Kutoka Ikulu ndogo ya Chato mpaka Ikulu ndogo ya Tunguu

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,517
Reaction score
3,399
Siku hizi Rais Samia anaenda Ikulu ya Chamwino iliyopi Dodoma mara moja kama kupokea wageni na kurudi zake siku hiyohiyo Ikulu ndogo Tunguu iliyopo Zanzibar.

Zamani sio sana tulikuwa na Ikulu ndogo ya Chato, bwana yule angeweza kukaa kule hata zaidi ya mwezi na hata nyakati fulani alimuapisha Waziri fulani hukohuko Ikulu ndogo ya Chato.

Sasa hivi tushasahau hayo, baada Uchaguzi Mkuu, Ikulu ndogo ya Tunguu ndiyo inayotajwa zaidi. Muda mwingi Rais Samia yupo huko.

Naombeni mnijuze, huko Ikulu ndogo ya Tunguu, ni makazi rasmi ya serikali kwaajili ya Rais au ni makazi binafsi ya kiongozi kama ilivyokuwa Ikulu ndogo ya Chato?

Naombeni mnijuze.
 
November yote alikua Dodoma, disemba Dom na dar,ila tunaambiwa anakaa sana tunguu
 
Nani sasa anaendesha nchi kama yupo Zanzibar kila siku; na makamu wake yupo angani kila kukicha. Ina maana tupo kwenye autopilot na Mwigulu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…