SUPER PREDATOR
JF-Expert Member
- Apr 29, 2014
- 2,093
- 725
Subiri kidogo wanakuja watu wa dini wataongea
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mafuriko ya MoNaBaN arusha leo
teh teh mkuu hii kweli ni katrina
Hawapondi ila wanadhibitisha kuwa Lowassa na ccm hakuna tofauti wote wezi, hivyo ni juu yako kuchagua Mwizi mwenye unafuu kwako.
Aiseeee jamaa katoa siri ya wapinzan kutoka nje
Hawa CCM kwa kweli sio wazima hata kidogo..yaani kuna jamaa kapanda jukwaani kwenye mkutano unaoendelea Iringa hakuna anachoongea tangu ameanza. Anasiliba upinzani tu na kutisha wananchi badala ya kunadi sera zao kwa wananchi. Ajabu ni wananchi wanaoshangilia ndio hawajielewi hata robo.... hakyanani hii nchi inawajinga wengi
Anasema Lowassa ni Mwizi, kila kitengo alichopewa aliiba, kuanzia Kwenye chama, wizarani Hadi alipokuwa waziri mkuu Lowassa ni Mwizi asilia.
Anasema yeye ndio kiboko ya Lowasa na Lowassa anamfaham vizuri tu.!
Habari wakuu,
Leo ni muendelezo wa kampeni, mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi ndugu Magufuli leo yupo uwanja wa Samora mjini Iringa. Tuwe pamoja kujuzana yanayojiri kutoka Iringa.
======
Anaeongea kwa sasa ni aliyekuwa waziri wa ardhi, ndugu William Lukuvi na anampigia chapuo mgombea anaewania ubunge jimbo la Iringa mjini ndugu Mwakalebela, pia anampigia chapuo mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi ndugu Magufuli.
Nape: Siku moja UKAWA walikuwa wanazindua mkutano wao Dar, nikiwa pale wakaanza kubishana Magufuli ametumia muda mrefu sana kuongea, nikawaambia mgombea wa UKAWA akifikisha dakika kumi na tano natoa milioni tano na nikazitanguliza, nikaulizwa ulijuaje, nikawaambia tatizo Lowassa anadhani Ikulu ni wodi ya wagonjwa.
Watanzania hatutaki Rais wa majaribio, ambae tukimwambia akakague majeshi yetu hawezi, tumchague tingatinga. Watanzania wameshaamua, hawawezi kupeleka fisadi Ikulu. Nakumbuka nilikuwa nahangaika na magamba, gamba namba moja Lowassa kashaondoka na chama kiko safi.
Kuna watu walikuwa wanakifanya chama chaka la kujifichia, wanaharibu katika serikali na kukimbilia katika chama wakiongozwa na Lowassa, tunaamini mabadiliko tunayoyataka ndani ya serikali na CCM tutayapata kwa ndugu Magufuli, katika orodha hakuna mtu alienistua kama Edward Lowassa. Nikasema na huyu fisadi anataka kwenda ikulu? Akasema hamuwezi kuzuia mafuriko, nikamwambia mafuriko yanazuiwa hata kwa kidole.
Mimi ni msemaji wa chama, kwanini hatukumpa nafasi mwizi? Hiyo habari ya ugonjwa anaijua yeye mwenyewe na tumuombee mungu tarehe 25 ashuhudie tunavyorudi Ikulu kwa kishindo!
Tunataka watuambie hata kazi moja tu ambayo Lowassa amefanya hakuiba, tulimpa uwaziri mkuu na miaka miwili tu Richmond, kazi gani ambayo tumempa Lowassa hakutumia madaraka yake vibaya na hakuiba? Mtu mwenye historia ya namna hii hatuwezi kumpeleka Ikulu, weka mbali na Ikulu.
Upande wa pili tunae Magufuli, nitajieni doa moja la Magufuli! Mbowe siku moja anasema vibaka wanachomwa moto, kibaka mkubwa Edward Lowassa yuko mtaani, leo amefika bei ya CHADEMA, wote kawatia mfukoni. Mzee Mtei kapigwa bilioni mbili, Mtei bilioni tatu na Msigwa ambae alisema atakaemuunga mkono Lowassa akapimwe akili. Sasa Msigwa tangulia mwenyewe ukapime akili yako mwenyewe.
Wakati wanajadili bei ya kuuzwa chama chao, Slaa alikuwemo ndani, nayajua mengi lakini leo nasema yanayomuhusu Msigwa, akaambie aende kufuta kauli akasema hawezi, akaambiwa basi nyamaza, akasema nipeni uji nishindwe kuinua mdopo, milioni 340 zikawekwa mezani ndio maana akipita anashindwa kumsema Lowassa na Magufuli, anabaki kusema nipeni kura. Uchungaji amesahau mtumishi huyu, tapeli mkubwa. Msigwa alisema watu wa Iringa msitumie bidhaa za ASAS, anaajiri vijana zaidi 400 Iringa na ndiye mlipa kodi mkubwa hapa Iringa. Anataka wale vijana 400 waje mtaani kuja kuwaandamanisha.
Tarehe 25 lazima tumwadhibu kwa kuhahakisha kura zote zinaenda kwa Mwakalebelela, wakati wa ujenzi wa barabara Iringa kwenda Dodoma, kambi ya Ujenzi ilitaka kuwekwa Iringa lakini ikabidi ikawekwe Dodoma akitaka eneo , kwanini! Msingwa. Sina mashaka Iringa tumemaliza, mwambieni pesa ziko wapi, pesa kidogo zilizobaki akale na mkewe, ya ubunge imeshaharibika.
Watanzania muombeeni mzee afya aone tunavyochukua nchi kwa kishindo, wanasema Nape alituambia bao la mkono, kelele watapiga sana lakini Ikulu inaenda kwa rangi za kijani, wenzetu wanahubiri mabadiliko, madadiliko ya kumuacha muadilifu tumpeleke mwizi, mabadiliko ya kumuacha mzima na kumpeleka marehemu. Kwa leo inatosha.
Magufuli
Anaeongea kwa sasa ni Magufuli na anawakosoa wale wanaosema serikali haijafanya kitu akiwemo mchungaji wa Iringa ambae aliamini anafata amri kumi. Anasema hata amani hamna chochote kilichofanyika! Anasema ni serikali hii hii ilileta vyama vingi 1992.
Sasa anaelezea kwanini ameomba urais ikiwemo kudumisha amani iliyopo na la pili ni kuafanya kazi na hatakuwa na blabla, analinganisha lami iliyoacha na mkoloni kwa miaka 76 na lami aliyojenga Kikwete kwa miaka 10. Pia anaelezea mipango yake ujenzi wa barabara njini Iringa ili magari makubwa yasikatishe Iringa mjini.
Anasema anafahamu hela ziko wapi na mapato hayo yatashuka chini kwa wananchi na anaeleza vipi atagharamia elimu bure mpaka kidato cha nne.
leo wasanii hawakuewpo nini maana naona maudhurio duni, hapo sa ndo mtaweza fanya tathimin vizuri, maana uwez fanya tathimin kwa kujaza wasanii
kuna kitu kimoja unajitia upofu....Kwa nini hawakumwadhibu(kwa kumshitaki mahakamani)muda wote mpaka alipoamua kuondoka mwenyewe..........Wananchi wanamchagua Lowasa si kwa kuwa ni kiongozi bora,bali kuiamsha na kuiadhibu CCM kwa kuwa kichaka cha kulea maovu kwa miaka yote hii.Kaa ukitambua hakuna kashfa yoyote mtakayozua sasa ionekane ni ''shocker''........