Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Heshima iwe kwenu wadau.

Baada ya kumsikiliza mtangaza nia namba 3 kutoka CCM ndugu Mwigulu Nchemba nimeingiwa na wasiwasi kidogo.

Kwa wale waliofuatilia na kumsikiliza mh. naibu waziri mtagundua kuwa Mwigulu alikuwa anaongea kama vile yeye si sehemu ya serikali.

Lakini cha ajabu zaidi mtakumbuka kuwa Hoja alizokuwa anaziongelea leo ni zile zile zilizokuwa zikiongelewa na wapinzani bungeni na yeye kuamka kuzipinga kwa kuwakejeli.

Kwa lugha nyepesi tunaweza sema kuwa Mwigulu katumia hoja za wapinzani kujinadi wakati ndye aliyekuwa mstari wa mbele kuzicrash hadi akasifiwa na Mwenyekiti wa chama na kupewa unaibu katibu mkuu bara pamoja na unaibu waziri kwa hiyo kazi.

Kwa lugha yepesi Mwigulu Nchemba tunaweza kumuita Chichidodo (Ndege mnafiki anayechukia kinyesi wakati chakula chake kinatokana na kinyesi)

Na hapa ndipo ninapopata wasiwasi kujua hasa nimwamini Mwigulu Nchemba yupi?!

1) Yule aliyekuwa anazipinga hoja za wapinzani?!

Au

2) Huyu aliyetumia hoja za wapinzani kutangaza nia?!

Umeongea ukweli yaan haya maccm manafiki kweli
 
Mnaweza kufanana malengo mkatofautiana ni jinsi gani ya kufikia hayo malengo. Acha wivu wa kike wewe hamna mtu kama mwigulu huko Ukawa wewe
 
Mimi amenishangaza mwingulu kuongea kama kiongozi wa kambi ya upinzania while yeye ni waziri

ama kweli dunia iko na vichekesho

Mapinduzi na upinzani bora utatoka ndani ya ccm. kwani wanajua fika na wanaona vizuri wapi wameburunda
 
Sisi watanzania ni wehu mana tunapo iamini tena ccm kwa kuipa ridhaa tena it means watz ni hakuna
 
Nimesikiliza vizuri na kwa umakini mkubwa hotuba za watangaza nia wote wanne wa CCM kwa kweli mtangaza nia aliyetoa hotuba nzuri na yenye ubora zaidi ni Mzee Wasira. Mwigulu kaongea vizuri sana lakini hotuba yake haifikii ubora wa hotuba ya Mzee Wasira. EL ni wakuhurumia maana ni kama mtoto.
HV wameshafika wanne au watatu?
 
Mwigulu ni miongoni mwa wanachama wachache sana wa CCM ambao unaweza ukatafuta kashifa zao ukashindwa kupata kashifa hata moja inayo mgusa,kama ilivyokuwa kipindi kile cha Mkapa alipo pitishwa na CCM,wapinzani wake walishindwa kabisa kumzushia kashifa kwa kuwa alikuwa hana kashifa yoyote.

Mwigulu akijitahidi kujitenga na baadhi ya mambo ya chama chake ambacho kimejaa viongozi wenyekashifa,hasa hili la kutumika na chama chake kutaka kuua upinzani ambalo linamfanya awe muongo,ana weza akawa kiongozi mzuri sana.
 
daaaah!! i wish mwigulu angekuwa ukawaa ingependeza xnaa but kwakuwa yupo kwenye mfumo mbovuuu basi muda c mrefuu naye atakuwa mchafu coz ya system ambayo yupoo
 
