigulu

Msema kweli haogopi kufungwa wala kufa

Dr Kilawa the Iron

Mh Dr ni hilo tu umeliona? Hebu tupe mtizamo wako wa jumla. Nadhani hili Swala lipo ingawa inaweza isiwe general issue... bila shaka amekusikia na washauri wake wako hapa watamweleza.
 
Madaktari ni wezi sana wa dawa,,tena sio kufungwa tu INATAKIWA MNYONGWE KABISA,Mnasababisha vifo vya watu kwa kolukosa dawa mahospitalini.

Unategemea nini kama unampa mshahara ambao hauwezi kumfikisha hadi tarehe ya mshahara mwingine?

Hisani huanzia nyumbani, ndio maana hata jeshi lisipolipwa vizuri huanza kutumia rasilimali walizo nazo kukidhi hitaji lao.

Dawa sio kuwafunga au kuwafutia leseni, bali walipe vizuri kwa kupunguza anasa zinazofanywa na wanasiasa, muwekee msimamizi mzuri, mjali, halafu na wewe uliyemuajili kupitia kodi anayolipa kuwq na nidhamu katika matumizi yako.

Haiwezekani eti madawa yako hapo nosihamishie katika duka langu, wakati wewe mh. mwanasiasa unalipwa mishahara wa mwezi kama marupurupu yangu ya kustaafu na miposho juu kwa kukaa katika kujadili jambo amabalo sisi wananchi tumekuajili kwalo!

Wizi wa dawa, au wa aina yeyote katika sehemu ya kadi kwa maana ya kumwibia mwajili muda wa kufanya kazi na vifaa kamwe hautaisha kama hamta harmonize vipato vya wafanyakazi wa umma na wanasiasa.
 
Madaktari ni wezi sana wa dawa,,tena sio kufungwa tu INATAKIWA MNYONGWE KABISA,Mnasababisha vifo vya watu kwa kolukosa dawa mahospitalini.
Kama wanaiba na aliyewaajiri anaishia kulalamika nadhani tatizo Hapa nila mwajiri,
 
So far katika wote wanaogombea, Upinzani na CCM kwa ujumla wake, naelekeaelekea kwa Mwigulu.

Ngoja nimsubirie na Mzee wa Utendaji, Magufuli.
 
Jamaa alietoa post hii hakumuelewa Nchemba au anatetea bila kujua,dawa za serikali zipo hadi kwenye maduka binafsi na ile logo uwa ipo kwenye cover sio kwenye dawa hivyo sio rahisi kutambua ila wanatoa hospitali.
 
Hotuba ya Mwigulu itakuwa imemzimisha Lowassa ndiyo maana Team Lowassa hawaonekani hapa watakuwa kwenye kazi ya kumzindua msukule wao.

Ya Lowassa jana ilikuwa ni kama tamasha tu, sawa tu na wanayoyafanya akina Diamond na wanamuziki na waigizaji wengine.Haikuwa na chochote ambacho mtu angeweza kutoka nacho pale.

Ata washabiki wa Lowassa mioyoni mwao wanajua wametoka kapa jana, gharama kubwa lakin hakuna hoja.
 
Wanachojua watz kuhusu dawa ni kidogo sana,mimi ni mtumishi.

ktk hosp yetu hatujanunua dawa kwa mwaka mzima kwa kukosa fedha,tatizo la dawa sio wizi,na kama wizi upo basi ni kwa kiasi kidogo saana,mwaka mzima hatuja nunua dawa,utaiba nini......kuendesha hosp ni gharama kubwa saana....kwa mwaka mzima tumeishia kununua vifaa tiba,mfanya biashara wa dawa ana fulsa ya kupata dawa sehemu yoyote tz na nje ya tz,taasisi za serikali zinapata dawa MSD,orodha ya dawa Zinazopatikana MSD ni ndogo saana ukilinganisha na zilizoko kwenye market,kwenye market kuna Blister park kwa sasa, za serikali ni loose na nyingi ni zile za bei poa....niishie kusema watz wanajua kidogo saana kuhusu hili swala la dawa,na wangejua zaidi nadhani pangewaka moto......

Ndugu yangu umeongea vinzuri naona watu wanasema tu wasiyoyajua
 
Mtoa post naona bangi zimemkolea, kama katumwa mwambieni ukweli tunaujua. Mwigulu yuko sahihi
 
Namimi nitie neno hapa, Ni kweli kabisa hotuba ya Bw. Madelu ilijaa katika kina cha mawazo ya watanzani, yale ambayo Wapinzani wamekuwa wakiyapigia kelele katika majukwaa, na hata bungeni. Lakini hotuba hii haiakisi hotuba ya mtu anayetaka kuwa Rais wa dola hii, hutuba inalevo ya kiuwaziri, kiutendaji zaidi, kuliko kuangazia juu zaidi katika mgazi ya Taifa kwa maana ya SERA.

Ilikuwa hotuba bora kwa mtu anayeshindanishwa katika nafasi ya uwaziti mkuu na sio uraisi. Nilitegemea mambo ya rasilimali, mahusiano ya kataifa, Ukuzwaji wa uchumi na sio huu wa machinga na mama ntilie na kadhalika akioanisha na National Vision 2025 ambayo tunataka kufikia huko.

Nadhani anahita muda zaidi kuona anaweza kuaddress mambo yapi kama rais.
 
Hajasema uongo kwani madaktari huwa wanauza dawa za serikali. Na hiyo nembo ya MSD si inakaa kwenye makasha ya vidonge?? we umekula maharage ya wapi? So far Mwigulu amenishawishi kwa hotuba yake sio kama ma mvi ambaye haeleweki.

RUV ACTVIST katoa ufafanuzi mzuri katika comment zake ni jukumu lako kumfuatilia kwa makini ili uelewe
 
Back
Top Bottom