Elections 2010 Kutoka kampeni za mwisho za CCM Jangwani

Ikionyesha wazi JK anakerwa na Dr. Slaa huku akikwepa kumtaja alimsengenya kwa kunuia kwenda Ikulu huku hata hana mke ila anategemea yule wa kuazima.....

Pia JK alihoji hoja za Dr. Slaa mbalimbali zikiwemo elimu bure, afya bure na kudai hazitekelezeki......

Katika khali inayoonyesha yeye ndiye mwasisi wa matangazo yaliyokuwa yanamchafua Dr. Slaa jana yaliyosambazwa na swahiba wake mmiliki wa kituo cha Channel Ten, JK alinukuu hitimisho la matangazo hayo aliposema hayo yamejaribiwa nchi nyingi lakini yalishindikana..............

Vile vile JK alihoji ahadi za treni iendayo kwa kasi na kusema hazitekelezeki na kuziita ni "absolutely ridiculous.................."

Kuwaita wenzie absolutely ridiculous ni kuwatusi kwa sababu maana yake ni wajinga......lakini usitegemee polisi aliyewateua yeye mwenyewe kumhoji juu ya hilo tusi la wazi kabisa la kuwadharau wenzie......
 
mmh, nilishinda hapa Moro naenda zangu kupanda basi nirudi bongo, niliondoka asubuhi kuepusha msongamano na huyu mkwere!! nitakua nikicheck updates via phone, msiniangushe basi. VIVA SLAA

Ok, updates za uhakika kuanzia keshokutwa asubuhi
 
Lakini hana ngoma kama EVA hawala wa JK wa Arusha..

hahahaha...hayo ni masuala ya gari la vipodozi kubeba kuwa karatasi za kura, CHADEMA bana hivi ninyi huwa mkiambiwa umbeya huwa hamuupitishi kwenye bongo zenu? juzi pia Slaa kakurukupuka na taarifa za matundu ya vyoo bila hata kuchuja karopoka.
 
katika hotuba yake ya mwisho amekuwa more energetic... lakini ni hotuba iliyotaka kuwadharaulisha Chadema na kuwafanya Watanzanai wakubali hali iliyopo kwa sababu wameshaizoea. Kwamba CCM ndio mmetuzoea mtuchague! Kwa kweli ujumbe ndio ulikuwa huo: Msitubadilishe ndio naona ambacho JK alitaka hasa kusema na sababu kubwa ni ile ile ya zamani "ni zimwi" lenu mlilolilozea.
 
CCM wasitudanganye, uongozi hauna uhusiano na mtu kuwa na mke au la, na kama ni hivyo tuanzie hukohuko CCM ambako BEN MKAA-HAPA na yeye aliazima mke wa mtu!!! nani aisyejua hili? tuangalieni hoja haya mengine hayana msingi, ningekua JK nisingeongea ujinga kama ule huku nikijua fika kuwa na mm ni wale wale, au tuanike uovu wa kila mtu????
 
Mwanakijiji, wale wazee ndo wamempa jk jeuri ya kutoa mipasho leo (ambayo haikuwa na maana yoyote kwangu zaidi ya kujihami na nonsense as usual), lakini above alll leo ndo nimemaliza ile chembe ya heshima nlokuwa nimebakiza kwa Mkapa.
 
@ Elli yeye mwenye mke (if he is commited in that marriage n he respects)katufanyia nini ambacho twaweza tembea kifua mbele kwa majivuno leo?
Hovyo kabisa, nyani haoni kundule kweli. Boriti jichoni mwake halioni, anaona kibanzi kwa mwenzie


anayoyafanya gizani asifiki hayajulikani.....
 
FANTA, nimekubali na nimeelewa ulichosema!!! so hakukua na haja yoyote ya kutaja mambo binafsi yamtu
 
hahahaha..juzi pia Slaa kakurukupuka na taarifa za matundu ya vyoo bila hata kuchuja karopoka.
MKAGUZI na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amemwagiza Mkaguzi Mkazi wa Mkoa wa Pwani kuzivalia njuga tuhuma zilizotolewa na mgombea urais wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, dhidi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwamba ilitumia Sh3.5 bilioni kwa ujenzi wa matundu 20 ya vyoo katika shule tano za msingi.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) juzi, Utouh alisema ameamua kufanya hivyo kwa kuwa fedha hizo zinatokana na Mpango wa Kuboresha Elimu ya Msingi (MMEM).
Dk Slaa alitoa tuhuma hizo hivi karibuni katika mkutano wake wa kampeni kwenye viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaa na kwamba, taarifa hizo zimo katika taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM na ahadi za Mbunge wa Bagamoyo, Dk Shukuru Kawamba, kwa Rais Jakaya
Kikwete.
Source

Unaona, watu makini hufanya uchunguzi kabla hawajasema, sio addict wa sisi em kama wewe anayeropoka bila kupima.
Jifunze kuficha upumbavu wako na kuachilia hekima yako!
 
Nipo stand ya msamvu-moro yaani mabasi ya dar hamna kabisaa, sijui ndo yaliyotumika kupeleka watu kwene kampeni za mkwere
 
FANTA, nimekubali na nimeelewa ulichosema!!! so hakukua na haja yoyote ya kutaja mambo binafsi yamtu
Mambo waloyazungumza ni mepesi mepesi yasokuwa na tija yoyote kwa taifa hili. Wametumia mda mwingi kumsema/kuwasema wagombea na mambo yao binafsi. Yaani ilikuwa kama huku uswazi kwetu watu wanamsema 'shoga' yao


Sikutegemea Mkapa culd spit that... Kweli siasa mchezo mchafu.
 
Nipo stand ya msamvu-moro yaani mabasi ya dar hamna kabisaa, sijui ndo yaliyotumika kupeleka watu kwene kampeni za mkwere
Pole sana, abood leo atakuwa biz na kijani na njano, panda 'hiace'.
 
Unaona, watu makini hufanya uchunguzi kabla hawajasema, sio addict wa sisi em kama wewe anayeropoka bila kupima.
Jifunze kuficha upumbavu wako na kuachilia hekima yako!



huo ndio ukurukupukaji wenyewe, kwanza bajeti ya halmashauri nzima ya b'moyo si zaidi ya bilioni 12, haingii akilini kwa mtu kama slaa kutoka hadharani na kusema matundu ishirini ya vyoo yametumia bilioni saba, lakini slaa anajua wapi kwa kupata taarifa sahihi na kwenye taarifa za utekelezaji wa ilani za wagombea(kwani kamati ya slaa aliyokuwa ana chair bungeni inahusika na nini hadi asijue). Sasa upuuzi kama huu anweza kuusema mtu tunayetegemea kuwa rais? Ungekuwa na akili timamu ungejua Utoh alimtukana sana Slaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…