Aaaaah haya bana (hapo kwa red), tia nia tu wapiga debe wako tupo for free

BTW mi naangalia uwezo wa mtu siangalie hizo personals kama kunywa pombe, manake kama kunywa karibia wote wanakunywa pombe. Uhuru kenyatta anakunywa balaa lakini ndo rais wa kenya sasa, mzee warioba kajijengea heshima sana nchi hii lakini alikuwa mnywaji balaa enzi zile akiwa PM wa mzee ruksa

hapo kwa pombe kweli ni "minor" kama pombe haimfanyi mtu kupoteza heshima na hekima. Mfalme hatakiwi kulewa. Sifa ya pombe ikivuma kuliko ya utendaji ndo inaleta shida kama kwa yule mkuu wa wilaya hivi majuzi. Tatizo langu na makongoro ni hapo nilipomlinganisha na mbatia. tukisema tumtathmini kwa uzoefu wa uongozi tunaanzia wapi maana yeye anajitokeza akiona fursa laini ya kubebwa na si kupambana - yaani ni mtu wa on and off. Siasa kwake si career, anajifanyia tu sijui kama hobbie au niseme nini.
 
Aaaaah haya bana (hapo kwa red), tia nia tu wapiga debe wako tupo for free

BTW mi naangalia uwezo wa mtu siangalie hizo personals kama kunywa pombe, manake kama kunywa karibia wote wanakunywa pombe. Uhuru kenyatta anakunywa balaa lakini ndo rais wa kenya sasa, mzee warioba kajijengea heshima sana nchi hii lakini alikuwa mnywaji balaa enzi zile akiwa PM wa mzee ruksa

em niambie kidogo tu uwezo wa makongoro ukiacha sifa ya kuwa mtoto wa baba wa taifa, au tusubiri kwanza ahutubie?
 
Hii sheria yakila mtu kuwa nauhuru wakutangaza nia ya Unyerere inabidi iangaliwe upya mana imekuwa dharau kwa taasisi hii mhimu

Hakuna ubaya, watajichuja wenyewe by a natural process. Hata wewe nenda utangaze. who knows unaweza kupata
 
Hawa Jamaa wametoa hela wapi ya kurusha matangazo live kwenye channels kibao?

Kwani kurusha matangazo live kwa SAA 3 ni shilingi ngapi? Inaweza kuwa sawa na kukodisha chopa ? Tulia kaa chini umsikilize Rais akiongea, Viva Mwigulu
 
em niambie kidogo tu uwezo wa makongoro ukiacha sifa ya kuwa mtoto wa baba wa taifa, au tusubiri kwanza ahutubie?

Kuna uzi humu ulimuelezea vizuri sana, ila ninayokumbuka sasa ni:

1) hilo la kuwa amewahi kuwa mbunge wa arusha - jimbo ambalo linachukuliwa kuwa ni gumu kushinda kama hukubaliki, tena ukichukulia kuwa siyo mwana wa arusha

2) amekuwa mwenyekiti wa ccm mkoa wa mara kwa miaka 5

3) kwa sasa ni mbunge wa bunge la EAC

4) alithubutu kupinga hadharani vitendo vya ufisadi mwaka 2008 akishinikiza watu kujivua gamba


Nadhani 1-3 pia zinajibu swali lako kuhusu uzoefu wake ktk siasa za Tanzania

Ila nimegundua tunatofautiana kimtazamo kidogo. Tofauti niliyoiona kwako na mimi kuhusu Makongoro ni kwamba wewe unamwangalia kiushindani ziaidi, ndo maana unajaribu kumlinganisha na mwigulu au mbatia kiutendaji. Wakati mimi namuangalia katika mtazamo wa kuokoa chama na hii nguvu ya ukawa, ukizingatia ccm imeishachafuka sana usoni mwa watanzania kwa hizi skendo za ufisadi na rushwa.
 
Tatizo la wanasiasa wengi ni kueleza NGONJERA nyingi za mipango bila kujibu swali la msingi la HOW(Strategies ZINAZO TEKELEZEKA). Hatutaki kuambiwa nitafanya nchi iwe na this and that, iwe hivi na vile. Tunataka HOW utatekeleza hizo "this n that" zako.
Thats why nakuwa mtu wa mwisho kumuamini mwanasiasa wa AINA YOYOTE

Hauwezi kuwa umemsikiliza mwigulu
 
Back
Top Bottom