Elections 2015 Kutoka Iringa: Kampeni CCM uwanja wa Samora

Elections 2015 Kutoka Iringa: Kampeni CCM uwanja wa Samora

Habari wakuu,

Leo ni muendelezo wa kampeni, mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi ndugu Magufuli leo yupo uwanja wa Samora mjini Iringa. Tuwe pamoja kujuzana yanayojiri kutoka Iringa.
======



Anaeongea kwa sasa ni aliyekuwa waziri wa ardhi, ndugu William Lukuvi na anampigia chapuo mgombea anaewania ubunge jimbo la Iringa mjini ndugu Mwakalebela, pia anampigia chapuo mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi ndugu Magufuli.

Nape: Siku moja UKAWA walikuwa wanazindua mkutano wao Dar, nikiwa pale wakaanza kubishana Magufuli ametumia muda mrefu sana kuongea, nikawaambia mgombea wa UKAWA akifikisha dakika kumi na tano natoa milioni tano na nikazitanguliza, nikaulizwa ulijuaje, nikawaambia tatizo Lowassa anadhani Ikulu ni wodi ya wagonjwa.

Watanzania hatutaki Rais wa majaribio, ambae tukimwambia akakague majeshi yetu hawezi, tumchague tingatinga. Watanzania wameshaamua, hawawezi kupeleka fisadi Ikulu. Nakumbuka nilikuwa nahangaika na magamba, gamba namba moja Lowassa kashaondoka na chama kiko safi.

Kuna watu walikuwa wanakifanya chama chaka la kujifichia, wanaharibu katika serikali na kukimbilia katika chama wakiongozwa na Lowassa, tunaamini mabadiliko tunayoyataka ndani ya serikali na CCM tutayapata kwa ndugu Magufuli, katika orodha hakuna mtu alienistua kama Edward Lowassa. Nikasema na huyu fisadi anataka kwenda ikulu? Akasema hamuwezi kuzuia mafuriko, nikamwambia mafuriko yanazuiwa hata kwa kidole.

Mimi ni msemaji wa chama, kwanini hatukumpa nafasi mwizi? Hiyo habari ya ugonjwa anaijua yeye mwenyewe na tumuombee mungu tarehe 25 ashuhudie tunavyorudi Ikulu kwa kishindo!

Tunataka watuambie hata kazi moja tu ambayo Lowassa amefanya hakuiba, tulimpa uwaziri mkuu na miaka miwili tu Richmond, kazi gani ambayo tumempa Lowassa hakutumia madaraka yake vibaya na hakuiba? Mtu mwenye historia ya namna hii hatuwezi kumpeleka Ikulu, weka mbali na Ikulu.

Upande wa pili tunae Magufuli, nitajieni doa moja la Magufuli! Mbowe siku moja anasema vibaka wanachomwa moto, kibaka mkubwa Edward Lowassa yuko mtaani, leo amefika bei ya CHADEMA, wote kawatia mfukoni. Mzee Mtei kapigwa bilioni mbili, Mtei bilioni tatu na Msigwa ambae alisema atakaemuunga mkono Lowassa akapimwe akili. Sasa Msigwa tangulia mwenyewe ukapime akili yako mwenyewe.

Wakati wanajadili bei ya kuuzwa chama chao, Slaa alikuwemo ndani, nayajua mengi lakini leo nasema yanayomuhusu Msigwa, akaambie aende kufuta kauli akasema hawezi, akaambiwa basi nyamaza, akasema nipeni uji nishindwe kuinua mdopo, milioni 340 zikawekwa mezani ndio maana akipita anashindwa kumsema Lowassa na Magufuli, anabaki kusema nipeni kura. Uchungaji amesahau mtumishi huyu, tapeli mkubwa. Msigwa alisema watu wa Iringa msitumie bidhaa za ASAS, anaajiri vijana zaidi 400 Iringa na ndiye mlipa kodi mkubwa hapa Iringa. Anataka wale vijana 400 waje mtaani kuja kuwaandamanisha.

Tarehe 25 lazima tumwadhibu kwa kuhahakisha kura zote zinaenda kwa Mwakalebelela, wakati wa ujenzi wa barabara Iringa kwenda Dodoma, kambi ya Ujenzi ilitaka kuwekwa Iringa lakini ikabidi ikawekwe Dodoma akitaka eneo , kwanini! Msingwa. Sina mashaka Iringa tumemaliza, mwambieni pesa ziko wapi, pesa kidogo zilizobaki akale na mkewe, ya ubunge imeshaharibika.

Watanzania muombeeni mzee afya aone tunavyochukua nchi kwa kishindo, wanasema Nape alituambia bao la mkono, kelele watapiga sana lakini Ikulu inaenda kwa rangi za kijani, wenzetu wanahubiri mabadiliko, madadiliko ya kumuacha muadilifu tumpeleke mwizi, mabadiliko ya kumuacha mzima na kumpeleka marehemu. Kwa leo inatosha.

Magufuli
Anaeongea kwa sasa ni Magufuli na anawakosoa wale wanaosema serikali haijafanya kitu akiwemo mchungaji wa Iringa ambae aliamini anafata amri kumi. Anasema hata amani hamna chochote kilichofanyika! Anasema ni serikali hii hii ilileta vyama vingi 1992.

Sasa anaelezea kwanini ameomba urais ikiwemo kudumisha amani iliyopo na la pili ni kuafanya kazi na hatakuwa na blabla, analinganisha lami iliyoacha na mkoloni kwa miaka 76 na lami aliyojenga Kikwete kwa miaka 10. Pia anaelezea mipango yake ujenzi wa barabara njini Iringa ili magari makubwa yasikatishe Iringa mjini.

