Kutoka Jinja Uganda: Kilimanjaro Queens wameshinda Kombe la CECAFA kwa kuifunga Kenya 2-1

Ta Muganyizi

R I P
Joined
Oct 19, 2010
Posts
5,355
Reaction score
2,736


Wadau najua wengi mna kiu ya kujua kinachoendelea kati ya timu ya Tanzania Bara Wanawake na Kenya wanawake. Hapa nipo mpakani maeneo ya Minziro mpakani mwa Tanzania na Uganda. Nimejaribu muda mrefu sikufanikiwa japo muda huu nimebahatisha mti mmoja ulioko juu ya mlima na kubahatisha matangazo ya mpira ya moja kwa moja kutoka jinja.

Updates:-
Mpira Umeisha : Tanzania 2 : 1 Kenya, Goli moja ni Mwanahamis Omary na Jingine ni Stumai Abdallah

Hadi kipindi cha kwanza kinaisha Tanzania ilikuwa 2 : 0 Kenya

Kipindi cha pili baada ya dakika nne Kenya wamepata bao mnamo dakika ya 49

Mpira unaendelea. Dakika 53 Tanzania 2 : 1 Moja, goli la pili kafunga Mwanahamisi Omary- Gaucho

Baada ya kufanya mawasiliano na KASIBANTE FM ya Bukoba nimeambiwa mnaweza kusikiliza live kupitia link hapo chini.

Anayetangaza ni Abdul Razak Majid(+255767 650076) ikiwa mie nitakata ghafla au umeme kukatika ghafla au matangazo kukatika bila kufikia mwisho muulizeni huyo Mtanzania Mzalendo awape matokeo

MPIRA UMEKWISHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA Tanzania Bingwa hadi mwisho Tanzania 2 : 1 Kenya Queens.

Ni CECAFA women Cup 2016...........Tanzania Queens Bingwaaaaaaaaaaaaaaaaaa

=====

TANZANIA Bara imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kwanza wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati mpira wa miguu, CECAFA Challenge baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kenya jioni ya leo Uwanja wa Ufundi (Uganda)

Wafungaji wa mabao hayo, Mwanahamisi Omar Gaucho na Stumai Abdallah la Kenya, limefungwa na Christine Nafula.

Tanzania walifika fainali baada ya kuwalaza wenyeji Uganda 4-1 mechi ya nusu fainali.
 
juu ya mti? radi mkuu....radi!
 
mkuu ubarikiwe, nami niko live na kasibante fm. kasibante maana yake nini?
 
mkuu ubarikiwe, nami niko live na kasibante fm. kasibante maana yake nini?

Mwana sijui maana yake nini labda nikupe namba ya huyo anayetangaza atakueleza maana yake. Mie hisia zangu zilikuwa zinanituma nielewe kuwa ni kifupisho cha mmiliki wa redio ambaye ni Khamis Kagasheki.....sasa sijui kama kuna uhusiano.
 
Asante kwa link, nausikiliza hapa redioni kupitia link
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…