Kutoka Instagram: Mjue Bilionea wa Arusha anayedaiwa kumtoa mdogo wake kafara ili kupata utajiri

Kutoka Instagram: Mjue Bilionea wa Arusha anayedaiwa kumtoa mdogo wake kafara ili kupata utajiri

Mkuu Ms.Lincoln hili soma la pesa ni mali ya nani, ni refu sana mkuu, nikianza kukuhubiria hapa nitaharibu huu uzi. Lakini kwa kifupi tu ni kwamba dunia na vyote viijazavyo ni mali ya MUNGU ndiyo, lakini Ibilisi Shetani "alishajimilikisha" kila kitu.

Ushahidi kuwa shetani kajimilikisha vyote ni ile siku alipomchukua YESU na kumpandisha juu ya mlima mrefu na kumwonyesha milki za dunia na fahari yake yote kisha akamwambia kama ukinisujudia nitakupa fahari yote hii. Sasa YESU hakumbishia Shetani na kumwambia dunia ni mali ya MUNGU, bali alisema tu; "imeandikwa tumsujudie MUNGU peke yake".

Sababu YESU hakubisha kuwa dunia na fahari yake ni mali ya shetani, hii inaleta maana kuwa dunia na fahari yake ni mali ya shetani, tena YESU mwenyewe alisema itakuwa rahisi kwa Ngamia kupenya kwenye tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia kwenye Ufalme wa MUNGU. Isitoshe YESU alipoulizwa kuhusu kulipa kodi, aliwauliza je, pesa ina muhuri wa nani na picha ya nani? Wakamjibu kuwa ina picha na muhuri wa Kaisari, YESU akasema basi yaliyo ya Kaisari mlipeni Kaisari, na ya MUNGU mpeni MUNGU.

Maneno hayo ya YESU yanatosha kukuonesha kuwa Pesa ni mali ya Shetani na siyo mali ya MUNGU. Tena fahamu kwamba siku zinakuja Shetani ataichukua pesa yake yote na ataanza kuwapiga watu "muhuri" au "alama"(kwasasa hivi amezuiliwa kwa muda) na kila atakayetaka kuitumia pesa ni lazima awe na huu muhuri au hii alama, yaani "666".

Sasa ukitaka kujua kuwa pesa ni mali ya shetani, watu wa MUNGU wameambiwa kuwa wakati shetani atakapoanza kuwatia watu wake mihuri(666), wao wavumilie tu mpaka kufa, maana hakuna jinsi zaidi ya kuvumilia kama ni njaa au chochote kile, wavumilie mpaka mwisho.

Kuhusu mimi kutafuta pesa, ni kweli mimi nafanyakazi zangu na ninapata pesa ya kula na kubadilisha mboga, lakini sijisumbui kuutafuta "utajiri" na "ufahari wa dunia hii". Kuna tofauti kubwa sana ya "kula kwa jasho" na kujisumbua "kuutafuta utajiri na ufahari" wa dunia. Kumbuka hata YESU mwenyewe alikuwa "fundi Seremala" na alikuwa anapata pesa za kumudu maisha lakini hakuhangaika kuutafuta UTAJIRI. Hivyo fahamu tofauti ya kufanyakazi na kutafuta utajiri.
Sawa sawa.
Ila sijapenda kabisa mlivyommilikisha shetani pesa.Bora mngemmilikisha nyoka.
 
Nakuja na post yake
Kwa kawaida ile dawa inayotoka kwenye kibuyu hupakwa baada ya kuchanja chale, huyu hajachanjwa chale halafu anapakwa dawa za kwenye kibuyu!!! Labda uganguzi wa kimamboleo, lakini hapo ni wizi mtupu, yule kuku wa kafara hajashughulikiwa, wala kuonekana jinsi alivyotumika kwenye kuagua.
Hata yale manjonjo na majigambo ya mganga hayaonekani, lo salaleeee, mtu anaibiwa kweupeeeee na kitoweo kinapatikana bila kutumika kwenye kuagua!!
 
Back
Top Bottom