KERO Kutoka halmashauri ya Busokelo, sijalipwa fedha zangu za uhamisho wala posho ya likizo tangu 2021

KERO Kutoka halmashauri ya Busokelo, sijalipwa fedha zangu za uhamisho wala posho ya likizo tangu 2021

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi niliajiriwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo mwaka 2021, nikifanya kazi katika Hospitali ya Wilaya. Baada ya miezi miwili nilipewa barua ya kuhamishwa kituo cha kazi, hivyo nikaandika barua ya kuomba posho ya uhamisho. Hata hivyo, hadi leo sijalipwa.

Nimekuwa nikiandika barua za kukumbushia, lakini hazijibiwi. Pia, kila ninapouliza uongozi kuhusu suala hilo, sipati majibu ya kueleweka.

Aidha, nadai posho ya likizo tangu mwaka 2024, lakini hadi leo bado sijalipwa. Tunaomba mamlaka husika itusaidie ili tuweze kupata stahiki zetu.

Pia soma ~ Naibu Waziri Qwaray: Waajiri wote lazima watenge bajeti ya kumlipa mtumishi pindi anapohama
 
Kama ulishahamia ulipohamishiwa endelea kupiga kazi hayo mengine samehe mkuu
 
Poleni sana ukiajiriwa ndo Kuna tabu hivyo ukijiajiri ndo yanakuwa mengine
 
Back
Top Bottom