OME123
JF-Expert Member
- Oct 4, 2010
- 1,497
- 605
Heshima iwe kwenu wadau.
Baada ya kumsikiliza mtangaza nia namba 3 kutoka CCM ndugu Mwigulu Nchemba nimeingiwa na wasiwasi kidogo.
Kwa wale waliofuatilia na kumsikiliza mh. naibu waziri mtagundua kuwa Mwigulu alikuwa anaongea kama vile yeye si sehemu ya serikali.
Lakini cha ajabu zaidi mtakumbuka kuwa Hoja alizokuwa anaziongelea leo ni zile zile zilizokuwa zikiongelewa na wapinzani bungeni na yeye kuamka kuzipinga kwa kuwakejeli.
Kwa lugha nyepesi tunaweza sema kuwa Mwigulu katumia hoja za wapinzani kujinadi wakati ndye aliyekuwa mstari wa mbele kuzicrash hadi akasifiwa na Mwenyekiti wa chama na kupewa unaibu katibu mkuu bara pamoja na unaibu waziri kwa hiyo kazi.
Kwa lugha yepesi Mwigulu Nchemba tunaweza kumuita Chichidodo (Ndege mnafiki anayechukia kinyesi wakati chakula chake kinatokana na kinyesi)
Na hapa ndipo ninapopata wasiwasi kujua hasa nimwamini Mwigulu Nchemba yupi?!
1) Yule aliyekuwa anazipinga hoja za wapinzani?!
Au
2) Huyu aliyetumia hoja za wapinzani kutangaza nia?!
Umeongea ukweli yaan haya maccm manafiki kweli