Anasema anafahamu hela ziko wapi na mapato hayo yatashuka chini kwa wananchi na anaeleza vipi atagharamia elimu bure mpaka kidato cha nne.





Viva magufuli viva
 
Last edited by a moderator:
WATAISOMA NAMBA:

Mgombea urais kupitia CCM Dr John Magufuli amewataka wanainch wa iringa leo wamchague kwa kura nyingi ifikapo tar 25/10 ili wale wapinzani wake waisome namba,magufuli amesema kuwa umati mkubwa uliokuja kumsikiliza unamuelewa na safari hii wataisoma namba kisawa sawa!!

Ataisoma yeye ajiandae tu hamna namna
 
Msigwa alipewa kikombe cha uji ili asipanue tena mdomo, kaisha
 
kweli ccm ni wasanii, kundi lote la bongo movie linapiga push up kumuingiza magufuli ikulu! kipaumbele lazima kiendelee kuwa elimu, elimu, elimu.
 
Viva magufuli viva

Naona mnaiga kila kitu toka zile NEMBO ZA CHADEMA na kauli mbiu yao,sasa mmekuja hata kwa wimbo wa msanii.Kweli mmekosa ubunifu.

Ila mwambie Nape UHAI na UZIMA ni Mungu anatoa.
 
Hatoshi yule mgonjwa

Waulize akina Celina KOmbani na Katibu wenu wa Wilaya ya Ilala kwa jina la Charles yuko wapi leo.

UTU na UBINADAMU upo palepale,UZIMA na UHAI atoaye ni MUUMBA wetu.Tusidhihaki kazi ya Mungu,Mungu hadhihakiwi.

Adhaniaye amesimama aangalie asianguke.
 
Sikio la kufa halisikii dawa. Nape atapata kiboko kikali kabla ya uchaguzi ujao, na asomae na afahamu
 
1. Magufuli aahidi kujenga barabara ya uwanja wa ndege wa Iringa na kuimarisha mifuko ya uwezeshaji ya wanawake na vijana.

2. Magufuli apania kupunguza ushuru kwa wananchi wa kawaida ili kukuza uchumi wa mtu binafsi kasha uchumi wan chi nzima.



12074864_893690027379560_800294550710482712_n.jpg


12049567_893690054046224_3844268741931817061_n.jpg


12038355_893690087379554_1804902182348431199_n.jpg


12038191_893690144046215_984207752500909091_n.jpg


12046641_893690164046213_6329644513760825455_n.jpg


12032133_893690194046210_6485283949180234099_n.jpg


12047200_893690274046202_7358172045992411990_n.jpg


Wakazi wa Iringa Mjini wakimsikiliza Mheshimiwa Magufuli katika Mtuno wa kutafuta kura za Urais.

MAGUFULI HAKAMATIKI : KATIKA HALI ISIYO YA KAWAIDA INAONYESHA MAGUFULI ANAZIDI KUNG'ARA KILA KONA YA NCHI YETU NI BAADA YA WATU KUPIMA SERA ZAKE NA ZA WENGINE NA KUGUNDUA KUWA SERA ZAKE ZINATEKEREZEKA NA ZA WENGINE HAZITEKEREZEKI BALI WANAZITUMIA KUWALAGHAI WANANCHI ILI WAINGIE IKULU TU : TUMESHTUKA HAPA NI KAZI TU

Iringa tumeshaamua kuifuta UKAWA bye byee Msigwa
 
Huwa nawaza hvi Nape huwa anawaza kutumia nn aiseee,kuna wakat unataman hata umtukane ila basi tu,Mungu anawaona wote wanaobeza afya ya Lowasa,ila cc tunampenda tu
 
Nepi ni mpuuzi sana, hata ameshindwa kujua kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi! Sijui kama ameshaandaa pa kujificha
Sawa Nepi huyo tumeishamfahamu na hatuna haja ya kumjadili. Kinachonipa tabu na kunisikitisha ni wananchi wanaokuwa wanawasikiliza watu kama hawa wakiporomosha mitusi na bado wanaendelea kuwashangilia!!! Je, ndipo hapo jamii ya kitanganyika ilipofikia? Je, ndio hayo jamii ya kitanganyika inataka kusikia? Je, tunawafundisha nini watoto ambao tunawavutia kwenye fiesta zetu hizi za kampeni kwa kuandamana na akina Diamond na Ali Kiba? Je, na akina Ali Kiba tundelee kuwaunga mkono kwa kuwa sehemu ya kuporomosha mitusi majukwaani?
Je, tutaelezaje hali kama hii ya kuwaita watu wazima 'maiti', wakati huo huo tuna msiba wa kitaifa kwa kuondokewa na waziri ambaye naye tunasikia wakati wa uhai wake alitumia mdomo wake vibaya, lakini sisi tunasema RIP? Ninajiuliza maswali mengi bila majibu! Ninaidieni hii jamii ya kitanganyika tena jamii maskini sana kati ya jamii maskini duniani inaelekea wapi?
 
[h=2][/h] Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akijinadi kwa Wananchi wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Samora, mjini Iringa.  Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, William Lukuvi akitangaza wasifu wa mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli wakati wa…
 
Ndugu zangu, mambo ni mengi ambayo magufuli anataka kuyafanya.. anataka kuleta maendeleo ya kweli na Tanzania mpya ambayo itawafanya wananchi wote wafurahie Serikali yao kuliko sasa.

CCM OYEEE
 
Back
Top Bottom